Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

GLOBAL FAMILY ENLIGHTENMENT ORGANIZATION(GLOFEO) added a News update.

$
0
0

Watoto wakihamasisha wenzao wenzo kwa maandamano ndani ta mtaa wa matopeni, katika maandamano hayo watoto walionesha michezo ya kupuliza bubles zitokanazo na povu la sabuni yenye rangi.Michezo ya watoto ikiandaliwa mahali maalum, huleta maana na huwakutanisha na kujenga uwezo wa kuvumiliana. hapo juu ni maandalizi ya kutengeneza povu la sabuni iliyochanganywa na rangi kwa ajili kupuliza na kurusha bables angani. Mchezo huu ni sawa na ule tuliocheza zamani tukienda kufua nguo mtoni,unafikicha sabuni na kisha kupuliza katikati ya viganja na bables kuruka angani.Katika kudumisha mira na desturi, ngoma za asili zina nafasi kubwa ya kutunza kumbukumbu ndani ya ubongo wa mtoto. Hapa watoto wadogo wanacheza ngoma za asili.Ubunifu hutokana na kutenda, hivyo ni vipande vya nyumba vilivyosambaratishwa na vikiungashwa kwa ustadi unapata nyumba kamili. Watoto wakipewa kazi kama hii huongeza concetration power na uvumilivu katika kila jambo. Katika mradi wa nyumba ya michezo ya watoto, kuna kuunganisha viande vya picha mbalimbali kwa kufuata maelekezo ya picha. Katibu mkuu wa shirika hapo juu naye akijaribu kuunganisha vipande vya tembo kwa kufuata maelekezo ya picha.Hapo juu ni reli iliyounganishwa na treni ikitembea.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles