Kuweza kufanya kazi kwa maelekezo ya mchoro ni mbinu muhimu sana itakayowezesha kuwa makini karibu katika kila kazi.
Mzazi ni muhimu sana kufuatilia harakati za ujifunzaji wa mtoto,huweza kumjengea imani mtoto na kuongeza uwezo wa kujiamini.
Watoto kufanya kazi za ubunifu kwa pamoja hujenga hulka ya ushirikiano na kuthamini uwezo wa kila mshiriki.
Ujifunzaji kwa vitendo ni muhimu ili kupanua uwezo wa kupambana na changamoto za kila siku zinazojitokeza katika jamii.
Watoto na michezo hawawezi kutenganishwa,inafurahisha na kuongeza hamasa katika makuzi ya ubongo wa mtoto, na mtoto anapocheza na mzazi/mlezi humfanya kuona umuhimu wa kushirikiana katika nyanja mbalimbali, humpa mtoto pia nafasi ya kueleza hisia zake na ndipo mzazi anaweza kutambua karama zake na hivyo kumuonesha njia ya kufikia kule mtoto anakopenda.