CHANIKA TUAMKE YOUTH ORGANIZATION (CTYO)
Ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa rasmi tarehe 13/03/2005 likijulikana kama Tuamke Arts Group na kusajiliwa tarehe 15/01/2014 Katika wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia na watoto na kupata namba 00NGO/00006839
Shirika linatekeza shughuli zake katika kata ya Chanika na Zingiziwa wilaya ya Ilala Dar es salaam.Lengo kuu la {CTYO} ni kuwawezesha vijana kushiriki katika mipango,kusimamia na kuitekeleza ili kuleta maendeleo Chanya.
{CTYO} Inafanya shughuli za Ushawishi na Utetezi katika kuhakikisha utekelezajiwa haki ya Afya ya uzazi kwa vijana,Uzingatiwaji wa Maadili,Malezi na Huduma bora ya rafiki kwa vijana.Pia CTYO imelenga kufanya uchambuzi wa sera mbalimbali za vijana na kusimamia utekelezaji wake.
Shirika la {CTYO} zamani Tuamke Arts Group kupitia mkurugenzi wake ndugu Seleman Nyonde limejifunza shughuli za Ushawish, Utetezi ,Uandaji wa Mpango wa kazi,Uandaaji wa Bajeti,Utunzaji wa kumbukumbu,Namna ya kuendesha Semina,Namna ya Uwajibikaji katika NGO na Kuandaa aTaarifa na Uwasilishaji wake. n.k Katika shirika la AMREF na SIKIKA kwa kupitia nafasi ya kujitolea.
DIRA
Kuwa na Vijana bora wanaoweza kupanga mipango,kuisimamia na kuitekeleza ili kujiletea maendeleo chanya.
DHAMIRA:
Kufanya ushawishi na utetezi kuhakikisha kuwa vijana wanapata Afya,Maadili,Malezi na Huduma bora Rafiki kwa vijana katika jamii na serikali kwa ujumla na kuchambua sera mbalimbali za vijana na kuhakikisha kuwa sera hizo zinakwenda na wakati na zinafanyiwa kazi.
MALENGO YA CTYO
12.1 Kuwajengea uwezo vijana kujiajiri wenyewe
12.2 Vijana kujikwamua kiuchumi
12.3 Kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi
12.4 Kukuza vipaji vya vijana katika sanaa na michezo.
12.5 Kuelimisha jamii juu ya Afya kwa vijana
12.6 Kuhakikisha kuwa vijana wanapata masilahi yao katika ngazi zote za serikali na jamii .