Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO) updated its Projects page.

$
0
0
Afya ya Uzazi ni haki ya kijana Tuitetee! AFYA YA UZAZI NA UJINSIA KWA KIJANA KUTETEWA ni muhimu kama kweli twahitaji vijana wenye kujiamini na kusimamia malengo ya maisha yao katika jamii na taifa letu kwa ujumla. LAKINI, tujiulize, nini maana ya Haki, Afya ya Uzazi na Ujinsia kabla ya kwenda popote:- HAKI Haki ni kitu ambacho mtu au watu wanaweza kukidai kisheria. Mfano, Mtu ana haki ya kuishi, itokeapo kutishiwa kutolewa uhai huo basi ana uwezo wa kumshitaki mhusika kisheria AFYA YA UZAZI Ni hali ya mtu kuwa katika hali nzuri kimwili, kiakili na kijamii katika maswala yote yahusianayo na mfumo wa uzazi Kimwili: Hana tatizo katika viungo vya uzazi au madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya viungo hivyo. Mfano, magonjwa ya ngono, mimba za utotoni na VVU/UKIMWI. Kiakili: Hana tatizo katika mfumo wake wa kiakili kutokana na maswala ya uzazi. Mfano, Matokeo ya matatizo ya afya ya uzazi kama kuchanganyikiwa kutokana na kuwa na msongo wa mawazo sababu ya mimba za utotoni, magonjwa ya ngono na VVU/UKIMWI hasa pale wanapotengwa na jamii kwa ujumla au kujiingiza katika utumiaji wa dawa za kulevya na uuzaji wa miili sababu ikiwa ni hizo hizo Kijamii: Hana tatizo lakutengwa na jamii kutokana na tatizo lililoletwa na matumizi hatarishi ya viungo vya uzazi. Mfano, Kutengwa sababu ya kuwa na maambukizi ya magonjwa ya ngono, mimba za utotoni au VVU/UKIMWI. UJINSIA Mahusiano ya kijamii kati ya mwanaume na mwanamke au kijana na mtu mzima. Ni mahusiano yanayojengwa kutokana na utamaduni ambao umekubalika na jamii husika.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles