Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO) has a new discussion about Afya ya Uzazi ni haki ya kijana je, tutaweza kuitetea kwa kutumia mazingira yetu ya Asili?.

$
0
0
Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO): Kila panapo kucha vijana wanahangaika katika kujikwamua na changamoto mbalimbali zinazowahusu. vijana wanapambana na matumizi ya madawa ya kulevya, ukatili wa kijinsia, changamoto mbalimbali za kielimu katika shule zetu, Biashara ya ngono,kasi ya maambukizi ya vvu nk. katika nchi yetu vijana wanaongoza kwa zaidi ya asilimia 60% kwa kasi ya ongezeko la maambukizi ya vvu. hii inasababishwa na vijana wengi kukosa nafasi ya kujifunza kuhusu haki za afya ya uzazi na ujinsia ikiwemo changamoto za kiutamaduni zinazo ruhusu wazazi/walimu kuona aibu kuzungumzia hata kufundisha katika mashule/majumbani ikiwa sera na sheria zimetoa mwongozo wa kutoa mafunzo hayo kwa vijana! Hali ya wazazi kuona aibu inasababisha vijana kushindwa kujitambua na kupelekea kudanganyika kirahisi na hata kuambukizwa vvu. kinakwamisha nini ikiwa sera na sheria zipo? hakuna njia nyingine zaidi ya kusimama kwa pamoja kutetea utekelezwaji wa sera na sheria zilizopo, lakini pia kuwahamasisha vijana kutengeneza chaguzi sahihi katika uwajibikaji wao juu ya afya zao na kuwasaidia kutambua mahitaji yao yanayoweza kuleta mabadiliko na maendeleo kwao na jamii kwa ujumla. Tunaamini kuwa "AFYA YA UZAZI NI HAKI YA KIJANA TUITETEE na kwa pamoja tunaweza kuitetea.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles