Habari wadau,napenda kuchukua fursa hii ya kipekee kwa kutoa taarifa kwa wadau wote wapenda maendeleo nchini kwetu Tanzania.
ikumbukwe kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu,hivyo wadau yatuoasa tuwe mstari wa mbele kwa kuielimisha jamii iliyojiandikisha ijitokeze kupiga kura siku ya uchaguzi ambapo ni tarehe 25 oktoba 2015, na tuhamasishe wananchi kuwa uchaguzi huu uwe wa AMANI na HURU kwani amani ndio njia pekee ya kudumisha amani na utulivu Nchi yetu ya Tanzania.
wenzangu wana harakati tambueni kuwa sisi ni miongoni mwa wadau wakubwa tunoisaidia serikali kufika maeneo ambayo yenyewe serikali haijafika.
Ombi maalumu kwenu ni kuwa kusaidia kuelimisha wananchi wajitokeze kupiga kura kuongeza asilimia ya wananchi watakao shiriki kupiga kura kutoka 48.64% ya Mwaka 2010 hadi 86 au kuzidisha zile asilimia 86 za mwaka 2005.
Ndugu zangu wakati ni huu tusingoje kusukumwa ni wajibu kutekeleza majukumu haya lakini tuzingatie yafuatayo
1. Nchi ibaki kwenye utulivu na kuwepo kwa AMANI ya kudumu
2. Ulinzi na mali za wananchi bila kujali itikadi za vyama
3. Tutoe fursa kwa wananchi wenye ulemavu waweze kufika na na kushiriki kusikiliza sera za
wagombea na vyama vyao na hatimae kushiriki kupiga kura siku ikifika.