Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Agape AIDS Control Programme added a News update.

$
0
0

TAARIFA ZA MRADI WA KUWASAIDIA VIJANA WAUZA CHIPS KUPATA STADI ZA BIASHARA NA KUTENGENEZA MATOROLI YA CHIPS ZINAZOTEMBEA (MOBILE CARTS VENDING CHIPS PROJECT)

Mradi huu ulikuwa unatekelezwa na Shirika la Agape AIDS Control Programme na ulikuwa unafadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (International Labour Organizatio-ILO) Kupitia Foundation For Civil Society (FCS). Lengo kuu la Mradi huu lilikuwa ni kuwawezesha vijana kujipatia kipato kwa njia ya kufanya biashara hususani biashara yenye ubunifu. Bajeti ya Mradi huu ilikuwa Milioni Kumi na Sita (16,000,000 Tshs au 10,000 USD).

Mradi huu umefanikiwa kufanya yafuatayo:

1. Kufundisha vijana wajasiliamali wauza chips juu ya Ujasiliamali na namna ya kuanzisha biashara na kukuza biashara. Mafanikio Vijana 43 wajasiliamali wauza chips kutoka katika Manispaa ya Shinyanga walifundishwa juu ya Ujasiliamli na namna ya kuanzisha biashara Mpya na kukuza biashara walizokuwa nazo.

2. Kufundisha vijana wajasiliamali wa chips namna ya kuunda/kutengeneza matoroli ya chips yanayotembea. Mafanikio Vijana 43 walifundishwa namna ya kutengeneza matoroli hayo na matatu yalitengenezwa ambapo Mkuu wa Wilaya na Kiongozi wa Mbio za Mwenge alipata nafasi ya kukabidhi machine izo kwa vijana hao wajasiliamali

3. Kufundisha vijana wajasiliamali wauza chips juu ya kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara na taasisi za kifedha na zile za kiserikali. Mafanikio Vijana 38 walihudhuria mafunzo hayo ya siku 2 katika ukumbi wa katemi hotel na tayari watatu wamepata mkopo kupitia CRDB na wengine 5 wamejiunga kwenye kikundi kupata mkopo kutoka VISION FUND

4. Kusaidia kuunda kikundi cha vijana wajasiliamali wauza chips. Mafanikio Vijana 40 wajasiliamali kutoka katika manispaa ya Shinyanga wameunda kikundi na kupata usajili kutoka manispaa ya Shinyanga ofisi ya Maendeleo ya Jamii


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles