Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

ASASI YA JINSIA NA MAENDELEO ROMBO(AJIMARO) created a Projects page.

$
0
0

NARATIVE_RIPORT_AJIMARO.doc UTANGULIZI

Katika mwezi wa kwanza hadi mwezi wa tatu mwaka 2014 Asasi ya jinsia na maendeleo rombo imeweza kuendesha mafunzo ya wanawake na uongozi mradi ambao umefadhiliwa na The foundation for civil society.

Kutokana na uendeshaji wa mafunzo haya yameweza kuleta mabadiliko makubwa kwa wanawake katika nyanja ya uongozi ambao umewawezesha kufanya utetezi ambao umegawanyika katika sehemu kuu zifuatazo:-

  •   Kushiriki katika mchakato mzima wa uandaaji wa sheria mpya na ubadilishaji wa sheria ambazo zinamkandamiza mwanamke
  • Kuwasaidia wanawake waliokatika mazingira magumu kwa kuwapa elimu na mitaji na kuwasaidia ili wakwamuke toka katika lindi la umaskini uliokithiri
  • Kuwasaidia wanawake wenzao kutumia fursa zilizopo katika jamii
  • Kuwasaidia wanawake wenzao katika utafutaji wa rasimali na jinsi ya kuzitumia rasilimali hizo
  • Kuwapa uelewa wanawake kujiunga katika vikundi na vyama mbalimbali ili kuweza kuwa na sauti ya pamoja na kushughulikia masuala ya wanawake kwa sauti moja

Shirika la AJIMARO likishirikiana na mfadhili wake The foundation for civil society wameshiriki kikamilifu katika mchako huu wa utoaji wa mafunzo ya uongozi na ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi kwa kuwawezesha vikundi vya wanawake toka kata zifuatazo:Ubetu/kahe

  1. Mamsera
  2. Olele
  3. K/Samanda
  4. Olili

Mafunzo haya yamesaidia wanawake kutokuwa nyuma katika masuala mbalimbali:

       I.        Kugombea uongozi na kuingia katika vyombo vya maamuzi

      II.        Upatikanaji wa habari muhimu zinazosaidia katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazomuhusu mwanamke

 

AJIMARO kwa kushirikiana na wawezeshaji wameweza kugawa vitini vya uongozi kwa washiriki ili uwe muongozo utakaowawezesha kutoa mafunzo hayo kwa wanawake wengine.

Kitini hicho ni mahususi kumsaidia mwanamke ambae anania ya dhati katika kumkomboa mwanamke kwa kuwapa elimu ambao yeye ameipata katika mafunzo haya.DODOSO_AJIMARO.doc

Kitini hicho kimeelezea matamko mbalimbali na kutambua dhana nzima ya uongozi pia kujua haki zao kutokana na katiba ya jamuhuri wa muungano wa Tanzania (kifungu cha tatu)inalinda uhuru wa mtu mwanamke au mwanaume kupata hifadhi ya maisha,kumiliki mali na pato la jasho lake, kufanya kazi na kupata haki ya kujielimisha kufikia upeo wake.kwa kifupi kutokana na katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Sera ya taifa ya maendeleo ya wanawake jinsia na watoto ya mwaka 2000 na shirika letu la AJIMARO inataka kuwepo kwa jamii yenye usawa,haki TAARIFA_YA_UFUATILIAJI.docxTAARIFA_YA_JUMLA.docx ,uhuru na fursa sawa kwa watu wote kuweza kushiriki kikamilifu na kutumia uwezo vipaji walivyonavyo katika shughuli za umma,uongozi wa nchi,utamaduni,na udhalishaji mali na upatikana wa huduma za kijami ili wapate kuendelea na kuwa na hali bora zaidi ya maisha 



Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles