Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

ASASI YA JINSIA NA MAENDELEO ROMBO(AJIMARO) created a History page.

$
0
0

AJIMARO ni jina lenye maana ya Asasi ya jinsia na maendeleo Rombo katika katiba yake AJIMARO imekusudia kuweka usawa wa kijnsia katika vyombo vya maamuzi,

Wengi wa wanawake wametambua haki na nafasi yao ya ushiriki katika vyombo vya maamuzi kwa kupitia mafunzo waliyoyapata .

 Mafunzo haya yamewasaidia wanawake kuinua hali zao kwa kuimiza kuingia katika vyombo vya maamuzi ili waweze kupanga,kutekeleza kwa kuzingatia ushirikishwaji wa wanawake na wanaume kwa uwiwano uliyo sawa na unaokubalika na wote ,

Ili kurahisisha na kuwezesha utekelezaji wa dhana ya uongozi kwa wanawake Ajimaro imeona ni vizuri kuwapa uelewa wanawake ili wajue dhana ya uongozi na umuhimu wa wao kushiriki katika vyombo vya maamuzi.                                                                                                            

Ajimaro inaunga mkono sera na mipango mbalimbali ya serikali ambayo inaimiza ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi ajimaro inatambua kuwa kufanikiwa katika utekelezaji wa dhana ya uongozi kwa wanawake unategemea sana msukumo wa Serikali hususani Almashauri,kata na vijiji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambao wamesimama madhubuti kwenye utetezi wa haki za wanawake kwa kuwasaidia kwa ushauri na msaada wa kisheria na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wanawake kama tunavyotambua baadhi ya wanawake wengi wananyanyasika katika mambo mbalimbali na wanapokwenda kwenye vyombo vya maamuzi inakuwa shida kupata haki zao

 Kufanikiwa kwa wanawake kuingia katika vyombo vya maamuzi ni kuisaidia jamii kutokana na baadhi ya mifumo,mila na tamaduni zilizojengeka katika jamii zinamkandamiza mwanamke na hivyo kuona kana kwamba ni imeonekana ni kawaida kwa mwanamke kuwa anaongozwa muda wote na hapaswi kuongoza na amekuwa mtu wa kuamuliwa tu badala ya kujadiliana na kufanya maamuzi kwa pamoja

Hatua hii ya wanawake kuwa kama ni kiburudisho tu na kunyimwa nafasi ya uwamuzi kwa mambo yanayomuhusu imesababisha wanawake kujiraumu kwa kujiuliza kwanini wamezaliwa wanawake na si wanaume kauli hizi zimekuwa zikijitokeza mpaka kwenye familia wakiongozana wanaume kuzaliwa basi familia uishi kwa furaha lakini tatizo wanapongozana wanawake kuzaliwa ndani ya familia uonekana kama wazazi hawa hawana watoto ni hasara tu kuwa na watoto wakike .

Mitazamo yote inasababishwa kutokana na wanawake kutokuwepo kwa wingi katika vyombo vya maamuzi

Ni matumaini yangu kuwa kutokana na mafunzo haya ambayo yamefadhiliwa na The foundation for civil society,tunaimani kuwa yataharakisha utekelezaji wa dhana ya uongozi na kuongeza ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi na kufikia malengo ya Ajimro,Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kuinua hali za wanawake ususani kueshimu kauli mbiu ya fursa sawa kwa wote

 

GERWALDA  KIMARO

MRATIBU WA MRADI -AJIMARO

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles