Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

ASASI YA UKOMBOZI WA VIJANA TANZANIA ( AUVITA) has a new discussion about KWANINI VIJANA WANAJIHUSISHA NA VITENDO VYA UOVU?.

$
0
0
ASASI YA UKOMBOZI WA VIJANA TANZANIA ( AUVITA):

CHANZO CHA VIJANA KUJIHUSISHA NA VIKUNDI MBALIMBALI VYA UHALIFU KATIKA JAMII

Imekuwa ni kawaida ya vijana kuanzisha vikundi mbalimbali vya uhalifu katika jamii suala ambalo jamii kiujumla haiwezi kulistahimili kwani vijana hawa wamekuwa ni vijana wanyang’anyi na pengine hata kudhuru maisha ya watu.

Hivi juzi tu, tumeshuhudia ama kushuhudiwa katika vyombo vya habari ama kwa kuona kwa macho yetu jiji Dar-es-salaamu vikundi vya vijana mbalimbali vijijihusisha na unyang’anyi kwa kutumia nguvu tena hadharani na sehemu nyingine mbalimbali za nchi hii siyo hali ya kuvumilia katika jamii kwani inahatarisha uhuru na uhai wa taifa kiujumla. Pamoja na jitihada mbalimbali kuchukuliwa na serikali ili kudhibiti tatizo hili katika jamii lakini sisi wana AUVITA kiukweli tunaliona tatizo hili kwa jicho tofauti ambapo serikali na asasi zingine tunaweza kushiliki kwa kutatua changamoto zifuatazo kwa vijana ili kuwaepusha na vitendo visivyo salama katika usitawi wa jamii.

Sababu za vijana kuunda vikundi vya kutenda maovu

Ukosefu wa ajira kwa vijana, kumekuwa na ongezeko kubwa kwa vijana katika jamii ambao hawana ajira suala hili linaendana sambamba na kutokuwa na sifa za kupata ajira hivyo vijana wengi hukosa kazi ya kufanya na kujiandaa rasimi kwa kuishi kwa kutumia nguvu za uporaji kwa kuunda vikundi mabalimbali kama tuonavyo leo.

Ukosefu wa elimu ya ujasiliamali kwa vijana, imekuwa ni kawaida ya vijana kutoka vijijini na kukimbilia mijini kwa kujitafutia kipato lakini wafikapo mijini huyakuta maisha ni magumu kupita kiasi kwa vile vijana hawa huwa hawajajiandaa rasimi kujishugulisha na biashara ndogondogo za kijiingizia kipato basi matokeo yake huwa ni kuvuta madawa ya kulevya na kundaa vijikundi vya uhalifu.

Ukosefu wa mitaji, pamoja na kuwa vijana hawa baadhi yao hupata mafunzo ya ujasiliamali ama kwa wenzao au asasi za kijamii lakini bado changamoto kubwa kwao huwa ni mitaji ya kuwawezesha kuanzisha biashara ndogondogo, kutokopesheka kwenye taasisi mbalimbali za kifedha, na kutijituma kujitafutia wenyewe mitaji.

Nini cha kufanya

Serikali iamzishe mafunzo ya ujasiliamali mashuleni na vyuoni kama somo na liwe la lazima kwa kila mtanzania kusoma.

Vijana wahamasishwe kijihusisha na shughuli za kilimo vijijini badala ya kukimbilia mijini ambako hkoswakazi ya kufanya na kujiingiza katika vikundi vya uhalifu.

Asilimia 10 ya mapato ya halimashauri zote nchni kutengewa vijana na akinamama itiliwe mkazo na serikali kwa kushirikiana na asasi za kijamii waelimishe vijana na kuwawezesha ili wajijengee misingi bora ya maisha.

Taasisi za kifedha ziwekeze kwa vijana kwa kuwaelimisha juu ya mbinu za kibiashara na jinsi wanavyoweza kunufaika na huduma za kifedaha kwa kuwekeza hasa katika kilimo ambacho hakiitaji ujuzi wa elimu ya juu sana, tukiwajengea uwezo vijana na taasisi zikifungua milango ya mikopo kwa vijana watajikwamua kiuchumi.

Asasi za kijamii zinazohusika na vijana zitumie muda mwingi kuongea na vijana na kuwaelimisha juu ya shughuli mbalimbali ambazo zinaweza kurahisisha maisha yao kilahisi.

Mwisho

Jamii yetu ni vijana wetu tuwaelimishe, tuwawezeshe na kuwajengea misingi bora ya maisha kwa maendeleo ya taifa letu.

NOMBA MICHANGO YENU ILI KUTATUA TATIZO HILI.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles