Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

UNITED AFRICANS updated its History page.

$
0
0
 

                  

 

 
  
 
 
  

UNITED AFRICANS

SHIRIKA LA UMOJA WA WATU WA AFRIKA

APAPO

MAANA YA APAPO

APAPO ni shirika la umoja wa watu wa Afrika lenye lengo la kushirikiana na serikari za Mataifa ulimwenguni katika kuleta mageuzi kwa kupambana,kuzuia na kuondoa changamoto ndani ya jamii zilizoainishwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa namba 102 la mwaka 1952.

KIFUPISHO CHA APAPO

APAPO ni kifupisho cha African Poor And Patient Organization.

KUANZISHWA KWA APAPO

Shirika la APAPO lilianzishwa kwa sheria namba 24 ya mwaka 2002 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa usajili Na.00005441 mnamo April 4, 2012.

MADHUMUNI YA KUANZISHA APAPO

Dhumuni la kuanzishwa APAPO lilitokana na waasisi wake kufanya utafiti dhidi ya chimbuko na suluhu la umaskini,ujinga na maradhi duniani.

LENGO KUU LA KUANZISHA SHIRIKA LA APAPO

Lengo kuu la kuanzisha APAPO ni kushirikiana na kuziunga mkono serikali katika kuleta mageuzi kwa kupambana, kuzuia na kuondoa changamoto zinazoikabili au ambazo zingeikabili jamii.

DIRA

Dira ya Shirika Tukufu la APAPO ni kuwa kioo cha Huduma za Afya, Elimu, Ulinzi na Usalama , Usawa wa Kijinsia, Kijamii, Kiuchumi na Kiutamaduni duniani.

DHAMIRA

Dhamira ya Shirika ni kuhakikisha kuwa rasilimali zilizopo zinatumika barabara katika kupambana, kuzuia na kuondoa ujinga, maradhi na umaskini ndani ya jamii.

MUDA NA MAENEO YA UTAFITI KABLA YA KUANZISHWA APAPO

Utafiti wa kubaini chimbuko na suluhu la umaskini, ujinga na maradhi ulianza mnamo Julai 1998 katika misitu ya Itanonge, Katuma Mkoani Katavi nchini Tanzania na kuendelea katika nchi mbalimbali duniani na kumalizika mnamo Julai 2010 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas nchini Uingereza.

MUDA NA MAENEOYA UCHUNGUZI AU MAFUNZO (Field) KABLA YA SHUGHULI RASMI ZA SHIRIKA

Kutokana na ukweli usiopingika usemao kuwa ‘Kabla ya kufungua MradiChunguza’ falsafa hii ilimfanya Gavana wa shirika baada ya usajili na kabla ya kuzindua miradi mbalimbali ikiwamo usajili wanachama wa APAPO, alichukua fursa kutembelea mikoa mbalimbali nchini Tanzania kwa ajili ya kulinadi shirika na kutafuta wajumbe au wawakilishi wa shirika watakaoliwakilisha shirika katika nchi na mikoa mbalimbali. Pamoja na mkoa wa Dar Es Salaam alipoweka kambi katika eneo la ubungo Msewe kwa kufungua ofisi ya muda kwa miezi minane kwa ajili ya kushirikiana na serikali kuu kwa urahisi na uhakika na kupata wajumbe mkoani humo.

Aidha alizulu pia mikoa ya Morogoro,Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma na Tabora kabla ya kurudi katika nafasi yake na kuanza shughuli rasmi baada ya kubaini changamoto zinazoendelea ndani ya jamii.

CHIMBUKO LA UMASKINI, UJINGA NA MARADHI NDANI YA JAMII

Matokeo ya utafiti yalionesha kuwa pamoja na vyanzo mbalimbali vinavyosababisha umaskini,ujinga na maradhi ndani ya jamii,ukiwemo ukosefu wa imani, matumaini, subira, uvumilivu na uadilifu,chanzo kikubwa kabisa ni wananchi hasa wanaoishi maisha ya chini kukosa maarifa, umoja, mshikamano na ushirikiano hususani kabla na wakati wa matatizo miongoni mwao wakinung’unika, wakilaumu, wakisubiri na kutegemea serikali kuondoa changamoto zinazoweza kuondolewa na wao wenyewe.

NCHI WANACHAMA WA APAPO

Shirika la APAPO ni la kimataifa lenye nchi wanachama wa nchi zote barani Afrika, ambalo linasambaa kwa kasi kubwa sana ili kuwafikia wananchi wote hasa waishio maisha ya chini na baadaye kuenea dunia nzima kama Dira ya Shirika ukilinganisha na muda wa kuzaliwa kwake.

KANDA ZA SHIRIKA

Shirika limegawanyika katika Kanda sita(6) za Afrika ambazo ni:-

  1. Kanda ya Afrika ya Kaskazini makao makuu yake Algeria;
  2. Kanda ya Afrika ya Magharibi makao makuu yake Guinea;
  3. Kanda ya Afrika ya Kusini makao makuu yake Botswana;
  4. Kanda ya Visiwa vya Afrika makao makuu yake Madagascar;
  5. Kanda ya Afrika ya Kati makao makuu yake Cameroon;
  6. Kanda ya Afrika ya Mashariki makao makuu yake Tanzania;
HUDUMA ZA SHIRIKA

Shirika lina aina mbili za Huduma kwa jamii kama zilivyoorodheshwa hapo chini:-

  1. HUDUMA ZA PEKEE NA
  2. HUDUMA ZA JUMLA

Huduma za Pekee.

Huduma hizi ni Mafao 12 kwa wanachama waliotimiza vigezo, masharti na wajibu:-

  1. Msaada wa Usafiri kwa wanafunzi wanachama au wanafunzi wa wanachama;
  2. Kipaumbele cha Ajira;
  3. Mikopo isiyokuwa na Riba;
  4. Lishe kwa wenye virusi vya Ukimwi na Ukimwi;
  5. Mafao kwa Wazee;
  6. Mafao kwa Wastaafu;
  7. Msaada wa Kisheria;
  8. Gharama za Elimu;
  9. Gharama za Matibabu ya Rufaa na yasio ya Rufaa
  10. Msaada wa kusafirisha Wagonjwa;
  11. Mazishi/Rambirambi na
  12. Harusi/Jubilee.

 

Huduma za Jumla

Huduma hizi zinatolewa au zitatolewa kwa jamii nzima bila kujali kuwa mwananchi ni mwanachama au la.

1.Usajili wa Wanachama kwa hiari;

2.Kutoa Ajira kwa Vijana na Wastaafu;

3. Kuzuia Ajali na Majeruhi au Vifo vitokanavyo na Ajali;

4. Kuzuia na kutuliza Ghasia, Vita, Virusi vya Ukimwi na Ukimwi;

5. Kutoa Msaada wa Matibabu ya Rufaa na yasio ya Rufaa, Elimu ya Chekechea, Msingi,      

    Sekondari na Chuo kwa Mayatima,Wakimbizi, watoto wa walemavu na watu maskini

    wasiokuwa na uwezo wa kumudu ada za viingilio na michango au ada za uanachama wa

    shirika;

6. Kutoa Msaada wa chakula, mavazi na malazi kwa wahanga wa njaa, vita,Maafa na Majanga;

7. Kusimamia Mazingira,Sheria,Wajibu, Haki za Binadamu na Usafiri wa nchi kavu na majini;

8. Kulinda Usalama wa Raia na Mali zao kwa kushirikiana na wadau wengine;

9. Kuyasaidia Mashirika ya Kiserikali na yasio ya Kiserikali yanayotoa huduma zinazofanana na shirika mama na kutoa Elimu ya Wema na Ubaya kwa Watoto na Vijana ikiwa ni kuwaandaa Kiroho, Kimwili, Kiakili, Kisaikolojia, Kijamii, Kiuchumi na Kiutamaduni ili kuzuia, kupambana, Kukabiliana na Kushinda changamoto ambazo zinaikabili au zingeikabili jamii.


AINA ZA UANACHAMA


(1) Kibarua au  Mjasiriamali Mdogo                 

(2) Mfanyakazi au Mjasiriamali Asiye Rasmi

(3) Mfanyakazi au Mjasiriamali Rasmi

(4) Asiyeweza Kufanya Kazi( Mtegemezi)

(5) Muasisi wa kuteuliwa (Mwakilishi)
 


UTARATIBU NA MASHERTI YA KUSAJILI WANACHAMA WA SHIRIKA

(A) MWANACHAMA WA KAWAIDA

Mtu yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka kumi na minane (18) anaweza kuwa Mwanachama wa Shirika kwa kulipa Ada ya Kiingilio au Uanachama kulingana na Aina ya Uanachama na Kipato cha mwezi alichonacho kama ifuatavyo:-


 AINA YA UANACHAMA                 KIWANGO CHA ADA                  KIPATO KWA MWEZI

Kibarua au Mjasiliamali Mdogo                                  T.Shs 16,000/=                                    T.Shs 1/= -T.Shs 160,000/=

Mfanyakazi au Mjasiriamali Asiye Rasmi    T.Shs 50,000/=                                     T.Shs 160,001/= -T.Shs 500,000/=

Mfanyakazi au Mjasiriamali Rasmi           T.Shs 100,000/=               T.Shs 500,001 nk.                                                                                                                   

Asiyeweza Kufanya Kazi (Mtegemezi)                      T.Shs 0                                                   Chini ya T.Shs 1,600/=
 
 
 

(B) MWASISI WA KUTEULIWA /MWAKILISHI/MJUMBE KATIKA KAMATI YA UONGOZI

Mtu anayetaka kuwa Mwasisi wa Kuteuliwa, Mwakilishi au Mjumbe wa Shirika katika Kamati ya Uongozi, kwa kuchaguliwa au Kuteuliwa, mwenye sifa ya kuwa Mwasisi wa Kuteuliwa, Mwakilishi au Mjumbe atalipa Ada kulingana na ngazi kama ifuatavyo:-

           

 Ada

 T.Shs 200,000/=

T.Shs 320,000/=

T.Shs 400,000/=

T.Shs 800,000/=

T.Shs

1,600,000/=

T.Shs 5,000,000/=

 Ngazi ya Uwakilishi

MTAA au KIJIJI

KATA

TARAFA

WILAYA

MKOA

TAIFA

 

 (C)   MTU ANAETAKA KUFANYA KAZI NDANI YA SHIRIKA

Mtu yeyote asiyemwanachama wa shirika, mwenye sifa na anahitaji kufanya kazi ndani ya shirika atalazimika kupitia njia zifuatazo kabla ya kuwa mfanyakazi wa Shirika:-

(i)        Ataandika barua ya Maombi ya  nafasi ya Uanachama na Kazi;

(ii)   Atajiandikisha kuwa Mwanachama wa Shirika kwa kulipa ada ya uanachama  isiyorudishwa T.Shs 50,000/=;

(iii)     Atasajiliwa kwa kulipa Ada ya Fomu ya Uanachama T.Shs 10,000/=;

(iv)     Atafanyiwa usaili;

(v)       Atahudhuria Mafunzo ya Kazi kwa nadharia kwa muda wa siku saba (7;)

(vi)     Atahudhuria Mafunzo ya Kazi kwa Vitendo kwa muda wa siku ishirini na tatu (23;) kutegemea na Nafasi iliyotangazwa.

(vii)  Atajaza Mkataba wa Kazi utakaoonesha kiasi cha Mshahara kwa mwezi kabla na baada ya kuthibitishwa, Makato ya 5% ya mshahara kwa ajili ya kuweka Akiba yake ya uzeeni katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii,10% ya Mshahara kwa ajili ya Ada ya Uanachama kwa mwezi; 5% kwa ajili ya wahitaji na

(viii)Atapewa muda wa Matazamio usiokuwa chini ya miezi mitatu na usiozidi miezi kumi na miwili kabla ya kuthibitishwa kazini rasmi.

 

 

Utaratibu Wa Kuajiri Wakuu wa Shirika na Makatibu Watendaji

Utaratibu wa kutangaza nafasi za Uanachama na kazi kwa ajili ya kuwapata Wakuu wa Shirika na Makatibu Watendaji hufanywa kwa Awamu au vinginevyo kulingana na mahitaji kuanzia ngazi ya juu hadi chini.

 

 

VIWANGO VYA ADA ZA MAOMBI YA UWAKILISHI/UJUMBE KATIKA KAMATI ZA UONGOZI

Baada ya wanachama walau mia moja arobaini na wanne(144) kuandikishwa katika ngazi na eneo husika, nafasi za Uwakilishi au Ujumbe kutangazwa, mwanachama atatuma maombi kulingana na ngazi kama ifuatavyo:-

 

 Ki           

 Ada

 T.Shs 20,000/=

T.Shs 30,000/=

T.Shs 40,000/=

T.Shs 80,000/=

T.Shs 160,000/=

T.Shs 500,000/=

 Ngazi ya Uwakilishi

MTAA au KIJIJI

KATA

TARAFA

WILAYA

MKOA

TAIFA

 

DHAMANA YA NAFASI YA UANACHAMA

Mwanachama yeyote isipokuwa Mtegemezi atawaleta wadhamini wake wanaofahamiana na kuaminiana vizuri kumi na wawili (12) wasiokuwa wanachama wa shirika ambao nao watakubali kuwa wanachama wa shirika kabla ya kuthibitishwa kwake yaani kuwa na sifa ya kuanza kupata Haki zake za msingi.

 

MUDA WA KUANZA KUPATA MAFAO AU HUDUMA ZA SHIRIKA

(A)          MWANACHAMA WA KAWAIDA

Mwanachama wa kawaida baada ya kutimiza vigezo na masherti mengine, ataanza kupata mafao au huduma baada ya kuchangia ada au mchango wa Uanachama wake walau mwezi mmoja (1.) tangu ajiunge na shirika.  

 (B)            MWANACHAMA TEGEMEZI

Mwanachama Tegemezi yaani mzee asiyejiweza, mlemavu na mgonjwa wa muda mrefu asiyeweza kufanya kazi, atapata Mafao au Huduma baada ya Kamati ya Uongozi ngazi ya mtaa au kijiji kuundwa na kuanza kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kutoa Huduma kwa Wategemezi au wahitaji.

 

(C)           MUASISI WA KUTEULIWA/MJUMBE AU MWAKILISHI

Muasisi wa Kuteuliwa/Mjumbe au Mwakilishi atapata Mafao wakati wowote kulingana au kutegemea na uwezo wa Kamati yake.


POSHO YA VIKAO

          Muasisi wa Kuteuliwa/Mjumbe au Mwakilishi

Kila mwezi katika vikao Muasisi wa Kuteuliwa/Mjumbe au Mwakilishialiyehudhuria kikao atalipwa posho asilimia kumi (10%) ya Ada ya Uasisi wa Kuteuliwa/Uwakilishi au Ujumbe aliyolipa katika Kamati ya Uongozi ngazi husika.

     

MICHANGO AU ADA ZA UANACHAMA KILA MWEZI    

 


Mwanachama yeyoteatachangia au atakatwa ada ya uanachama kila mwezi 20% ya pato au mshahara wake kwa kulipa kidogo kidogo kila juma 5% ya ada au mchango wote kama kigezo cha kupata huduma au haki zake za msingi ndani ya shirika.

MIKUTANO

Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni ndogo za uendeshaji wa shirika, wanachama wote katika Mtaa au Kijiji wana wajibu wa kukutana mara moja kila mwisho wa juma kwa ajili ya kujadili maswala mbali mbali, kupata taarifa za shirika, kutoa matatizo yao kwa viongozi na kujua namna ya kuyatatua kwa mfumo wa kushirikishana, kutoa kero, duku duku zao, hoja na maoni yao kwa viongozi wao kwa lengo la kuboresha huduma za shirika, kujadiliwa kwa ajili ya kupata huduma, kubuni na kuhoji miradi nk.

AKIBA YA UZEENI

Mwanachama yeyoteanaetimiza wajibu wake, shirika kupitia michango au ada yake ya uanachama kila mwezi, atawekewa akiba ya uzeeni 5% ya pato au mshahara wake kupitia mfuko wa hifadhi ya jamii utakaopendekezwa na shirika.

NB: Ada au michango katika nchi wanachama wa APAPO itategemea na msimamo wa thamani ya Dola ya         

        Marekani katika nchi husika kwa kutumia Sarafu ya nchi husika.

 

VIGEZO NA MASHARTI RAHISI

Iwapo Mwanachama, mjumbe au mwakilishi au mtumishi atasimama au atagoma kutekeleza au kutimiza wajibu wake katika shirika makusudi au kwa njama au vinginevyo kwa sababu zisizo za ugonjwa au vinginevyo bila taarifa atapoteza baadhi au haki zake za msingi.

 

 

SHUGHULI KUBWA YA APAPO

Shughuli kubwa ya APAPO ni kuwaelimisha wananchi ili wajitambue, waamke, waungane, wajitegemee na wajiajiri kwa kutumia lasirimali walizonazo pamoja na vyanzo vingine vya Mapato ya Shirika katika kujiinua kiuchumi na kujikomboa dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi miongoni mwao badala ya kubweteka, kunung’unika, kulaumu na kusubiri serikali zenye kuelemewa na mizigo mikubwa na hivyo kushindwa kumudu mahitaji mengine ya wananchi kwa wakati.                                                                                        

MAJUKUMU NA WAJIBU WA VIONGOZI NA WATENDAJI WA SERIKALI ZA MITAA KWA SHIRIKA

Pamoja na Sera ya Taifa ya Ajira 2008 inayobainisha Majukumu na Wajibu wa kila mdau, ili kufikia lengo lililokusudiwa ikiwa ni pamoja na kupunguza au kuondoa tatizo la ukosefu wa Ajira na viwango vya ajira isiyokidhi kiwango, Viongozi na Watendaji wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa watakuwa na wajibu ufuatao kwa Shirika:-

·   Kushirikishana na kushirikiana bila kuingiliana wala kupingana katika kuielimisha jamii juu ya utumiaji wa rasilimali walizonazo na kutumia fursa zilizopo ili kuondokana na tatizo la umaskini wa mawazo na kipato na kuweka wazi mipaka ya uwajibikaji; 

    Kulitambulisha Shirika katika ngazi zingine za Utawala kwa  wakati;

·      Kutoa ushauri wa mara kwa mara katika utekelezaji wa majukumu yake ili kuleta tija katika jamii;

·   Kufuatilia na kusambaza taarifa za shirika kwa jamii nzima;

·      Kufanya Ubia na Shirika kwa kutoa fursa ya kutumia ofisi za serikali za mitaa ngazi ya mtaa/kijiji kuwa vituo vya Huduma za Shirika kwa wananchi wa maeneo husika ikiwa ni pamoja na Uandikishaji Wanachama wa Shirika, Mayatima, Wazee, Walemavu na wagonjwa wa muda mrefu wasio na kipato;

·   Viongozi wa ngazi zote (mfano Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa/kijiji) kukubali kuwa walezi wa Shirika ngazi husika watakaohudhuria vikao vya Kamati za Uongozi wa shirika kila mwezi kikatiba, kuwashauri viongozi wa shirika na kuhakikisha utekelezaji wa mpango huu kwa jamii ya eneo husika.

 

SEMINA ELEKEZI KWA VIONGOZI NA WATENDAJI WA SERIKALI ZA MITAA

Kwa mujibu wa kanuni za ushirikishaji wa wadau wengine wa Maendeleo, Maofisa wa shirika wana wajibu wa kutoa Semina Elekezi endelevu kila inapobidi kwa viongozi na watendaji wa Serikali za Mitaa wenye lengo la kushirikiana na kuliunga mkono Shirika katika utekelezaji wa majukumu ili kuwapa uelewa wa shughuli na Huduma za Shirika kwa jamii wanayoiongoza .

 

KAULI MBIU

1.      KAULI MBIU YA MPANGO

“Wananchi, Tuungane Tujitegemee”

2.      KAULI MBIU YA AJIRA

“Wajibu na Haki “

 

MAWASILIANO

KAMISHINA WA SHIRIKA.................................................................................................+255764876045

 

TOVUTI: WWW. Envaya.org/apapo

 
  

           

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles