Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

ASASI YA UKOMBOZI WA VIJANA TANZANIA ( AUVITA) updated its History page.

$
0
0

Shirika hili limeanzishwa kutokana na Shauku kubwa aliyokuwa nayo ndugu Simba Mramba ya kuisaidia jamii yake na kuweka mazingira ambayo kuishi kwake sikumoja kutakumbukwa na vizazi vijavyo. kutokana na mawazo hayo aliamuwa kuanzisha shirika ambalo litawaunganisha vijana wa Tanzania na kutoa elimu mbalimbali kwa umma wa watanzania. kupita mawazo yake hayo aliamua kuhusisha baadhi ya wananchi na wanachuo wanzake akiwa chuoni Mtwara STEMMUCO, ili waungane kwa pamoja kuisaidia jamii ya watanzania kupitia elimu yao, hata hivyo kupitia shuguli mbalimbali za uhifadhi wa mazingira chuoni hapo na maeneo mbalimbali ya mtwara mjini waliweza kulinda na kuyatetea mazingira.

Kwakutambua kuwa RUSHWA imetanda katika jamii na nikikwazo cha maendeleo ya jamii hususani katika katuika tabaka la chini , ndugu Simba Mramba aliweza kuwashawishi wenzake na wakaamuwa kuanzisha klabu ya TAKUKURU (Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania) kupitia taasisi hii waliweza kutoa elimu ya maadili mema na utawala bora ndani na nje ya mji wa Mtwara kwa kutumia midahalo mbalimbali na vyombo vya habari wakishirikiana na TAKUKURU Mkoa wa Mtwara.

Kupitia shughuri hizi ndugu Simba Mramba kwa ushawishi wake alimua kuifikisha huduma hii kwa jamiii huku wakiwa na maono enderevu ya ustawi wa jamii ya watanzania kwa kuijenge jamii misimgi na uwezo wa kuyatambua matatizo ya KIMAZINGIRA, KIJAMII, KIUCHUMI NA KITEKNOLOJIA na mbinu za kuweza kupambana nayo.

Kwa kuzingatia hayo na kushauriana na wenzake waliamua kuanzasha Asasi ya Ukombozi wa Vijana Tanzania (AUVITA)ili kuijenga na kuiendeleza jamii ya Tanzania.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles