Habari wadau wa maendeleo,napenda kuwasilisha taarifa ya masikitiko juu ya hawa wenzetu waliopewa dhamana na serikali kwa ajili ya kutengeneza chombo kitachotuongoza sisi na vizazi vyeti ( WABUNGE WA KATIBA ) kwa kweli hawaoni ni kiasi gani wa Tanzania wanavyowachukulia kwa mitazamo tofauti kuhusu madai wanayosema ni muhimu kwao ya kudai posho zaidi ya ile iliyopangwa,Je wanatuchukuliaje sisi wa Tanzania wenzao tuliokosa fursa ya kushiriki bunge hilo kwa huo msimamo wao wa kudai posho kubwa angali bado kunachamgamoto kubwa za kimaendeleo zinazotusumbua ikiwa ni pamoja na Huduma duni za Afya,Miundo mbinu ya barabara.
Pia watambue kuwa kuna waajiliwa wengi mshara chini ya laki tatu kwa mwezi,wao wanapata laki tau kwa siku lakini hawatosheki na kutaka ziada ya laki mbili ili iwe laki tano kwa siku je hao watu ni wazazlendo kweli wa nchi hii au wakimbizi ? tunaomba watafakari kwa kina juu ya msimamo wao. naomba tuwe wazalendo na nchi yetu.