Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

YOUTH COMMUNITY DEVELOPMENT added a News update.

$
0
0

Ndugu Simba Mramba .

Mwanzilishi wa Asasi ya Youth Community Development. (YOCODE) na ndiye mwenyekiti wa sasasi hiyo. Anawakaribisha vijana katika ukombozi mpya. Sikuzote huamini kuwa hamuna lisilowezekana Duniani na maisha ya mutu hupangwa na mtu mwenyewe, kwa ushirikiano na vijana kwa kuwapatia elimu mbalimbali maisha ya vijana yatabadilika na kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.

Anasema kuwa.

Ni dhahili kabisa jamii ya watanzania  inahitaji elimu mbadala tofauti na ya darasani ambayo itawajengea wanajiamii hususani vijana misingi ya kujiami, kupata utashi wa kuhoji,dadisi na kujua nini kinaendelea katika jamii. vijana wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika jamii washiriki katika shughuri za uzalishaji na maendeleo ya jamii zao kila mmoja, wafanye kazi kwa tija na kuwajibika popote walipo, waondoe mawazo mgando ya utegemezi na wajiajiri wenyewe kupitia rasilimali zinazo wazunguka, waondoe mtazamo hasi na wajenge fikra chanya juu ya maisha yao.

"umasikini si janga kama tetemeko la aridhi, njaa na mafuriko bali husababishwa na binadamu mwenyewe na anaweza kuuondoa mwenyewe kwa kutambua wajibu wake na kuwajibika" Simba Mramba.

"Ni bora ufanyekitu kwenyejamii ambacho sikumoja jamii itakukumbuka na kuishi kwako kutaonesha thamani katika jimii kuliko kuishi kusahaulika" Simba Mramba.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212