MIRADI MIPYA YA MARAFIKI WA ELIMU DODOMA (MED) 2014
- Mradi wa Haki Zangu Sauti Yangu/My Rights My Voice(MRMV) 2014.
- Mradi wa vipindi vya Radio 2014.
- Mradi wa Youth 2 Youth 2014.
.........................................................................................................................
VIPINDI VYA RADIO - DODOMA
MED kwa ushirikiano na shirika la HakiElimu katika mwaka 2014 tutaendesha vipindi vya Radio katika kituo cha Radio Sports FM cha Dodoma. Katika vipindi hivo mada mbalimbali zitajadiliwa na washiriki kutoka Wilaya za Dodoma, Kondoa, Mpwapwa, Bahi, Chemba, Mpwapwa, kongwa na Chamwino.
Lengo la vipindi hivi ni kuongeza ushiriki wa wananchi katika kujadili masuala mbalimbali ya kijamii hususan katika kuboresha Elimu na Demokradsia nchini.
MRADI WA KUHAMASISHA UTAWALA BORA NA DEMOKRASIA SHULENI
MED kwa mwaka 2014 inaendelea na mradi wa Haki Yangu Sauti Yangu kaika shule zaidi ya 24 za Msingi na Sekondari katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Mradi huu utakao husika na kujenga uwezo wa Mabaraza ya wanafunzi, Kamati za Shule, Bodi za Shule na Menejimenti za shule unafadhiliwa na shirika la kimataifa la Oxfam GB.
MRADI WA MAKTABA ZA JAMII.
MED inaendelea kufanya mazungumzo na ofisi ya Afisa Mtendaji wa kata ya Kikuyu Kusini kwa ajili ya kufungua Maktaba ya Jamii itakayo hudumia wakazi wa Kata a Kikuyu Kusini, Kikuyu Kaskazini na Mkonze katika Manispaa ya Dodoma. Iwapo mradi huo utafanikiwa; wanafunzi wa shule za sekondari za Kikuyu, Mkonze, Chidachi na Wella pamoja na wanafunzi wa shule za msingi Mkonze, Kikuyu A, Kikuyu B, Mkonze na Chidachi watanufaika na huduma hiyo ya Maktaba.
MED imekuwa ikijihusisha na shughuli za kuhamasisha jamii kuboresha Elimu, Kushiriki katika Mikutano ili kuongeza ushiriki wa wananchi katika masuala ya kijamii na kukuza Demokrasia, Kuelimisha vijana na jamii kuhusu madhara ya Matumizi ya Madawa ya Kulevya, Madhara ya UKIMWI kwa jamii na Taifa, Kuhamasisha Utamaduni kwa kuwa na vikundi vya Sanaa; na pia MED inahamasisha jamii katika kuhakikisha kuwa inalinda Afya zao dhidi ya Magonjwa kama Malaria, Kipindupindu nk.
Mwaka 2010 MED kwa uhisani wa Shirika la HakiElimu na Kifimbo FM; iliendesha vipindi 23 vya Radio vilivyojadili masuala mbalimbali ya Elimu ikiwemo Elimu ya Demokrasia katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabubge na Madiwani. Mwaka 2011 MED kwa kushirikiana na HakiElimu na Uwezo.net itaendelea na mradi wa kuendesha vipindi vya Radio kwa ajili ya Uhamashishaji wa Kuendeleza na kuboresha Elimu Mkoani Dodoma.