Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

UNITED AFRICANS updated its History page.

 

                  

 

 
  
 
 
  

UNITED AFRICANS

SHIRIKA LA UMOJA WA WATU WA AFRIKA

APAPO

MAANA YA APAPO

APAPO ni shirika la umoja wa watu wa Afrika lenye lengo la kushirikiana na serikari za Mataifa ulimwenguni katika kuleta mageuzi kwa kupambana,kuzuia na kuondoa changamoto ndani ya jamii zilizoainishwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa namba 102 la mwaka 1952.

KIFUPISHO CHA APAPO

APAPO ni kifupisho cha African Poor And Patient Organization.

KUANZISHWA KWA APAPO

Shirika la APAPO lilianzishwa kwa sheria namba 24 ya mwaka 2002 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa usajili Na.00005441 mnamo April 4, 2012.

MADHUMUNI YA KUANZISHA APAPO

Dhumuni la kuanzishwa APAPO lilitokana na waasisi wake kufanya utafiti dhidi ya chimbuko na suluhu la umaskini,ujinga na maradhi duniani.

LENGO KUU LA KUANZISHA SHIRIKA LA APAPO

Lengo kuu la kuanzisha APAPO ni kushirikiana na kuziunga mkono serikali katika kuleta mageuzi kwa kupambana, kuzuia na kuondoa changamoto zinazoikabili au ambazo zingeikabili jamii.

DIRA

Dira ya Shirika Tukufu la APAPO ni kuwa kioo cha Huduma za Afya, Elimu, Ulinzi na Usalama , Usawa wa Kijinsia, Kijamii, Kiuchumi na Kiutamaduni duniani.

DHAMIRA

Dhamira ya Shirika ni kuhakikisha kuwa rasilimali zilizopo zinatumika barabara katika kupambana, kuzuia na kuondoa ujinga, maradhi na umaskini ndani ya jamii.

MUDA NA MAENEO YA UTAFITI KABLA YA KUANZISHWA APAPO

Utafiti wa kubaini chimbuko na suluhu la umaskini, ujinga na maradhi ulianza mnamo Julai 1998 katika misitu ya Itanonge (Katuma) Mkoani Katavi nchini Tanzania na kuendelea katika nchi mbalimbali duniani na kumalizika mnamo Julai 2010 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas nchini Uingereza.

MUDA NA MAENEOYA UCHUNGUZI AU MAFUNZO (Field) KABLA YA SHUGHULI RASMI ZA SHIRIKA

Kutokana na ukweli usiopingika usemao kuwa ‘Kabla ya kufungua MradiChunguza’ falsafa hii ilimfanya Gavana wa shirika baada ya usajili na kabla ya kuzindua miradi mbalimbali ikiwamo usajili wanachama wa APAPO, alichukua fursa kutembelea mikoa mbalimbali nchini Tanzania kwa ajili ya kulinadi shirika na kutafuta wajumbe au wawakilishi wa shirika watakaoliwakilisha shirika katika nchi na mikoa mbalimbali. Pamoja na mkoa wa Dar Es Salaam alipoweka kambi katika eneo la ubungo Msewe kwa kufungua ofisi ya muda wa miezi minane kwa ajili ya kushirikiana na serikali kuu kwa urahisi na uhakika na kupata wajumbe mkoani humo, alizulu pia mikoa ya Morogoro,Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma na Tabora kabla ya kurudi katika nafasi yake na kuanza shughuli rasmi za kusajili wanachama watakaounda Kamati Tendaji au za Uongozi baada ya kubaini changamoto zinazoendelea ndani ya jamii.

CHIMBUKO LA UMASKINI, UJINGA NA MARADHI NDANI YA JAMII

Matokeo ya utafiti yalionesha kuwa pamoja na vyanzo mbalimbali vinavyosababisha umaskini,ujinga na maradhi ndani ya jamii,ukiwemo ukosefu wa imani, matumaini, subira, uvumilivu na uadilifu,chanzo kikubwa kabisa ni wananchi hasa wanaoishi maisha ya chini kukosa maarifa, umoja, mshikamano na ushirikiano hususani kabla na wakati wa matatizo miongoni mwao wakinung’unika, wakilaumu, wakisubiri na kutegemea serikali kuondoa changamoto zinazoweza kuondolewa na wao wenyewe.

NCHI WANACHAMA WA APAPO

Shirika la APAPO ni la kimataifa lenye nchi wanachama wa nchi zote barani Afrika, ambalo linasambaa kwa kasi kubwa sana ili kuwafikia wananchi wote hasa waishio maisha ya chini na baadaye kuenea dunia nzima kama Dira ya Shirika ukilinganisha na muda wa kuzaliwa kwake.

KANDA ZA SHIRIKA

Shirika limegawanyika katika Kanda sita(6) za Afrika ambazo ni:-

  1. Kanda ya Afrika ya Kaskazini makao makuu yake Algeria;
  2. Kanda ya Afrika ya Magharibi makao makuu yake Guinea;
  3. Kanda ya Afrika ya Kusini makao makuu yake Botswana;
  4. Kanda ya Visiwa vya Afrika makao makuu yake Madagascar;
  5. Kanda ya Afrika ya Kati makao makuu yake Cameroon;
  6. Kanda ya Afrika ya Mashariki makao makuu yake Tanzania;

NCHI ZINAZOUNDA KANDAYA AFRIKA YA MASHARIKI

   Nchi zinazounda Kanda ya Afrika ya Mashariki ni Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya,    Rwanda, Sudani, Sudani ya Kusini, Somalia, Tanzania na Uganda.s

HUDUMA ZA SHIRIKA

Shirika lina aina mbili za Huduma kwa jamii kama zilivyoorodheshwa hapo chini:-

  1. HUDUMA ZA PEKEE NA
  2. HUDUMA ZA JUMLA

Huduma za Pekee.

Huduma hizi ni Mafao 10 yanayotolewa au yatakayotolewa kwa wanachama waliotimiza vigezo,masharti na wajibu:-

  1. Msaada wa Usafiri kwa wanafunzi wanachama au wanafunzi wa wanachama;
  2. Kipaumbele cha Ajira;
  3. Mikopo isiyokuwa na Riba;
  4. Lishe kwa wenye virusi vya Ukimwi na Ukimwi;
  5. Mafao kwa Wazee;
  6. Mafao kwa Wastaafu;
  7. Msaada wa Kisheria;
  8. Gharama za Elimu;
  9. Gharama za Matibabu ya Rufaa na yasio ya Rufaa
  10. Msaada wa kusafirisha Wagonjwa;
  11. Mazishi/Rambirambi na
  12. Harusi/Jubilee.

 

Huduma za Jumla

Huduma hizi zinatolewa au zitatolewa kwa jamii nzima bila kujali kuwa mwananchi ni mwanachama au la.

1.Usajili wa Wanachama kwa hiari;

2.Kutoa Ajira kwa Vijana na Wastaafu;

3. Kuzuia Ajali na Majeruhi au Vifo vitokanavyo na Ajali;

4. Kuzuia na kutuliza Ghasia, Vita, Virusi vya Ukimwi na Ukimwi;

5. Kutoa Msaada wa Matibabu ya Rufaa na yasio ya Rufaa, Elimu ya Chekechea, Msingi,      

    Sekondari na Chuo kwa Mayatima,Wakimbizi, watoto wa walemavu na watu maskini

    wasiokuwa na uwezo wa kumudu ada za viingilio na michango au ada za uanachama wa

    shirika;

6. Kutoa Msaada wa chakula, mavazi na malazi kwa wahanga wa njaa, vita,Maafa na Majanga;

7. Kusimamia Mazingira,Sheria,Wajibu, Haki za Binadamu na Usafiri wa nchi kavu na majini;

8. Kulinda Usalama wa Raia na Mali zao kwa kushirikiana na wadau wengine;

9. Kuyasaidia Mashirika ya Kiserikali na yasio ya Kiserikali yanayotoa huduma zinazofanana na shirika mama na kutoa Elimu ya Wema na Ubaya kwa Watoto na Vijana ikiwa ni kuwaandaa Kiroho, Kimwili, Kiakili, Kisaikolojia, Kijamii, Kiuchumi na Kiutamaduni ili kuzuia, kupambana, Kukabiliana na Kushinda changamoto ambazo zinaikabili au zingeikabili jamii.


AINA ZA UANACHAMA


(1) Kibarua au  Mjasiriamali Mdogo                 

(2) Mfanyakazi au Mjasiriamali Asiye Rasmi

(3) Mfanyakazi au Mjasiriamali Rasmi

(4) Asiyeweza Kufanya Kazi( Mtegemezi)

(5) Mwasisi wa kuteuliwa (Mwakilishi)
 


UTARATIBU NA MASHERTI YA KUSAJILI WANACHAMA WA SHIRIKA

(A) MWANACHAMA WA KAWAIDA

Mtu yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka kumi na minane (18) anaweza kuwa Mwanachama wa Shirika kwa kulipa Ada ya Kiingilio au Uanachama kulingana na Aina ya Uanachama na Kipato alichonacho kwa mwezi kama ifuatavyo:-


 AINA YA UANACHAMA                 KIWANGO CHA ADA                  KIPATO KWA MWEZI

 

Kibarua au Mjasiliamali Mdogo                                  T.Shs 16,000/=                                        T.Shs 1,600/= -T.Shs 160,000/=

Mfanyakazi au Mjasiriamali Asiye Rasmi    T.Shs 50,000/=                                         T.Shs 1,601/= -T.Shs 500,000/=

 

 

Mfanyakazi au Mjasiriamali Rasmi           T.Shs 100,000/=                  T.Shs 500,001 nk.                                                                                                                   

Asiyeweza Kufanya Kazi (Mtegemezi)                      T.Shs 0                                                        Chini ya T.Shs 1,600/=
 
 
 

(B) MWASISI WA KUTEULIWA /MWAKILISHI/MJUMBE KATIKA KAMATI YA UONGOZI

Mtu anayetaka kuwa Mwasisi wa Kuteuliwa, Mwakilishi au Mjumbe wa Shirika katika Kamati ya Uongozi, kwa kuchaguliwa au Kuteuliwa mwenye sifa ya kuwa Mwasisi wa Kuteuliwa, Mwakilishi au Mjumbe atalipa Ada kulingana na ngazi kama ifuatavyo:-

           

 Ada

 T.Shs 200,000/=

T.Shs 300,000/=

T.Shs 400,000/=

T.Shs 800,000/=

T.Shs

1,600,000/=

T.Shs 5,000,000/=

 Ngazi ya Uwakilishi

MTAA au KIJIJI

KATA

TARAFA

WILAYA

MKOA

TAIFA

 

 (C)   MTU ANAETAKA KUFANYA KAZI NDANI YA SHIRIKA

Mtu yeyote asiyemwanachama wa shirika, mwenye sifa na anahitaji kufanya kazi ndani ya shirika atalazimika kupitia njia zifuatazo kabla ya kuwa mfanyakazi wa Shirika:-

(i)        Ataandika barua ya Maombi ya  nafasi ya Uanachama na Kazi;

(ii)               Atajiandikisha kuwa Mwanachama wa Shirika kwa kulipa ada ya uanachama  isiyorudishwa T.Shs 50,000/=;

(iii)             Atasajiliwa kwa kulipa Ada ya Fomu ya Uanachama T.Shs 10,000/=;

(iv)             Atafanyiwa usaili;

(v)               Atahudhuria Mafunzo ya Kazi kwa nadharia kwa muda wa siku saba (7;)

(vi)             Atahudhuria Mafunzo ya Kazi kwa Vitendo kwa muda wa siku ishirini na tatu (23;)

(vii)          Atajaza Mkataba wa Kazi utakaoonesha kiasi cha Mshahara kwa mwezi, Posho ya Kujikimu awapo nje ya eneo la kazi, Makato ya 5% ya mshahara kwa ajili ya kuweka Akiba katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii na10% ya Mshahara kwa ajili ya Ada ya Uanachama kwa mwezi; na

(viii)        Atapewa muda wa Matazamio usiokuwa chini ya miezi mitatu na usiozidi miezi kumi na miwili na kulipwa posho ya kujikimu 50% ya kiwango cha Mshahara kabla ya kuthibitishwa kazini rasmi na kupata Mshahara kamili.

 

 

 

Utaratibu Wa Kuajiri Wakuu wa Shirika na Makatibu Watendaji

Utaratibu wa kutangaza nafasi za Uanachama na kazi kwa ajili ya kuwapata Wakuu wa Shirika na Makatibu Watendaji hufanywa kwa Awamu kuanzia ngazi ya juu hadi chini kulingana na mahitaji.

 

 

VIWANGO VYA ADA ZA MAOMBI YA UWAKILISHI/UJUMBE KATIKA KAMATI ZA UONGOZI

Baada ya wanachama walau mia moja arobaini na wanne(144) kuandikishwa katika eneo husika na nafasi za Uwakilishi au Ujumbe kutangazwa, mwanachama atatuma maombi kulingana na ngazi kama ifuatavyo:-

 

 Ki           

 Ada

 T.Shs 20,000/=

T.Shs 30,000/=

T.Shs 40,000/=

T.Shs 80,000/=

T.Shs 160,000/=

T.Shs 500,000/=

 Ngazi ya Uwakilishi

MTAA au KIJIJI

KATA

TARAFA

WILAYA

MKOA

TAIFA

 

DHAMANA YA NAFASI YA UJUMBE/ UWAKILISHI AU UTUMISHI

Ujumbe au Uwakilishi au Utumishi

Mwanachama yeyote asiye au aliye katika sekta rasmi ndani na nje ya shirika au Mjasiliamali mdogo au wa kati mwenye sifa ya kuwa mjumbe au Mwakilishi au mtumishi wa Shirika kwa ngazi yoyote, atawaleta wadhamini kumi na wawili (12) wasiokuwa wanachama wa shirika ambao watakubali kuwa wanachama wa shirika ili wapate mafao au huduma stahili za shirika.

 

MUDA WA KUANZA KUPATA MAFAO AU HUDUMA ZA SHIRIKAs

(A)          MWANACHAMA WA KAWAIDA

Mwanachama wa kawaida baada ya kutimiza vigezo na masherti ya kupata mafao ataanza kupata mafao baada ya kuchangia ada ya Uanachama wake miezi mitatu mfululizo.    

 

 

 (B)            MWANACHAMA TEGEMEZI

Mwanachama Tegemezi yaani mzee asiyejiweza, yatima, mlemavu na mgonjwa wa muda mrefu asiyeweza kufanya kazi, atapata Mafao kulingana na uthibitisho wa balozi, Kamati Tendaji au ya Uongozi wa Shirika au Serikali ya Mtaa au Kijiji chake.

 

(C)           MJUMBE AU MWAKILISHI

Mjumbe au Mwakilishi atapata Mafao kulingana au kutegemea na uwezo wa Kamati yake kifedha kupitia Akaunti ya Kamati Tendaji au ya Uongozi katika eneo lake.

(D) MTU ASIYEKUWA NA KIPATO

Mtu yeyote asiyekuwa na kipato kama vile mlemavu, mzee na mgonjwa wa muda mrefu atapata huduma zaShirika bure kupitia Kamati ya Uongozi iliyopo katika eneo analoishi.

POSHO YA VIKAO

          Mjumbe au Mwakilishi

Kila mwezi Mjumbe au Mwakilishialiyehudhuria kikao atalipwa posho asilimia kumi (10%) ya Ada ya Uwakilishi au Ujumbe aliyolipa katika Kamati ya Uongozi.

     

MICHANGO AU ADA ZA UANACHAMA KILA MWEZI    

 Mwanachama asiye au aliye katika sekta rasmi ndani na nje ya shirika au Mjasiliamali mdogo au wa kati,atachangia au atalipa au atakatwa ada ya uanachama kila mwezi 10% ya pato au mshahara wake wa mwezi kama kigezo cha kupata mafao au huduma stahili za shirika.

AKIBA

Mwanachama asiye au aliye katika sekta rasmi ndani na nje ya shirika au Mjasiliamali mdogo au wa kati,anaetimiza wajibu wake, shirika kupitia michango au ada yake ya uanachama, kila mwezi atawekewa akiba ya uzeeni kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii mfano NSSF nk.

NB: Ada na michango katika nchi wanachama wa APAPO itategemea na msimamo wa thamani

       ya Dola ya Marekani katikanchi husika.

 

VIGEZO NA MASHARTI RAHISI

Iwapo Mwanachama, mjumbe au mwakilishi au mtumishi atasimama au atagoma kutekeleza au kutimiza wajibu wake katika shirika makusudi au kwa njama atapoteza haki zake za msingi.

 

 

SHUGHULI KUBWA YA APAPO

Shughuli kubwa ya APAPO ni kuwaelimisha wananchi ili wajitambue, waamke, waungane, wajitegemee na wajiajili kwa kutumia rasilimali walizonazo pamoja na vyanzo vingine vya Mapato ya Shirika katika kujiinua kiuchumi na kujikomboa dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi miongoni mwao badala ya kubweteka, kunung’unika, kulaumu na kusubiri serikali zenye kuelemewa na mzigo mkubwa na hivyo kushindwa kumudu mahitaji mengine ya wananchi kwa wakati.                                                                                        

MAJUKUMU NA WAJIBU WA VIONGOZI NA WATENDAJI WA SERIKALI ZA MITAA KWA SHIRIKA

Pamoja na Sera ya Taifa ya Ajira 2008 inayobainisha Majukumu na Wajibu wa kila mdau, ili kufikia lengo lililokusudiwa ikiwa ni pamoja na kupunguza au kuondoa tatizo la ukosefu wa Ajira na viwango vya ajira isiyokidhi kiwango, Viongozi na Watendaji wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa watakuwa na wajibu ufuatao kwa Shirika:-

·         Kulitambulisha Shirika katika ngazi zingine za Utawala kwa  wakati;

·   Kushirikishana na kushirikiana bila kuingiliana wala kupingana katika kuielimisha jamii juu ya utumiaji wa rasilimali walizonazo ili kuondokana na tatizo la umaskini, ujinga na maradhi na kuweka wazi mipaka ya uwajibikaji;

·         Kutoa ushauri wa mara kwa mara katika utekelezaji wa majukumu yake ili kuleta tija katika jamii;

·    Kufuatilia na kusambaza taarifa za nafasi za kazi kwa jamii nzima mara zinapotangazwa hna kuziingiza kwenye kanzi ya taarifa za soko la Taifa la Ajira;

·         Kufanya Ubia na Shirika kwa kutoa fursa ya kutumia ofisi za serikali za mitaa ngazi ya mtaa/kijiji kuwa vituo vya Huduma za Shirika kwa wananchi wa maeneo husika ikiwa ni pamoja na Uandikishaji Wanachama wa Shirika, Mayatima, Wazee, Walemavu na wagonjwa wa muda mrefu wasio na kipato;

·         Viongozi wa ngazi zote (mfano Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa/kijiji) kukubali kuwa walezi wa Shirika ngazi husika watakaohudhuria vikao vya Kamati za Uongozi wa shirika kila mwezi kikatiba, kuwashauri viongozi wa shirika na kuhakikisha utekelezaji wa mpango huu kwa jamii ya eneo husika.

·         Viongozi wa Kata kukubali kuweka na kusaini Mkataba wa Utekelezaji wa Mpango huu na makubaliano ya kupokea 10% ya Mapato ya Shirika kutoka kila Mtaa/Kijiji kila baada ya miezi mitatu (3) kwa ajili ya Utekelezaji wa Shughuli za Maendeleo ya Kata husika.

 

 

SEMINA ELEKEZI KWA VIONGOZI NA WATENDAJI WA SERIKALI ZA MITAA

Kwa mujibu wa kanuni za ushirikishaji wa wadau wengine wa Maendeleo, Maofisa wa shirika watakuwa na wajibu wa kutoa Semina Elekezi endelevu kila inapobidi kwa viongozi na watendaji wa Serikali za Mitaa wenye lengo la kushirikiana na kuliunga mkono Shirika katika utekelezaji wa majukumu ili kuwapa uelewa wa shughuli na Huduma za Shirika kwa jamii wanayoiongoza .

 

KAULI MBIU

1.      KAULI MBIU YA MPANGO

“Wananchi, Tuungane Tujitegemee”S

2.      KAULI MBIU YA AJIRA

“Wajibu na Haki “

 

MAWASILIANO

MKURUGENZI MTENDAJI………………………....+255713 121313/+255768121313

MKUU WA OPARESHENI.......................................................................+255764876045

 

BARUA PEPE:  apapoafricatz@gmail.com

TOVUTI: WWW. Envaya.org/apapo

 
  

           

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles