Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

african poor and patient organization updated its Projects page.

$
0
0

 

Shirika baada ya kupata nguvukazi (Wanachama Wafanyakazi) katika nchi na mikoa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Tanzania (Rukwa, Tabora, Katavi na Kigoma,) Wanachama Waliofuzu Mafunzo ya Kazi kwa nadharia na wengine Mafunzo ya kazi kwa vitendo ngazi ya mkoa, limekwishaanza kuwapeleka maeneo ya kazi na wengine maeneo ya Mafunzo ya Kazi kwa vitendo katika nchi na mikoa mbalimbali barani Afrika.

Aidha nchini Tanzania mkoani Dar Es Salaam baada ya Shirika kushirikiana na mamlaka za Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa  mkoa wa Dar Es Salaam ngazi ya mkoa hadi mtaa, kupitia Mkuu wa shirika mkoani humo Bi. Paskazia Mauki, linatoa nafasi kwa wananchi kujiunga na kufanya Kazi na Shirika ngazi ya wilaya katika wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke nafasi 2 kila wilaya (Nafasi ya 1 Wakuu wa Shirika na nafasi ya 2 Makatibu Watendaji.)

Nafasi ya kwanza kwa vijana na wastaafu wenye Elimu ya Stashahada na kuendelea na nafasi ya pili kwa wote wenye Elimu ya kidato cha nne na kuendelea na ujuzi wa kutumia Kompyuta  walioupata katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

                                                                    

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles