VITUO vya UKWELI NA UWAZI chenye wanachana 24 chini ya malezi ya ASMET cha Makao Mkuu ya WIPAHS, Dar es Salaam kilimaliza muda wake wa mzunguko wa kwanza na kuwa huru. Chini ya uongozi wa mwenyekiti Bi Pili na Kamati yake Tendaji walisimamia maendeleo ya Kituo na kufikisha akiba kwa mtindo wa kununua HISA zenye thamani ya Tshs. Milioni Mia Sita na kukopeshana zaidi Tshs millioni saba. Tafrija ya kumaliza mzunguko ilifanyika Makao Makuu tarehe 19 Disemba 2013 na kuhudhuriwa na mgeni rasmi Mwenyekiti wa WIPAHS, Alhaji Haji Swaib.
↧