Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Majani Natural and Scientific Health Promoters (MANSHEP) added a News update.

 

ZABIBU (Vitis vinifera L.)NA FAIDA ZA TIBA


Zabibu ni matunda yenye madini (kalishiamu, potashiamu na magnesiumu), sukari, vitamin na dawa-lishe kwa wingi.

Divai au Mvinyo Usiochacha

 

Maji ya matunda ya zabibu (juisi ya zabibu) hujulikana kama divai au mvinyo. Maneno haya ya Kiswahili yanatokana na tafsiri ya neno la Kiingereza ‘Wine’ lakini pia neno hili la Kiingereza limetoholewa kutoka katika maneno ya Kiebrania ‘Yayin’ au ‘Tirosh’ na maneno ya Kigriki ‘Oinos’au ‘Gleukos’. Maneno haya ya lugha za kale yalitumika kumaanisha maji ya matunda ya zabibu yasiyochacha, yaani divai au mvinyo mpya upatikanao katika vichala (new wine) na divai ya namna hii hapo zamani, ilitambuliwa kama kinywaji kitamu chenye baraka (Isaya 65:8; Mika 6:15) na ilitumiwa kwa kiasi kama dawa nzuri ya matatizo ya tumbo (1 Timotheo 5:23).

 

Maji ya matunda ya zabibu yaliyochacha na kuzalisha alkoholi (mvinyo uliochacha), maji ya matunda mengine yaliyochacha na vinywaji vingine vyenye alikoholi (ethyl alcohol) vilivyotengenezwa baada ya kuchachusha nafaka, vilijulikana kama ‘Shekar’ katika lugha ya Kiebrania. Ingawa wakati mwingine watu walimaanisha mvinyo au divai kama kinywaji kilichochacha kwa kutumia maneno ya Yayin na Tirosh (Hosea 4:11; Mwanzo 9:20-21), vinywaji vilivyochacha vilitambuliwa kama vinywaji vyenye madhara kwa afya na vilifananishwa na sumu ya nyoka (Mithali 23:31-35). Hii ni kutokana na ukweli wa kisayansi kuwa ethyl alcohol ina uwezo wa kudhuru seli za mwili na kuharibu afya ya ini, moyo, akili na mwili kwa ujumla. Pamoja na ukweli huu kuhusu madhara ya kiafya yaliyotokana na kunywa vinywaji vyenye alkoholi, mvinyo uliochacha hapo zamani ulitumika kama dawa ya kusafishia au kutibu vidonda na majeraha (Luka 10: 30-34). Hii ilitokana na uwezo wa alkoholi (pombe) wa kuuwa bakteria hatari wanaoshambulia vidonda na kusababisha usaha.

 

Maji ya matunda ya zabubu ambayo hayajachacha (divai au mvinyo mpya) hasa yale yanayotokana na matunda ya zabibu nyekundu, licha ya kuwa kinywaji kizuri kwa ajili ya kuimarisha afya pia ni dawa nzuri. Divai hii ina sukari ya asili inayotia nguvu katika nyama za mwili, lakini pia ina vitamin B za aina mbalimbali ambazo huimarisha afya ya neva. Divai pia ina dawa-lishe aina ya quercetin (Flavonoid), resveratrol na dawa-lishe za aina nyingine nyingi ambazo hufanya kazi za kutibu mwili.

 

Mvinyo uliochacha

 

Mvinyo uliochacha (fermented wine) ambao unatokana na zabibu nyekundu pia haupotezi dawa-lishe zinazosaidia kuleta afya ya tumbo na mishipa ya damu kwenye moyo kwa wazee wenye umri wa kuanzia miaka 50 na kuendelea. Tafiti mbalimbali huonyesha kuwa wazee wanapokunywa kiasi cha mililita 100 hadi 200 za mvinyo mwekundu kwa siku, hupunguza uwezekano wa kupata shambulio la moyo (myocardial infarction risk) kwa takribani asilimia 30 hadi 50. Dawa lishe katika mvinyo huu, hutokana na maganda ya zabibu wakati wa kukamua zabibu kabla haijachachushwa. Lakini ethyl alcohol iliyomo ndani ya mvinyo uliochacha (pombe) inadhuru seli za mwili na kusababisha matatizo ya kiafya na haina faida yoyote mwilini.

 

Faida za kiafya

·         Zabibu huupatia mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hasa ile inayosambaza damu kwenye nyama za moyo. Zabibu ni dawa nzuri kwa magonjwa mbalimbali ya moyo. Huimarisha afya ya mishipa ya damu na kuzuia ugonjwa wa kukakamaa kwa mishipa hiyo.

·         Husaidia damu kuwa nyepesi na kuzuia isigande ndani ya mishipa ya damu na kwa sababu hii zabibu hupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa kiharusi (Cerebrovascular accident) au stroke.

·         Zabibu pia inasaidia kuzuia na kutibu tatizo la upungufu wa damu mwilini.

·          Kutumia zabibu mara kwa mara huzuia na kutibu ugonjwa wa bawasili (haemorrhoeids)

·         Husaidia katika tiba na kinga ya magonjwa ya ini kwa vile huongeza uwezo wa ini wa kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi.

·         Huimarisha afya ya figo na uwezo wake wa kuondosha sumu ndani ya damu.

·         Husaidia katika matibabu ya ugonjwa unaosababisha uvimbejoto wa maungio (Arthritis) na baridi yabisi.

·         Kutokana na sukari yake ya asili, zabibu hupunguza uchovu wa mwili na kutibu maumivu yasiyokuwa na sababu bayana (Psychosomatic disorders).

·         Husaidia katika matibabu ya shinikizo la damu (hypertension).

·         Juisi ya zabibu (Divai) husaidia tumbo na utumbo kufanya kazi vizuri na kuzuia ukavu wa kinyesi (chronic constipation). Lakini pia divai huimarisha afya ya mishipa ya damu katika mfumo wa kumeng’enya, kusaga na kusharabu chakula na viinilishe. Huondosha sumu ndani ya ini na kuongeza uzalishaji wa nyongo inayosaidia kuyeyusha chakula chenye mafuta mengi kinachoingia tumboni. Divai pia husaidia bakteria rafiki kwa binadamu wanaoishi ndani ya tumbo (normal flora) kustawi vizuri na kusaidia umeng’enyaji wa chakula katika utumbo kuwa rahisi. Madini yaliyomo ndani ya zabibu, pia huifanya divai kuwa dawa nzuri inayopunguza maumivu ya tumbo yanayotokana na kujiminyaminya kwa misuli ya kuta za matumbo (antispasmodic effect).

 

Matumizi

·         Tumia (kula) kila siku vidonge (punje) vya zabibu visivyopungua vitano kwa ajili ya afya ya mfumo wa damu na nyama za moyo.

·         Kunya juisi ya zabibu (mvinyo usiochach au divai mpya) kila siku bilauli mbili, moja asubuhi moja jioni. Hakuna sababu ya kunywa mvinyo uliochacha pale unapopata faida za kiafya kutoka katika mvunyo usiochacha.

 

Rejea

  • American Heart Association,Inc : Alcohol, wine and cardiovascular diseases(2010) retrieved 3.5.2010 at www.americanheart.org/presenter.jhtml
  • Constant, J: Alcohol, ischaemic heart disease and the French Paradox. Clin. Cardiol., 20:420-424 (1997).
  • George D. Pamplona-Roger: Encyclopedia of Foods and Their Healing Power Vol. 1, Editorial Safeliz, Madrid, (2008). Pp 362 -381.
  • Kaye Middleton Fillmore, et al: Moderate alcohol use and reduced mortality risk: Systematic error in prospective studies. Addiction Research and Theory, vol.14 (2):101-132, April 2006.
  • Peatfield R.C: Relationship between foods, wine and beer-precipitated migrainous headache. Headache 35: 355-357(1995).
  • William Patton: Bible Wines; Kessinger Publishing, LLC (2003).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles