DIRA YA ASASI
kuhakikisha mabadiliko katika nyanja ya kiuchumi na kijamii yanakuwepo
katika jamii ili jamii iweze kunufaika kwayo
UTUME WA SHIRIKA
kuifanya jamii iweze kuhamasika dhidi ya kufikia malengo ya milenia
kuwajali, kuwathamini na kuwajengea uwezo wa maisha watu waishio
katika mazingira magumu hususani wanawake na vijana walio katika
hatarinikuathirika/ walioathirika kiuchumi na kijamii
MALENGO YA SHIRIKA
kwa kuwa shirika linalenga zaidi katika kupambana na umasikini, umasikini,
ujinga, na maradhi shirika limejikita zaidi zaidi katika vipengele vikuu kama
Elimu, kilimo na utunzaji wa mazingira pamoja na ukimwi na malaria,
ujasriamali, utawala bora na haki za binadamu
Hivyo:
kuushirikiana na serikali na vyombo vingine visivyo vya kiserikali vya ndani na nje ya nchi katika kutoa huduma kwa jamii.
kuainisha mahitaji na kushiriki katika kupanga nakutekeleza huduma hizo ipasavyo.
Kuishawishi Serikali na vyombo vyake ili vitoe huduma bora katika jamii kwa haki na usawa.
Kuhamasisha jamii kushiriki katikaharakati za maendeleo ndani ya Wilaya na Nchikwa ujumla.
Kubuni njia zitakazoleta Ufanisi katika vipengele vya hapo juu.
Kuandaa na kuzalisha habari zitakazosambazwa kwa Wananchi kupitia Maktaba za jamii.