Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

CHAMA CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA KIJAMII VUGA updated its Projects page.

$
0
0

 MRADI WA UTAWALA BORA NA HAKI ZA KIRAIA

UNAENDESHWA NA ASASI YA CHAMAKIVU KWA UFADHILI WA THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIATY FCS.

                                   3.0 HISTORIA YA MRADI HUU.

Mradi huu unajulikana kama mradi wa Utawala bora katika awamu hii ya kwanza mradi umewafikia watu 370 toka Kata tatu za Vuga,Usambara na Mponde za Halmashauri ya Bumbuli Wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga,

 Mahitaji ya mradi huu yametokana na Ufahamu mdogo wa sera na mipango mbalimbali katika ngazi ya Vijiji ambapo kunasababisha maendeleo ya Vijiji kuwa duni ukizingatia Vijijini ndio sehemu kubwa ya kudhalisha, Katika maeneo mengi ya Tanzania mwamko wa wananchi kufahamu sera na kushiriki katika shughuli za maendeleo na kudai mapato na matumizi ya Kijiji ni jambo lililopo kwa kiwango kidogo sana , na hivyo kusababisha kuwapa mianya viongozi wasiokuwa waadilifu kutumia nafasi hiyo kufanya wanavyotaka na kusababisha umaskini kuzidi kukithiri,

Wananchi wengi wanalalamikia serikali za Mitaa/Vijiji kutokana na wao ndio wanaokusanya mapato kwa njia ya kodi,leseni,ada na vyanzo mbalimbali vya mapato,kwa hiyo ufatiliaji wa mapato hayo ni muhimu ili Serikali za Mitaa/Vijiji walete ushawishi kwa umma kuwa mapato hayo yamepokelewa kwa kufuata sheria na kutumiwa ipasavyo kwa matumizi yalokusudiwa

Katika eneo la mradi (Kata sita za Wilaya ya Lushoto Halmashauri ya Bumbuli) Hakujawahi kufanyika mafunzo/matamasha yanayohusisha uhamasishaji na uelimishaji wa jamii juu ya utawala bora na haki za kiraia, licha ya kuwa kunapengo kubwa sana kwa wanajamii hao juu ya ufahamu wao kuhusiana na dhana ya utawala bora na haki za kiraia. katika kufahamu hali ya eneo la mradi CHAMAKIVU iliandaa Utafiti mdogo ambao ulituwezesha kufahamu kuwa uwelewa wa wakazi wa maeneo hayo ni mdogosana

Watu wachache waliohojiwa ( 100 ) katiyaoni asilimia 12% ndo waliofahamu dhana ya utawala bora na ;-

  • 8% ya wananchi wanashiriki katika shughuli za maendeleo
  • 6% ya wakazi wanashiriki katika mipango
  • 4% ya wakazi walioshiriki katika mikutano
  • 1.5 ya wakazi waliodai taarifa.
  • 22% ya mabango yanawekwa katika mbao za matangazo.
  • Takwimu hizi si za kuridhisha ukilinganisha na takwimu za kitaifa.

Katika kuchochea maendeleo katika eneo la mradi CHAMAKIVU imepanga kuongeza asilimia kumi kwa kila eneo kutokana na uhamasishaji na uelimishaji utakaoendeshwa na mradi huu

 

4.0 MALENGO YA MAFUNZO

  1. Kuwaongezea ufahamu kwa viongzozi juu ya kujua majukumu yao kwa kufuata misingi ya utawala bora
  2. Kuwawesha jamii kujua majukumu ya viongozi wao kwa mujibu wa Katiba na sheria mbalimbali za serikali za Mitaa/Vijiji
  3. Kuwawezesha wananchi kudai/kuhoji taarifa za mapato na matumizi kwa mujibu wa Katiba na sheria mbalimbali za serikali za Mitaa/Vijiji
  4. Kuwawesha wananchi kushiriki katika kupanga,kutekeleza na kutathimini shughuli za kijiji kwa mujibu wa Katiba na sheria mbalimbali za serikali za Mitaa/Vijiji
  5. Kuwawezesha wananchi kushiriki katika mikutano ya serikali za Vijiji kwa mujibu wa katiba ya nchi na sheria mbalimbali za serikali za Mitaa/Vijiji

6. Kuwawezesha wananchi kufahamu umuhimu wa kushiriki katika shughuli za maendeleo zakujitolea

 

5.0 SHUGHULI ZILIZOFANYWA KATIKA MRADI HUU

1) Kutoa mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa Vijiji/Kata wadau wa maendeleo na wananchi juu ya masuala ya utawala bora na uwajibikaji,

Jumla ya viongozi wa Kata, Vijiji/Vitongoji na wajumbe wa Halmashauri za Vijiji 190 na wananchi 180 waliudhuria katika mafunzo ya utawala bora ngazi ya Kaya, Wanawake 200 na wanaume 170 jumla 370,

Wananchi waliweza kutoa kero zao zinazowasumbua

Kero ni:-

v  Viongzozi kutotimiza wajibu wao wa utoaji wa huduma za kijamii na badala yake kuwepo na michango mingi

v  Kutotekeleza mipango iliyopangwa na wananchi

v  Wananchi kuletewa miradi tofauti na mahitaji yao

v  Viongozi kutumia siasa vibaya

v  Viongozi kuwa bize katika vikao vya Halmashauri kuliko kuhudumia wananchi katika ngazi ya kijiji na Kata

v  Wataalamu na viongozi kuingiliana majukumu

v  Viongozi kuwa wakali sana kwa watu kwa kutoa amri badala ya kutushirikisha na kutuelemisha kwanza

v  Wamekuwa watu wa kutoa maamuzi

v  Viongozi wa kike kunyanyaswa kutokana na jinsia yao

v  Kiongozi kuweka ofisi nyumbani kwake badala ya jengo la serikali

v  Viongozi wamekata taamaa ya kuwahudumia wananchi na badala yake wamekuwa wakisubili miradi kutoka Halmashauri

v  Mafunzo yanapotokea wanaopelekwa hawaludishi mrejesho kwa wanakijiji

v  Sheria nyingi ndogo ndogo zimekuwazikitungwa na Halmashauri lakini jamii hawazifahamu sheria hizo na hivyo utekelezaji wake unakuwa mgumu na kusababisha malumbano kati ya viongozi na wananchi.

 

Kero za viongozi;-

  • Kukosekana kwa vitendea kazi
  • Kutopatiwa mafunzo ya mara kwa maa
  • Wajumbe kuzarau vikao
  • Ukosefu wa yunifom
  • Kutopewa posho kwa watendaji/wenyekiti wa vitongoji
  • Kutohusishwa katika vikao vyote

 

 

Mada ni :-

  • Haki na wajibu wa raia
  • Dhana ya demokrasia
  • Utawala bora na utawala wa sheria
  • Ushiriki na ushirikiswaji
  • Muundo wa serikali za mitaa/vijiji
  • Sifa za kiongozi bora
  • Jinsi ya kumuwajibisha kiongozi
  • Kazi za viongozi wa Vijiji na Kata
  • Mipango shirikishi
  • Utekelezaji wa shughuli za mipango iliyobuniwa ya kuleta maendeleo
  • Jinsi ya kubuni mipango
  • Usimamizi na udhibiti wa fedha
  • Jinsi ya kuweka vipaumbele

Mwezeshaji alitoa vichangamsho washiriki waliimba na kucheza na kuwafanya wachangamke kila mara na kuwa tayari kwa ajiri ya kupokea masomo

mwezeshaji aliweza kueleza mambo mbalimbali katika uongozi stadi za uongozi

  • Kujua unaowaongoza na kuchambua mahitaji ya jamii unayoingoza
  • Kutafuta njia ya kupokea na kutosheleza mahitaji yao
  • Kuzingatia jinsi watu unaowaongoza wanavyojisikia
  • Kutambua mahitaji na matarajio ya wananchi unaowaongoza
  • Kuwa tayari kukiri na kusahihishwa makosa
  • Kuwa jasiri katika utendaji
  • Kuwa tayari kujirekebisha

 

Muezeshaji aliwasilisha mada yake iliyojikita kwenye ufahamu wa jinsi ya kufanya uchambuzi katika uongozi aligawa makundi na kila kundi alilitaka kuleta majukumu yake akiwa yeye ndio kiongozi

a)   Watenda wa Vijiji /Kata na Madiwani        

1             Kushirikisha/mshirikishaji

2             Ushawishi

3             Mbunifu

4             Mwenye maono

5             Mwenye kutoa motisha

6             Mwenyekugawa majukumu

7             mwenye kuwa na mpango kazi wa muda mrefu na mfupi

8             Mfuatiliaji na mwenye kutathimini

b)       Kuorodhesha majukumu kama kiongozi wa kijamii

1        kufuatilia huduma za kijamii        

2        kufanya utafiti wa mahitaji katika jamii

        3        kuweka kumbukumbu

          4        kutoa mrejesho

 c)       viongozi wa dini taasisi, maimamu na maskofu

          1        kulea waumini kiroho na kimwili

          2        kuwahimiza waumini kuwa na maadili mema

          3        kulinda na kutetea maslahi ya waumini

Viongozi wa elimu maafisa wa elimu wa Kata na walimu wakuu

1             Kusaidia utoji wa taaluma shuleni

2             Kusimamia matumizi ya fedha ya umma

3             Kuhakikisha shule inamiuondombinu sahihi

4             Kusimamia nidhamu ya walimu,wanafunzi na watumishi wengine wa Shuleni

5             Kusimamia vikao na kuweka kumbukumbu

6             Kuwa kiungo kati ya shule na jamii

7             Kuwa na mpango kazi wa muda na mbadala

8             Kuhudhuria vikao vya kijiji na Kata

Mwisho mwezeshaji alijumuisha mada iliyomezani na kuongeza kazi za kila kundi

Mwezeshaji pia aliwapa faida za mawasiliano katika uongozi jambo ambalo walishindwa kulitaja katika makundi yote na kueleza kuwa faida za mawasiliano ni:-

1             Kuokoa muda

2             Kupata taarifa kwa wakati

3             Kupunguza malalamiko

4             Kuinua pato la jamii na taifa

5             Kupata marafiki

6             Kuelimika

7             Kupunguza migogoro

8             Ni kiunganishi kati ya jamii na viongozi

 

Mwezeshaji aliwaeleza vizuizi vya mawasiliano ili kuwafanya waweze kuwa makini katika njia hii ya mawasiliano

1             kukosa kipato

2             kuwa na miundombinu mibovu

3             kukosa lugha nzuri ya kuwasiliana

4             kutoitisha vikao

5             kucheleweshwa au kutotoa mrejesho

6             migogoro na migongano katika mazingira

7             maumbile ya watu mfano walemavu

 

6.0 MATOKEO

Watendaji/Wenyekiti katika ngazi ya Kijiji na Kata wamefahahamu umuhimu wa uwazi,uwajibikaji katika majukumu yao ya kila siku.                                  kutokana na mafunzo haya viongozi hawa wamefahamu jinsi ya kutofautisha majukumu yao binafsi, kifamilia na ngazi waliokuwa katika jamii jambo ambalo mwanzoni hawakufahamu na muda mwingi walikuwa wakitumia katika mambo yao binafsi,familia na safari nyingi za Halmashauri kuliko kuwatumikia wananchi ilifikia wakati ndani ya wiki ofisi ya kijiji hufunguliwa mara mbili hadi tatu na si kwa masaa ambayo kiongozi huyo anatakiwa kukaa katika ofisi hiyo.

Viongozi wamelewa jinsi ya kutengeza kalenda ya msimu jambo ambalo lilikuwa hawalifahamu na kusababisha wananchi wengingi kutoudhulia katika mikutano ya Vijiji kutokana na siku za mikutano huwa kipindi cha kulima,mavuno,siku ya soko na siku za ibada hivyo wameweza kufahamu jinsi ya kupanga kalenda ya msimu.

Wamefahamu jinsi ya kupanga vipaumbele na aina tatu za kupanga vipaumbele

  • kuanisha vipaumbele kwa njia ya kupiga kura
  • kuainisha vipaumbele kwa njia ya utashi
  • kuinisha vipaumbele kwa mlinganisho kijozi

 

Viongozi wamefahamu jinsi ya kuweka mapato na matumizi katika mbao za matangazo

Viongozi wamefahamu kamati kuu tatu ambazo ziko kisheria nazo ni:

  • Kamati ya fedha mipango na uchumi
  • Kamati ya huduma za kijamii
  • Kamati ya ulinzi na usalama

Na kufahamu kamati zingine ni kamati ndogo ndogo zinazotokana na kamati kuu tatu jambo ambalo mwanzoni viongozi hao walichanganya kamati na kushindwa kutofauti kamati ambazo zipo kisheria na zile zilizotoholewa kutoka katika kamati kuu tatu,

 

Viongozi wamefahamu kuwa kamati hizo tatu za kisheria inashauri kuwa mwenyekiti wa Kitongoji/Kijiji asiwe kiongozi katika kamati hizo na badala yake kati ya wajumbe ndio wawe kiongozi katika kamati hizo na wamejua sababu za kwanini wameshauriwa hivyo.

 

Viongozi wamefahamu kuwa wanaweza kumualika mwananchi wa kawada wanawezaq kumualika katika mkutano wa Halimshauri ya kijiji kutoa ushauri wake ikiwa kunasababu ya kumualika mwananchi huyo

7.0 MATOKEO KWA WANANCHI

wananchi wametambua kuwa wanahaki ya kushiriki katika mikutano ya Kijiji na kuhoji mapato na matumizi,

mwanzo wananchi walikuwa hawashiriki mfano:

Kuna wafanya biashara walikuwa wakija kukata miti katika kijiji cha Vuga lakini wananchi hawakushirikishwa na hawafahamu pesa za mfanyabiashara huyo zimekwenda wapi? Kutokana na mafunzo haya wananchi wamepeleka kesi kwenye vyombo vya sheria na sasa linashughuilkiwa. Mfano mwengine ni wanakijiji walikuwa wakihukumiwa kutokana na sheria ambazo zinakiuka katiba ya nchi katika kijiji cha kwemzuza mwananchi ambae hakubaliani na matakwa ya viongozi basi huchukuliwa mifugo kama fidia kutokana na kuhoji au kumpinga kiongozi bila kufuata utaratibu wa kisheria na wananchi hawashirikishwi katika maaamuzi badala yake wanaleta maagizo tu wa nini wafanye.

Kwa sasa wananchi wamefahamu majukumu yao kama vile kuhakikisha kiongozi aliyemchagua anatimiza wajibu wake ipasavyo na anaongoza wananchi kwa mujibu wa sheria na pia wamefahamu kuwa wana haki ya kupinga uonevu katika jamii ikiwemo rushwa,uonevu,wizi na ubadhilifu wa mali za umma.

 

  • Wananchi wamefahamu maana ya:-
    • Kitongoji,
    • Kazi za Mwenyekiti wa Kitongoji
    • Majukukumu na madaraka ya Mwenyekiti wa Kitongoji,
    • Maana ya Kitongoji,
    • Kazi za Kitongoji,
    • Maana ya Kijiji,
    • Madaraka na majukumu ya mkutano mkuu wa Kijiji,
    • Maana ya Halmshauri ya Kijiji
    • Mamlaka na majulumu ya Halmashauri ya Kijiji,
    • Maana ya kamati za Halmashauri ya Kijiji,
    • majukumu ya Halmashauri ya Kijiji.
    • Wananchi wamefahamu wajibu wa kila mwanakijiji katika kijiji
    • Maana ya ushiriki na ushirikishwaji katika mipango ya Kijiji
    • Wananchi wamefahamu jinsi ya kumtoa mwenyekiti wa Kijiji au mjumbe nai kupeleka mapendeko katika Halmashauri ya kijiji na wao kupiga kura na kuludishwa katika Mkutano mkuu wa Kijiji

      8.0 MIKAKATI YA WANANCHI

      Wananchi kutokana na ufahamu walioupata kwa sasa wamehaidi:-

      • Kuhudhuria katika mikutano ya Kitongoji,Kijiji na kuhakikisha inafanyika mikutano hiyo kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.  
      • Kushiriki katika kupanga,kusimamia,kufuatilia na kutahimini matokeo yote ya miradi
      • Kufuatilia mapato na matumizi ya fedha za Kitongoji/Vijiji
      • Kushiriki katika

        9.0 CHANGAMOTO

        Baada ya warsha ya siku 2 ya watendaji Kata/Madiwani na wadau wa maendeleo kufanyika kwa ustadi mkubwa na kumtumia Israel Ilunde katika kuwezesha warsha hiyo,

        Mtendaji wa Kata ya Vuga ALLY SHEKHAWA ambae alikuwa Katibu katika warsha yetu aliandika barua kwa watendaji wa vijiji vya Kata ya Vuga wasishiriki na wazuie wenyekiti wa vitongoji na wananchi wanaoishi katika vijiji/vitongoji hivyo kutoshiriki na kushirikiana na CHAMAKIVU katika mikutano ukizingatia ndio kipindi ambacho tulipanga ratiba ya kwenda kutoa mafunzo katika vijiji hivyo ikiwa ni moja ya utekelzaji wetu wa mradi, Mtendaji huyo aliandika barua hiyo na kuwapa watendaji wa Vijiji nakala kupeleka Polisi ya Tarafa ya Soni, Mkuu wa Wilaya kwa kudai kuwa hatukufuata taratibu, Bila sisi CHAMAKIVU kutupatia barua hio, Ofisi ya CHAMAKIVU na ofisi ya Kata zinangalina hakuna taarifa yoyote ambayo alitupatia au katazo la sisi kusitisha utekelezaji wa mafunzo yetu wakati taarifa ya utekelezaji wa mradi anayo na anafahamu mwaka mzima tutafanya nini, Baada ya muda tulifikiwa na ugeni kutoka Lushoto na Soni ni wakuu wa upelelezi na kufika ofisi ya CHAMAKIVU na kufanya mazungumzo na mratibu JUMAA I DHAHABU na maofisa hao waliahidi kushirikiana nasi baada ya kugundua taarifa walizozipata kwa mtendaji huyo ni tofauti na walivyokuja kujionea katika kazi zetu

        Kutokona na changamoto hiyo tuliwasiliana na wadau wengine wa Asasi za kirai na Afisa maendeleo wa Wilaya ya Lushoto,Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya Bumbuli watu ambao ni miongoni mwa watu waliyoshiriki katika warsha ya viongozi ambayo tulifanya katika mradi huu . CHAMAKIVU haikuishia hapo ilikwenda moja kwa katika ofisi ya mtendaji huyo na kukutana na Afisa huyo na kumtaka Atupe sababu za kuzuia mafunzo hayo, na kumpa taarifa ya hatua tutakazo chukuwa ikiwa mradi huo utatekelezwa chini ya kiwango basi

        tutafungua mashtaka na kutulipa fidia ya gharama zote za mradi,gharama za muda tuliotumia lakini hatawajibika kwa jambo lolote ambalo jamii litawapata kutokana na kukosa haki yao ya kikatiba ya kupata taarifa juu ya utawala bora ambayo ipo katika sera na MKUKUTA

        Baada ya hapo walipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa Asasi isiyo ya kiserikali ya TAYODEA ndugu DAVID CHANYEGHEA akitakiwa kuruhusu shughuli za CHAMAKIVU ziendelea haraka na asipofanya hivyo basi atakuwa anakiuka na hatua za kisheri zitachukuliwa zaid,i na kutokana habari hizo kutoa katika gazeti la HABARILEO na hapo mtendaji aliandika barua ya kuwaruhusu watendaji wake kushirikiana na CHAMAKIVU baada ya siku 2 za mvutano na kuendelea na mafunzo katika vijiji

      11.0 SHUKRAN

      • THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIATY FCS- Kutupatia ufadhili mara kwa mara, kutupatia mafunzo mbalimbali ya kutujengea uwezo wa ASASI na mafunzo ya usimamizi wa miradi na kutuletea wataalamu kuja ofisini kwetu kuangalia shughuli zetu ikiwepo ukaguzi wa miradi wanayotufadhili.
      • MH MBUNGE WA JIMBO LA BUMBULI- Kuomba MADIWANI wa Jimbo la Bumbuli kushiriki katika mafunzo hayo bila kukosa kupitia Katibu wake.
      • MKURUGENZI HALMASHAURI YA BUMBULI- Kutambua mafunzo haya na kutoa muwakilishi kutoka katika ofisi yake kushiriki katika mafunzo hayo.
      • MWALIMU MKUU SHULE YA VUGABAZO SEC SCHOOL- MW. MTEMI- Kutupatia ukumbi na viti kipindi cha mafunzo,
      • MTENDAJI KATA YA MPONDE, WENYEKITI NA WATENDAJI WA VIJIJI VYA KATA YA MPONDE- Kwa kuhamasisha washiriki kuhakikisha kuwa wanashiriki bila kukuosa hata mmoja na kuamua kusitisha shughuli zote katika kipindi cha mafunzo yaliofanyika katika Kata ya MPONDE
      • MH. DIWANI KATA YA USAMBARA, WENYEKITI NA WATENDAJI WA VIJIJI VYA KATA YA USAMBARA- Kwa kuhamasisha washiriki kuhakikisha kuwa wanashiriki bila kukuosa hata mmoja na kuamua kusitisha shughuli zote katika kipindi cha mafunzo yaliofanyika katika Kata ya USAMBARA

       

      • AFISA MAENDELEO YA JAMII WILAYA YA LUSHOTO, TUMAINI GWATALILE, Kutupatia baazi ya wawezeshaji kutoka Halmashauri ya Wilaya Lushoto kutoka IDARA YA MAENDELEO JAMII JINSIA NA WATOTO LUSHOTO.
      • POLISI JAMII TARAFA YA SONI, DORINA KHAMIS POYO INSP.- Kushirikiana na ASASI katika shughuli mbalimbali pia kusaidia kujibu maswali ya kisheria yanayohusu jeshi la POLISI yanayoulizwa na jamii katika mafunzo tunayoendesha, pia amekuwa akija kwa upole ofisini kwetu akipewa taarifa za uchochezi na baadhi ya watendaji na wanasiasa wanopinga mafunzo haya na pia amekuwa mtetezi kwa maafsa wengine wanaopewa taarifa za uchochezi zidi yetu.
      • MRATIBU ELIMU KATA YA VUGA- Amekuwa karibu nasi na kutushauri hususani anapokaimu nafasi ya mtendaji Kata akiwa hayupo lakini pia amehamasisha walimu walioalikwa wameshiriki wote,
      • ISRAEL ILUNDE- MWEZESHAJI ktoka KIBAHA MKOANI WA PWANI ambae washiriki walimfurahia sana kipindi chote cha mafunzo,
      • FATMA DAUDI SAID- MWEZESHAJI kutoka ofisi ya MAENDELEO YA JAMII Lushoto mwnafunzi wa Chuo kikuucha TUMAINI UNIVERSITY-IRINGA
      • EDWARD YOHANA– MWEZESHAJI- kutoka ofisi ya MAENDELEO YA JAMII LUSHOTO na mwanafunzi RUAHA CDTI IRINGA.
      • SABITINA A MAKWALA– MWEZESHAJI kutoka ofisi ya MAENDELEO YA JAMII LUSHOTO na mwanafunzi wa chuo cha MONDULI CDTI ARUSHA,
      • WATENDAJI NA WENYEKITI WA VIJIJI VYA KATA YA VUGA- kuhamasisha washiriki wa mafunzo kushiriki bila kukosa pamoja kuzuia na mtendaji wa Kata ya Vuga hawakusitisha washiriki kwa haraka na badala yake wakatupa taarifa haraka na kutusaidia kuhakikisha mafunzo haya yanafanyika kwa maslahi ya jamii ya Vuga,
      • MKURUGENZI WA TAYODEADAVID CHANYEGHEA- Kusaidia kuwakemea watendaji wa Kata kuzuia mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa vijiji/vitongoji na jamii.
      • WANACHAMA NA VIONGOZI WA CHAMAKIVU- Kujitolea na kusimamia shuguli za ASASI muda wote wa mafunzo.

                                           

    •                                          12.0 HITIMISHO

      Dhana ya utawala bora kama ilivyofafanuliwa katika Dira ya Taifa ya mwaka 2025 na MKUKUTA II, Inatuelekeza kwenda na utamaduni wa uongozi shirikishi, sikivu,unaoishi utamaduni wa demokrasia kwa kauli na vitendo,

      Tumepata kwa muhtasri matarajio ya wananchi ndani ya Dira ya Taifa na MKAKATI WA KUKUZA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASIKINI TANZNIA, Imetueleke

      za kujadili misingi ya UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI na kusisitiza ushiriki wa Wananchi wote katika shughuli,masuala na michakato ya Umma ili kuharakisha maendeleo.

      Nimatarajio yetu kutokana na mafunzo haya ya UTAWALA BORA tulioendesha kwa Viomgozi na Wanajamii walioshiriki watailetea jamii mafanikio ya maendeleo ya kweli na endelevu kwa kusimamia misingi ya

      UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI.

        

      JUMAA I. DHAHABU

      MRATIBU & MSIMAMIZI WA MRADI

      0716215064/0785810064

        AWAMU YA KWANZA OCTOBA -  DESEMBA 2013

 

 

 

 

MABARAZA YA KATIBA MPYA, WAENDESHAJI CHAMAKIVU WAFADHILI THE FOUNDATIO FOR CIVIL SOCIATY

CHAMA CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA KIJAMII VUGA

P.O.BOX 112 SONI-LUSHOTO-TANGA. E-mail vugalushoto@yohoo.com

htt://envaya.org/CHAMAKIVU

UTANGULIZI

CHAMA CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA KIJAMII VUGA ,

Ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi Tanzania nzima ambapo makao makuu ya shirika yapo Kjiji cha Bazo Kata ya Vuga Jimbo la Bumbuli Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga.

Malengo ya CHAMAKIVU ni:-

      Kuelimisha jamii juu ya maswala ya kilimo na ufugaji

      Kuelimisha jamii juu maswala utawala bora na haki za raia

      Kuelimisha jamii juu ya VVU/UKIMWI

 

CHAMA CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA KIJAMII VUGA(CHAMAKIVU) lilianzishwa rasmi mwaka 2006 na kupata usajiri wake tarehe 18/12/2008 namba ya usajiri NGO/00002774, lina wanachama 15 wa kujitolea wakiwa na lengo la kufikisha taarifa sahihi katika ngazi ya Kaya. CHAMAKIVU imetekeleza   mradi wa kujengewa uwezo wa shirika mradi ambao ulisaidia CHAMAKIVU kuweza kufahamu namna ya uandishi wa miradi,utunzani wa taarifa za fedha na uandaaji wa mpango mkakati na masuala ya mazingira                                                   Mradi ambao pia uliwaalika vikundi vingine vitano navyo ni kikundi cha mazingira,kikundi cha Jitegemee,kikundi cha Mwela theatre group na kikundi cha Mapambano na kikundi cha Muungano   nao wapate fursa ya kushiriki mafunzo hayo sababu CHAMAKIVU waliweza kuwatafuta wataalamu kutoka ndani ya asasi yetu ,kutoka Wilayani Lushoto na wengine toka Dar es Salaam

SHUGHULI ZA SASA ZA SHIRIKA.

1)    kuelimisha jamii juu ya kusimamia akiba ya chakula na biashara

2)    kuhamasisha jamii juu ya matumizi ya zana bora za kilimo

3)    Kuhamasisha uanzishwaji na uendelezaji wa vikundi vya kijamii

4)    Kuyasaidia makundi yaliopo katika mazingira magumu.

5)    Kuelimisha jamii juu udhalishaji wa mazao na bustani

6)    Kuelimisha jamii juu ya matumizi ya mbolea

7)    Kuelimisha jamii juu ya kilimo cha umwagiliaji

8)    Kuelimisha jamii juu ya kudhalisha mazo kwa nishati mbadala

 

Shirika linatekeleza shughuli zote zilizotajwa hapo juu kwa kujitolea na huku likijitahidi kuhamasisha makundi mengine kushirikiana nayo katika utekelezaji wake.

 

HISTORIA YA MRADI HUU.

Mradi huu unajulikana kama mradi wa uimalishwaji wa Asasi mradi uliowafikia wanachama 10 wa CHAMA CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA KIJAMII VUGA watu 15 toka katika vikundi vya kijamii hususani vikundi vya kilimo .Mradi huu ulilenga kuongeza ufahamu juu uandaaji wa miradi shirikishi,uandaaji wa mpango mkakati,maswala ya kilimo kwanza utunzaji wa kumbukumbu za fedha za wafadhili na zile zitokanazo na michango ya wanachama na wadau wengine.

Mahitaji ya mradi huu yametokana na kutokuwepo kwa wanachama wa CHAMKIVU na vikundi vidogo viidogo vya kijamii wenye ujuzi juu ya uandaaji wa miradi,maswala ya kilimo kwanza, utunzaji wa mahesabu na uandaaji wa mpango Mkakati,Hakukuwa na mwanachama au mwanakikundi yeyote aliyekwisha wahi kushiriki au kushirikishwa katika mafunzo ya namna yeyote kati ya mafunzo yaliyotajwa hapo juu,tangu Shirika lilivyoanzishwa mwaka 2006 Tumekuwa tukipoteza fursa nyingi zilizopo kwa sababu ya ukosefu wa ujuzi huo.Hatukuwa tunaweza kuandaa miradi ,hatukuwa na mfumo/muundo  unaoweza kuchochea/kuleta matokeo chanya,hatukuwa na utaratibu mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu za mahesabu ambazo zimekuwa kama hitaji mojawapo muhimu kwa wahisani/wafadhili pindi watoapo vigezo vya upatikanaji wa ruzuku.hatukuwa tunafahamu mambo mbalimbali ya kilimo Kwa minaajiri hiyo wanachama tuliona ni vema kuomaba ufadhili toka Foundation For Civil Society shirika ambalo linatoa ruzuku kwaajili ya kujengea uwezo asasi za kiraia.Baada ya miezi kadhaa maombi yetu yalikubaliwa na utekelezaji ulianza mara moja. Shirika liliazimia na lilitimiza ushirikishaji wa wadau wote muhimu katika kuandaa malengo ya pamoja ili utekelezaji ,ufuatiliaji na tathimini vifanywe kwa pamoja.

 MALENGO YA MAFUNZO

uwaongezea ufahamu wanachama 10 wa Chama Cha Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Vuga (CHAMAKIVU) na viongozi 15 wa vikindi vya wakulima juu ya maswala ya uandaaji wa miradi,usimamizi wa fedha na maswala kilimo kwanza

 

Kuwaongezea ufahamu wanachama 10 wa Chama Cha Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Vuga (CHAMAKIVU) juu ya uandaaji wa mpango makakati

 

SHUGHULI ZILIZOFANYWA KATIKA MRADI HUU

1)     Kutoa mafunzo ya uandaaji ,wa miradi kwa wanachama 10 wa CHAMAKIVU na wawakilishi wa vikundi vya kilimo watu 15. Kati ya mambo waliyojifunza ni pamoja na ,

  • Uchunguzi wa hali halisi katika jamii
  • Ubunifu wa mradi
  • Uandaaji wa rasilimali
  • Utekelezaji wa mradi
  • Uhakiki wa mradi
  • Tahimini ya mradi
  • Uandaaji tena wa mradi

1)    Mafunzo juu ya usimamizi wa fedha kwa wanachama 10 wa CHAMA CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA KIJAMII VUGA na wawakilishi wa vikundi vya kilimo watu 15

Shughuli hii imeandaliwa kwa lengo la kujua/kufahamu juu ya kufanya malipo ndani na nje ya shirika ,kujaza Analyisis book na cash book na namna ya kufaili hati za malipo.Mambo tuliyojifunza nipamoja na

  • Maana ya usimamizi wa fedha
  • Mambo muhimu ya kuzingatia katika usimamizi wa fedha
  • Umuhimu wa kuwa na usimamizi wa fedha
  • Uandaaji wa vitabu vya mahesabu na hati za malipo
  • Uandaaji wa taarifa za fedha.

1)    Mafuzo juu ya uandaaji wa mapango mkakati kwa wanakikundi 10 wa CHAMAKIVU

Shirika liliandaa shughuli hii kwa lengo la kutoa maelekezo juu ya maana ya mpango makakati na namna ya kuandaaa mpango mkakati na umuhimu wake.

Mambo tuliyojifunza nipamoja na

  • Maana ya mpango makakati
  • Umara,udhafu, fursa na vikwazo katika shirika(SWOT ANALYSIS)
  • Utambulisho wa shirika
  • Utume wa shirika
  • Ngazi za changamano
  • Amali na utamaduni wa shirika
  • Wadau
  • Aina za wadau
  • Umuhimu wa wadau

1)    Mafuzo juu ya maswala ya kilimo kwa wanakikundi 10 wa CHAMAKIVU na wanakikundi 15 toka katika vikundi vya wakulima

Shirika liliandaa shughuli hii kwa lengo la kujua maana na ubora wa kilimo kwanza na umuhimu wake.

  • Mambo tuliyojifunza nipamoja na
  • Jinsi ya kutunza vyanzo vya maji
  • Miti na uoto unaotakiwa katika vyanzo vya maji
  • Matumizi mazuri ya ardhi
  • Jinsi ya kutumia wanyama kazi
  • Umuhimu wa kutumia matrekta na mapawatira
  • Kuimarisha ifadhi ya mazingira katika kilimo
  • Mahusiano ya afya bora kwa mkulima na kilimo bora
  • Umuhimu wa mazao ya chakula na biashara
  • Ubora wa kilimo cha umwagiliaji
  • Mahusiano ya kilimo bora na miundombinu
  • Jinsi ya kudhalisha mazao kwa nishati mbadala
  • Jinsi ya kujikinga na wadudu wanaoalibu mimea

 

MHUTASARI

Mradi huu umewawezesha washiriki katika utoaji wa maoni ya marekebisho ya Katiba na hivyo kuzima vilio, huzuni na malalamiko yasiyoisha ambayo yangetufanya tusipate Katiba isiyo na uwakilishi sawia wa wananchi.                                                                                          Malalamiko ambayo yalilamikiwa wakati wa kuchukua maoni ya mala ya kwanza na hata uundwaji wa mabaraza ya Katiba ya vijiji kwa kusema kuwa washindi walioshinda hawakushinda kihalali na hivyo wasingeweza kutoa maoni yao lakini kwa kupitia mradi na wataalamu tuliowatumia walikuwa wanaudhoefu wa kutosha juu ya masuala ya kuendesha mikutano ya aina hii,shughuli za mradi tulifanya na Mikutano kwa siku 3 kwa vikundi vya kijamii na wadau kutoka katika jamii

Pia tulifanya usambazaji wa rasimu ya Katiba kwa wadau hao na waliweze kuchangia na kutoa maoni kwa uhuru na haki.

HISTORIA YA MRADI HUU

Kulikuwa na malalamiko mengi ya wananchi katika Kata yetu ya Vuga kutokana kukosa taarifa ya ujio wa tume ya kuchukua maoni ya marekebisho ya Katiba na hivyo watu wengi kukosa fursa ya kushiriki katika kutoa maoni yao na wasijue wanaweza wakatumia njia gani kuwakilisha maoni kutokana na eneo la mradi kuwa Kijijini sana

Pia katika eneo la mradi kumekuwa na matatizo ambayo yalijitokeza kipindi cha kuchagua mabaraza ya Katiba na.

Wagombea wengi wamechaguliwa kwa misingi ya uanachama wa vyama vyao waliomadarakani . Suala hilo lilijitokeza maeneo mengi ya mradi ukivihusisha vyama hivyo. Vyama hivi kila kimoja kilihamasisha wanachama wake kuchagua wagombea kutoka katika chama chake dhidi ya wagombea wa chama kingine. Kutokana na utafiti huo asasi yetu iligundua kuwa   wafuasi wa vyama vya siasa walipita nyumba hadi nyumba kuomba kura kwaajili ya wagombea wao. Katika maeneo mengine viongozi wa kada mbalimbali za kisiasa katika vyama waliendesha kampeni za wazi kuhimiza kuchaguliwa kwa wagombea kutoka vyama vyao kinyume kabisa na nia nzuri ya Tume kuwa mchakato huu usitawaliwe na itikadi za vyama.

Baadhi ya viongozi wa serikali walipigania zaidi watu wao waingie na kuwaachafua wale wenye sifa na hata kauli za baadhi ya viongozi hao walisikika wakisema kuwa wao waatahakisha watu wao wanapita sababu wao ndio serikali na hivyo kuzua manung”uniko mengi katika jamii kwa kupitia mradi huu tunaimani kuwa wananchi watakuwa na imani na kuitumia vizuri fursa yao ya kiKatiba kwa kutoa maoni yao kwa amani na utulivu na kutumia haki yao kiKatiba

LENGO LA MRADI

Kuviwezesha vikundi vya kijamii na makundi maalumu katika jamii kushiriki katika kutoa maoni ya marekebisho ya Katiba

MATOKEO YA AWALI                                                                                                           Vikundi vya kijamii na wanajamii wameelewa na wameshiriki katika kutoa maoni ya marekebisho ya Katiba

2.Uelewa umeongezeka kwa wanajamii 158 toka katika makundi maalumu ya Kijamii toka Vijiji vya Bazo na Vuga Kishewa wametoa maoni ya marekebisho ya Katiba.

MATOKEO YA KATI

Vikundi vya Kijamii na makundi maalumu katika jamii wanatoa maoni ya marekebisho ya Katiba mpya

UTANGULIZI

  1. MRATIBU ALIANZA KWA KUWAKARIBISHA WASHIRIKI WA BARAZA
  2. UTAMBULISHO NA KUELEZA MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA NA KUFUATWA.
  • ALIELEZA MUDA NA SIKU ZA BARAZA
  • KUFUATA SHERIA NA KANUNI ZA MKUTANO WA BARAZA
  1. ALIMTAMBULISHA MUWEZESHAJI NA BAADHI YA VIONGOZI WA SHIRIKA NA PIA ALITAMBULISHA MAKUNDI YALIOSHIRIKI

MAKUNDI HAYO NI

  • WANAOISHI NA VVU/UKIMWI
  • WANAWAKE
  • WAJANE
  • VIJANA
  • WALEMAVU
  • WANAFUNZI
  • WAZEE
  • VIKUNDI VYA KIJAMII
  • WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

MRATIBU ALIFANYA HESABU JUU KUJUA IDADI YA WASHIRIKI NA KUPATA JUMLA YA IDADI YA WASHIRIKI MIA MOJA NA MBILI(102) ME-50 &KE-52)                                                                                

MRATIBU ALIMKARIBISHA MWEZEJI ILI KUENDELEA UTOAJI WA MADA.

v  MWEZESHAJI ALIANZA KWA KUSALIMIA WASHIRIKI NA KUENDELEA KAMA IFUATAVYO:

 

MUWEZESHAJI

MALENGO YA BARAZA

Kuviwezesha vikundi vya kijamii na wanajiamii kuweza kutoa maoni ya mabadiliko ya rasimu Katiba mpya

Baada ya mwezeshaji kutoa maelezo ya malengo ya rasimu ya Katiba mpya alianza kuelezea na kuwataka washiriki kufungua ukurasa no 31 sura ya sita ambayo inaelezea muundo wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, na mwezeshaji kuwataka washiriki kuunda vikundi ambavyo vitajadili katika eneo hilo la muungaNo na jumla ya vikundi 8 ambayo kila Kikundi kilikuwa na jumla ya washiriki 13

Maswali muhimu yaliyojadiliwa ya(Sura ya sita Ibara ya 60)

  1. Aina ya muungano(Serikali ngapi)

v  Serikari ya Jamhuri ya muungaNo wa Tanzania

v  Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar

v  Serikali ya Tanzania Bara.

 

  1. Mambo mangapi na yapi yawe ya muungano
  • Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania
  • Ulinzi na usalama wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
  • Uraia na uhamiaji
  • Mambo ya nje
  • Usajiri wa vyama vya siasa
  • Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na mambo ya Muungano

 

MAPENDEKEZO:(VIKUNDI)

 

MWEZESHAJI:

Kuuliza wanavikundi kama wamekubaliana na masawali husika ambayo yalikuwa yanajadiwa. Kisha kukaribisha mapendekezo

Kikundi No.1

v  Muungano wa serikali moja. Sababu:                                                                                      -kukiwa na serikali zaidi ya moja kutakuwa na gharama kubwa ya uendeshaji gharama ambazo watakao bebeshwa ni wananchi na kusababisha kuongezeka kwa umaskini kwa wananchi na kusababisha didimio la uchumi wa nchi

           -kuwaenzi Waasisi wawili wa muungaNo Nyerere na karume.ambao wao kwanamna  

               moja waliweza kusaidia kutunganisha pamoja ili kuwa taifa lenye nguvu na tija

 

2. Nyongeza katika swali la pili

-uwiaNo wa ugawaji wa lasilimali za taifa.

mfano utakuta zanziba ni sehemu ndogo sana tofauti na Tanzania bara lakini panapotokea mgawanyo wa rasilimali hazigawanywi sawa kutokana na hilo Tanzania bara hupata kidogo na wakati huo zanzibar hupata kikubwa hali ya kuwa wao ni sehemu ndogo.

Kikundi No 2

v  Kuwe na Serikali moja

Sababu: Umaskini, hii ni kutokana na nchi yetu kuwa maskini na kushindwa kukidhi mahitaji ya wananchi.

Kundi hili liliona kuwa na serikali moja kutasaidia maendeleo ya haraka kutokana na muunganiko wa mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuleta maendeleo

                             

Mapendekezo

Kifungu cha sita kisiwepo kwasababu kitaleta migogoro katika serikali hiyo kwani vyama vingine vinataka ushindani na uadui

Kundi hili liliweza kujadili kwa kina na kutaka kuwa vyama vya siasa visiwepo katika masuala muungano kutokana na vyama hivyo vinaweza kuleta udini,ukabila na kusababisha uadui na migogoro katika jamii

Na wakashauri kuwa kuwepo na wasajiri wawili Tanzania bara na Zanzibar msajiri wa Zanzibar atakuwa anashughulikia vyama vya Zanzibar msajiri wa Tanzania bara atakuwa anashughulikia vyama vya bara,

            Kikundi No.3

v  Kuwe na serikali moja

Sababu kupunguza ubaguzi kundi hili liliweza kutoa ufafanuzi wa ubaguzi na kueleza kuwa iwapo kutakuwa na serikali tatu kila serikali kutakuwa na sheria na kanuni zake ambazo zinaweza kuwa kikwazo kwa raia wa upande mmoja anapokuwa upande mwingine wa serikali nyingine.

  • Mambo yote yatafanywa na watu wote (Tanzania bara na Zanzibar)

WanaKikundi walitoa ufafanuzi kuwa umuhimu wa kuwepo na serikali moja kutasaidia kuwepo na uhuru wa kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine na kuweza kushrikiana na kufuata sheria na kanuni za pamoja

  • Ulinzi imara kwa sababu jeshi litakuwa moja

WanaKikundi walitoa ufafanuzi kuwa kukiwa na jeshi la pamoja kutasaidia kulinda mipaka yetu kwa pamoja na kuzuia maadui waliokuwa na nia mbaya na nchi yetu

 

2 Mapendekezo.

Kuwe na usawa katika malipo kwa wafanyakazi wa selikari. Kwasababu wengine wanalipwa mishahara midogo wengine mikubwa mfaNo waalimu wanalipwa na mishahara midogo tofauti na kazi wanayofanya na kutosikilizwa mawazo yao na kuyathamani.

Walimu waliweza kutoa maoni kwa kutaka kutugwa kwa sheria ya upandishwaji wa madaraja pindi wanaporudi kutoka vyuoni.

Kikundi Namba 4

Swali la kwanza

v  Serikali tatu

Kundi namba 4 liliweza kujadili juu ya Serikali ya Zanzibar, Serikali ya Tanganyika na serikali ya Jamhuri ya muungaNo wa Tanzania

Sababu Hii inaonyesha kuwa hata waandaji wa rasimu hii wanaijua vilivyo

-Ubaguzi, imeonekana kuwa kuna ubaguzi kati ya wana Zanzibar na Wana Tanzania bara kwasababu Zanzibar wana baraza lao la wawakilishi na hakuna muwakilishi hata mmoja kutoka Tanzania bara.

 

Mapendekezo

Wanapendekeza mambo yote saba ya muungano yapitishwe.

Kikundi Namba 5

v  Wapendekeza kuwa na serikali zote 3

Sababu:Lugha, hii ina maana kuwa kuwepo na Serikali inayoitwa Tanzania bara badala ya kuitwa Tanganyika

-          Hii itasaidia kulinda asili ya muungano

-          Usalama kwa serikali zote tatu kwa sababu kutakuwa na usawa

-          Kutakuwa na umoja na ushirikiano

 

Mapendekezo

Michezo- Michezo iimarishwe ili kuziwakilisha nchi zetu Nje.

Elimu- Mitaara yote iwe ya Jamhuri ya muungano

Mavazi- Lazima kuwe na vazi la muungano

 

 

Kikundi Namba 6.

v  Wanapendekeza serikali mbili yaani Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Serikali ya ya Zanzibar.

Sababu:Hii itasaidia mgawanyo bora wa rasilimali za Taifa

             -Ulinzi bora ndani ya jamhuri na mpakani

              

Mapendekezo

Hakuna haja ya kuomba uraia kama kutakuwa na serikali mbili au kama vitakuwepo lakini kusiwe na masharti magumu cha msingi ni kufuata sheria ya muungano

  

KIKUNDI Namba 7

v  Wapendekeza serikali moja

Hoja:Kuzuia kuporomoka kwa uchumi

 

MAPENDEKEZO. Kusiwe na vigezo vigumu kuomba uraia

                               Mambo yote saba ya muungano yapitishwe

 

KIKINDI NAMBA 8.

v  Kuwepo na serikali tatu: Yaani Serikali ya Tanzania, Serikari ya Zanzibar na Serikari ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Hoja:

 

Mapendekezo:Raia wawe huru kuomba uraia katika serikali zote tatu bila kuwa na masharti magumu

                           Kwa maana hicho kifungu cha sita cha mambo ya muungano kisiwepo.

             Mambo sita ya muungano yaliobakia yawepo.

                                       MAONI YA WANAJAMII

 

Mwanajamii 1(ME)

Anapendekeza kuwa na serikali moja

Hoja-Hii ni kutokana na umaskini wa wananchi hivyo wameona kuwa kukiwa na serikali moja kutasaidia kupunguza umaskini wa nchi zote mbili.

 

Mwanajamii 2 (ME)

v  Anapendekeza kuwa na serikali tatu:

Hoja:Jamhuri ya Mungano wa Tanzania tayari ni shirikisho la nchi mbili tofauti yaani Tanzania na Zanzibar na kuzalisha kitu kimoja yaani Tanganyika

-Tayari ni matakwa ya waliokuwa wengi. Tume ilitambua kuwa Watanzania walio wengi wanapendekeza serikari tatu.

- Kutokuwa na usawa, kuwa na serikari tatu kutasaidia utendaji mzuri wa kujamii, kiuchumi na hata kisiasa.

 

Mwanajamii 1(KE)

v  Anapendekeza kuwa na serikari tatu

Hoja: Kuepuka garama, hii itasaidia kupunguza gharama kwasababu watu wako kitu kimoja rais atakuwa mmoja tofauti ya kuwa na serikari tatu zenye raisi zaidi ya mmoja.

-Matabaka, hii itasaidia kuondoa matabaka kwasababu watu wote watakuwa wamoja.

-Vita, hii pia itasaidia kuondoa vita kwasababu hakutokuwa na matabaka.

 

Mwanajamii 4(ME)

v  Anapendekeza kuwa na serikali tatu

Hoja, hii itasaidia kupata ajira haraka hasa kwa vijana kwani tayari kutakuwa na upana wa utafutaji wa masoko

-          Kila serikali iwe na mfumo wao ili kuepuka ubaguzi (kidini)

-          Kulinda historia ya jina la Tanganyika kwani Tanzania imebakia kuwa Tanzania bara na Sio Tanganyika kwani Zanzibar imebakia kuwa Zanzibar.

MAPENDEKEZO

Muundo wa shirikisho Ibara ya 57 sura ya 6 kifungu cha kwanza

-Michezo na Utamaduni viwe katika Jamhuri ya muungaNo ili vijulikane ndani na nje ya nchi

-Elimu, Mtaala uwe mmoja si Tanzania wala Zanzibar.

 

Mwanajamii wa 5(ME)

Mapendekezo : Mambo saba ya muungaNo.

Ushuru wa bidhaa, Anapendekeza kuwa kama mtu atalipia ushuru Tanzania basi apite Zanzibar bila kulipa tena, hivyo hivyo mtu akilipia Zanzibar basi Tanzania asilipe tena.

 

 

Mwanajamii wa 6(KE)

Kuwe na serikali moja.

Hoja-Hii itasaidia Nchi zote kufanya vitu kwa uhuru bila kuingiliwa na nchi nyingine

 

MAPENDEKEZO:

-Serikari Ya Tanzania iitwe Tanganyika na sio Tanzania bara kama inavyojulikana kwa wengi.

-Kuhusu usajili wa vyama vya siasa- anapendekeza kusajiliwa isipokuwa chama ambacho kitajulikana kitaleta machafuko nchini haswa kuchochea vita.

-Kuwe na bunge la muungaNo kujadili mambo ya muungaNo

-Uraia na uhamiaji, Wanapendekeza uraia kuwa mmoja.

Sarafu ya benki kuu inatosha kuwa kielelezo tosha cha muungaNo kwani Kuna picha mbili za waasisi wa MuungaNo yaani Nyerere na Karume.

 

Mwanajamii wa (6) (ME)

v  Kuwe na serikali moja.

Udini, Kukiwa na serikali tayari kutakuwa na matabaka ya kidini ambayo Tayari yatachochea uadui kati ya serikali hizo

 

Mapendekezo: Swala uhamiaji na uraia lisiwe swala MuungaNo

 

Mwanajamii wa (7) (ME)

v  Serikali moja

Hoja: Huyu anapendekeza kuwa na serikali moja kwani hii itasaidia

            -Kuondoa matabaka

            -Watu wote kuwa sawa (Tanzania na Zanzibar)

            -Itasaidia kuondoa umasikini.

 

Mwanajamii wa (8)(ME)

v  Kuwa na serikali moja

Hoja, Uadui , Kuwa na serikali tatu kutazua migogoro miongoni mwa nchi hizo tatu kwani kila nchi itakuwa na sheria zake ambazo zimejiwekea hivyo kuwabana wengine wan chi nyingine.

 

Mapendekezo: Kusiwepo na wawekezaji katika selikari hiyo itakayokuwepo kwani watakuwa kikwazo na chanzo cha mgogoro.

 

Mwanajamii wa (9)(KE)

v  Kuwa na serikali moja

Hoja:Migogoro, kama kutakuwa na serikari tatu ina maana watu lazima watakuwa na migogoro hasa ya ya ardhi(mipaka) kwani kila mmoja atapende nchi yake iwe bora kuliko nyingine.

 

CHANGAMOTO.

Washiriki kudai posho

Washiriki kuwa wengi kuzidi bajeti ya mradi

Lugha- Washiriki walikuwa wakichanganya lugha ya (kigeni)

 

                             HITIMISHO:

v  Walio wengi wanapendekeza serikali moja.

 

 

 

 

                                               CHANGAMOTO

  • IDADI YA WASHIRIKI ILIKUWA KUBWA KULIKO BAJETI
  • WASHIRIKI KUDAI POSHO
  • FUNGU LILICHELEWESHA NA KUSHINDWA KUFANYA MAANDALIZI YA KUTOSHA
  • UMBALI WA MAENEO WANAPOTOKA WASHIRIKI

 

                                   MAPENDEKEZO

v  TUTENGEWE BAJETI YA KUTOSHA

v  WANANCHI ELIMU YA DHANA YA KUJITOLEA

v  FUNGU LITOLEWE KWA MUDA ULIOPANGWA

v  FUNGU LIWE KUBWA ILI TUWEZE KUFIKIA VIJIJI VYOTE

 

                                           SHUKRANI

The foundation for civil society kwa kutoa ufadhili Wanajamii walioshiriki katika mkutano

Tume ya mabadiliko ya Katiba kwa kutupatia kibali na rasimu za kutosha za Katiba

Mkuu wa shule ya sekondari Vuga Bazo kwa kutupati ukumbi kwa siku zote za mkutano

Wanachama na viongozi wa Chama cha Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Vuga

Vikundi vidogo vidogo vya Kijamii kwa kukubali wito wetu na kushirikiana nasi kwa muda wote

Tunawashukuru pia Waandishi wa Habari kwa kuchukua habari zetu katika mkutano wetu wa mabadiliko ya Katiba.

Tunamshukuru muwezeshaji wetu

Prisca Roti Kaniki kwa kuendesha mjadala kwa umahili wa hali ya juu

Tunamshukuru mchua dondoo wetu Naima Amiri kwa kuchukua taarifa za washiriki kwa umahiri wa hali ya juu.

                Tunamshukuru mratibu Jumaa Dhahabu kwa usimamizi mzuri katika shuhuli zote.

                Tunawashukuru viongozi na wanachama wote wa CHAMAKIVU

Tunamshukuru Mishi Mgahawa aliohudumia vizuri chakula kwa washiriki wetu.

 JUMAA IDD DHAHABU

MRATIBU & MSIMAMIZI WA MIRADI

                                                                                                                                                                                                  

                                                                                  


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles