Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

VOLUNTEER FOR YOUTH IN HEALTH AND DEVELOPMENT added a News update.

$
0
0

UFUNGUZI TAWI JIPYA

Napenda kuwapa taarifa wadau na wanaharakati wote kuwa Makao makuu ya Voyohede Mtwara yamekubari ombi la kufungua tawi jipya Dar es salaam kwa mkataba maalumu ambao utasainiwa na wanachama wa Dar ambao ofisi na eneo la mradi lipo kule Tabata kisukuru. Hivyo wabia wa asasi hii mnachaguo la wapi muende. Muongozo au mpango mkakati wa VOYOHEDE makao makuu unatambua uwepo wa tawi moja ambalo litafuata taratibu zilizopo katika mkataba, lengo lakuwa na matawi machache ni kwa kuwa uwezo wa kuwawezesha na kuwaongoza wanachama wa tawi husika ni mdogo na kwa hiyo basi shughuli hii itafanyika kwa kuzingatia uwezo na maslahi ya pande zote mbili yani makao makuu na tawini. Matawi yatajitegemea kwa kila jambo maelezo na miongozo yao kabla ya kutekelezwa yatatakiwa yakubaliwe na wanachama wa tawi husika bila kuvunja mkataba wake na makao makuu. VOYOHEDE-MAKAO MAKUU MTWARA inaona ufunguzi wa tawi hili la Dar es salaam ni fursa kubwa kwao na kwa tawi hivyo inaomba ushirikiano na upendo kama ndugu wa familia moja.

Nawatakia mafanikio mema,

Wenu,

Afisa Habari na Utawala

VOYOHEDE-TANZANIA


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles