Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Majani Natural and Scientific Health Promoters (MANSHEP) added 2 News updates.

$
0
0

large.jpg

MATUFAA KWA AFYA,LISHE NA TIBA

An apple a day will keep the doctor away…An apple before bed makes the doctor beg his bread” (kula tunda moja la tufaa kila siku humfanya mtu asiwe na haja ya kuonana na daktari…kula tunda la tufaa kila siku humkosesha daktari mapato yake). Misemo hii ya Waingereza inaonyesha umuhimu wa matunda ya matufaa kwa ajili ya kudumisha afya ya binadamu, kukinga na kutibu magonjwa mbalimbali. Matufaa yana Vitamini K, nyuzinyuzi za chakula pamoja na dawa-lishe (phytochemicals) aina ya quercetin flavonoid.

Faida za kiafya

  • Matufaa ni tiba nzuri ya ugonjwa wa kuharisha.
  • Husaidia katika matibabu ya uvimbejoto wa utumbo (colitis)
  • Husaidia katika matibabu na kuzuia shinikizo la damu
  • Husaidia katika tiba na kuzuia magonjwa ya mzio (allergy) pamoja na pumu ya mapafu.
  • Hutibu tatizo la kupata choo kikavu au kutokupata choo (constipation)
  • Ni dawa nzuri sana kwa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
  • Husaidia katika matibabu na kuzuia mawe katika figo.
  • Hupunguza hatari ya kupata saratani ya mapafu, saratani ya utumbo na ugonjwa wa kisukari.
  • Huimarisha afya ya ini.
  • Husaidia figo kuondosha sumu aina ya uric acid ndani ya damu.

Matumizi na kipimo

  • Kwa ajili ya tiba kula matufaa kiasi cha kilo mbili kila siku kwa muda wa siku saba mfululizo.
  • Kunywa juisi ya matufaa bilauli moja kila baada ya saa nane kila siku.

Rejea

  • Benny P.J at al: A Review on the medicinal significance of common fruits. International J. of Biomedical Research Analysis, Sep-Oct 2010, vol.1, issue 2, pp.60-64.
  • Zhao P et al: Antitumor activities of apple extracts. Chinise Journal of Clinical Oncology 2006, 3(1):37-40.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles