Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Mzeituni Foundation has a new discussion about TUSEME KUHUSU KATIBA MPYA.

$
0
0
Mzeituni Foundation:

Mzeituni Foundation,tunatambua umhimu wa katiba mpya yenye kujibu mambo ya msingi yanayojibu kero za wananchi na kugusa maisha yao ya kila siku moja kwa moja,ili mwisho wa siku tuwe na Tanzania tunayoihitaji,Tanzania yenye Amani inayonufaika na uwepo wa rasilimali zake.

Tumefurahi pia kwa rasimu ya katiba ambayo walau imejaribu kugusa na kuyasemea mambo mhimu ambayo kwa muda mrefu watanzania wamekuwa wakiyapigia kelele.

Ni wito wet kuwa kila mmoja wetu ashiriki kwa namna ya pekee na kwa masilahi ya nchi na Taifa kwa ujumla

Wanasheria na wataalamu wa mambo ya katiba pia wachukue fursa ya kutosha kupitia rasimu hii ya kwanza na kutoa inputs zao hasa kwa wananchi wa kawaida ili waelewe ni kipi kinaendelea na wakati ufikapo wa kupiga kura ya maoni basi wawe tayali kuikubali au kuikataa kwa sababu za msingi.

Tukikosea kutumia nafasi yetu hii vizuri kupata katiba nzuri yenye manufaa kwa mtanzania itatugharimu miongo kadhaa.Kwa hiyo "Chondechonde" watanzania katiba ndiyo sheria mama za nchi,tusipuuze kuendelea kutoa maoni yetu huku tukiweka uzalendo wetu mbele badala ya itikadi za kisiasa/dini/rangi/kabila au kipato.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles