Kikundi maarufu wilayani Temeke Naukala ndima Sanaa group moja ya kikundi ambacho kipata nafasi ya kushiriki katika Tamasha la utamaduni la wilaya ya Handeni, kutokana na kundi hili lina hasiri ya wilaya ya Handeni kama jina lenyewe livyojieleza limeona ni vyema kwenda kushiriki ili kuunga mkono jitihada za wana handeni kwa kuliaandaa tamasha kubwa kihasi kwamba kila kona kwa sasa linatambua uwepo wa tamasha hilo
Matarajio
- Kukubalika na wadau mbalimabli wa sanaa ambao wamehadi kushiriki na wengine kudhamini tamasha hilo kama vile, Trans grace products, Screen masters,Mtandao wa saluti 5.com,Dullah tiles& Construction Ltd , Katomu Solar specialist, Country business directory (CBD), Michuzi media, Duka la mavazi la chichi Local Ware,Smart Mind & Arters chini ya Anesa Campany Ltd,Lukaza Brog
- Kununuliwa kwa cd zetu za nyimbo za kundi ambazo zaidi ya nyimbo nne ni za wilaya ya Handeni
Nyimbo hizo ni …………………………………..
- Kuamsha hisia za wana Handeni juu ya kukabiliana na changamoto zilizopo wilaya ya Handeni kwa kutumia sanaa
- Kutaja mafanikio na maendeleo ya wilaya ya Handeni kwa kutumia sanaa
- Nyimbo zetu zitawawezesha wana Handeni kutumia fursa zilizopo kwa ajiri ya kuleta maendeleo
- Kuonesha utamaduni wa wana Handeni kwa kutumia sanaa
Fadhili Lugendo mwenyekiti wa naukala ndima amesema amesema kuwa kunachangamoto nyingi katika wilaya yetu ya Handeni kama vile:
- Ubakaji
- Mimba kwa wanafunzi
- Maji
Kutokana na taarifa za Hakimu Mkazi Mwandamizi,Mfawidhi wa wilaya ya Handeni amesema kuwa
Kesi nyingi za tuhuma za ubakaji na mimba kwa wanafunzi zinazowafikia zinashindwa kutolewa maamuzi kutokana na mashahidi wanashindwa kuthibitisha.
Kutokana na changamoto hizo naukala ndima itato elimu ya umuhimu wa kumlinda mtoto juu ya mashambulizi na vitendo vya udhalilishaji na ubakaji kwa kuwatambulisha haki za mtoto kwa Wazazi/walezi wanawajibu wa kumlea mtoto na kumsaidia kukua. Wazazi/walezi lazima wampe mtoto malazi bora,chakula,mavazi,elimu, na ulinzi.Wazazi/walezi,wazee na jamii wanawajibu wakumsaidia mtoto kukua kimwili,kiakili, kiroho,kimaadili na kijamii,pia wanawajibu wa kumsaidia mtoto kuelewa na kudai haki zake na kujua wajibu wake.
- Haki ya kulelewa na watu wengine
Kama mtoto hana wazazi aukamafamilia haimtendei haki kiasi ambacho hali yake itaathirika kutokana na mazingira kuna ulazima wa jamii kumsaidia mtoto huyu kwa namna moja ama nyingine.
- Haki ya kupata elimu
Watoto wote wanahaki ya kupata elimu bila ya ubaguzi wowote.kwa mantiki hiyo mtoto anawajibu wa kwenda shule.huku akiwa ametimiziwa mahitaji muhimu
habari na Fikiri mvugaro mshauri wa Naukala ndima