Youth Action Development (YAD) ni shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia maendeleo ya jamii ya Tanzania na hasa limejikita katika maendeleo ya vijana. Shirika hili linafanya kazi kwa manufaa ya watanzania wote na si kwa ajili ya kunufaisha kundi la watu au mtu binafsi.
Youth Action Development ni shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia maendeleo ya vijana kwa matendo. Shirika ambalo halina ubaguzi wa Rangi, Kabila, Dini au Jinsia, lenye namba ya usajili SO. No. 14486 ya mwaka 2006 chini ya sheria No. 5 ya mwaka 1954 na kupata cheti cha ukubalifu mwaka 2007, No 1811 chini ya sheria ya NGO ya mwaka 2002 . Shirika hili linafanya kazi kwa manufaa ya watanzania wote na si kwa ajili ya kunufaisha kundi la watu au mtu binafsi. Asasi hii ilianza kufanya kazi zake rasmi mwaka 2009 katika mkoa wa Dar es salaam.
Lengo kuu la shirika hili ni kusaidiana na Serikali ili kufikia lengo la kukuza uchumi na kupunguza umaskini ambalo ni MKUKUTA II na MKUZA pia na kufikia lengo la Milleniam (MDGs).
Shirika hili liaanza kufanya shughuli zake mwaka 2004 likiitwa Kinondoni peer educators, wakati huo lilikuwa halijasajiliwa. Limesajiliwa rasmi mwaka 2006 na kupata cheti cha ukubalifu mwaka 2007. Tulianza na wanchama 11 kwa sasa tuna wanacha 47.
Malengo ya shirika la YAD ni pamoja na:-
- Kuwainua vijana kiuchumi na kuwawezesha kujitegemea kwa kukusanya nguvu ya pamoja na kuanzisha miradi ya maendeleo ya mmoja mmoja na ya kikundi.
- Kuunganisha vijana katika shughuli zote za maendeleo katika jamii ili kuwawezesha kupambana na maadui wa Taifa letu ambao ni UJINGA, MARADHI, UMASIKINI na RUSHWA.
- Kutoa Elimu ya Afya katika jamii Kuhusu UKIMWI, Madawa ya kulevya, na milipuko ya magonjwa Mashuleni, Mitaani, katika viwanja vya michezo, sehemu mbalimbali za mikusanyiko na sehemu za kazi.
- Kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kiutaalamu kwa serikali pamoja na mashirika yenye malengo ya kimaendeleo.
- Kutoa elimu ya uraia na ujasiliamali katika jamii.
|
|
|