YAFUATAYO NI MAONI YA WANANCHI WALIOSHIRIKI KATIKA KONGAMANO LA KUSANYAJI WA MAONI YA RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Asasi ya Kumbura Twiyapve Group ilipata kibali cha kuendesha mkutano ya kukusanya maoni ya Rasimu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mkutano TAREHE 5/8/2013
Zoezi la kukusanya maoni kupita Mabaraza ya Katiba ya Asasi,Taasisi na Makundi yanayofanana yalifanyika tarehe 29-30/8/2013 yafuatayo ni maoni yao;washiriki walikuwa 80 35 wanawake na 45 ni wanaume.
MAPENDEKEZO YAO
Muundo wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania washiriki walipendekeza muundo huo uwe wa serikali mbili kwa sababu serikali ya shirikisho haitakuwa na mipaka iwapo ikipitishwa kutakuwa na mgogoro mkubwa wa kimipaka na kuhatarisha amani na utulivu ulipo hapa nchini.
serikali ya Tanzania Bar inatambulika mipaka yake,serikali ya Zanzibar inatambulika kwa mipaka yake,serikali ya tatu haina mipaka yake na itakuwa ni serikali tengemezi itakayowaumiza wananchi
walipendekeza katika katiba ijayo ipige marufuku ndoa ya jinsia moja kulinda utu na utamaduni wa Mtanzania.
walipendekeza madaraka ya rais yandelee kuwa nayo ili kuweza kuleta hadhi na heshima ya nchi hasa ikizingatiwa kuwa rais si mtu bali taasisi.
walipendekeza nafasi ya uteuzi wa kisiasa hususan wanawake ziendelee kuwepo yaani uwepo viti maalum.
nafasi ya mgombea uras isitolewe kwa mgombea binafsi na badala yake iwe kwa nafasi nyingine za udiwani na ubunge.
mbunge anapokufa jimbo litangazwe ili kuruhusu wananchi waweze kupata fursa ya kuchagua kiongozi wamtakaye.
umiliki wa ardhi uwe na uwiano kwa jinsia zote wanawake na wanaume.
hukumu ya kifo iendelee kuwepo ili kuleta usalama na uwelewano katika jamii.
vipengele vyote vilivyosalia washiriki walipendekeza viendelee kuwepo kama ilivyoanishwa kwenye rasimu ya katiba
Maoni haya yametolewa bila ya kushinikizo lolote la kisiasa maoni hayo yametolewa kwa kufuata muongo na kanuni ziliandaliwa na tume ya mabadiliko ya katiba.
wananchi walikuwa huru kutoa maoni yao.
wananchi walipongeza tume ya mabadiliko ya katiba kwa kuandaa jukwaa la kukusanya maoni kwa kila mtanzania,mijini na vijijini bila ya ubaguzi wowote
Ramadhan Rashid Divujagale
Mwenyekiti wa asasi ya Kumbura Twiyapve Group
MPANGO MKAKATI WA ASASI WA MIAKA MITATU2012-2014
MAELEZO YA MWENYEKITI WA KTG
Maandalizi ya mpango mkakati na bajeti ya KUMBURA TWIYAPVE GROUP 2013 – 2015 imehusisha wadau mbalimbali kama jamii. Wadau wa maendeleo Asasi za kiraia, viongozi wa KTG wa wanachama wa KTG. Kwa heshima na taadhima napenda kuwashukuru wadau wote kwa njia moja ama nyingine kwa mchango na ushirikiano mkubwa waliotupatia katika kuandaa mpango mkakati huu. Siyo rahisi kuorodhesha wadau wote waliohusika.
Uandaaji wa mpango mkakati na bajeti kwa upande mwingine ni changamoto kutoka nje ya mpango mkakati na bajeti. Ninawasisitiza wanachama wote wa KTG na wadau kutotoka nje ya mpango mkakati na bajeti kama ilivyopangwa na gharama zake. Ninaamini tumepanga kutokana na vipaumbele vya KTG na jamii.
Kama inavyofahamika na wengi kwamba serikali pekee haiwezi kutoa huduma kwa watu wake wote hivyo ninawasisitiza wadau mbalimbalikamavile Asasa zisizo za kiserikali, Taasisi za Dini, na Jumuia za Kiraia kutoa huduma kwa watanzania kwa kushirikisha sekta binafsi na jamii tutaweza kutengeneza daraja ambalo litaziba uwazi au nafasi au mapungufu yaliyoachwa na Serikali ya matumizi sahihi ya rasilimali.
Mwisho ninawaomba wadau wote kuiwezesha jamii kupitia michango ya hali namaliili waweze kutekeleza mipango mkakati na bajeti iliyoidhinishwa na kutoa matokeo yaliyokusudiwa.
……………………………
MWENYEKITI – KTG
MAELEZO YA KATIBU WA KTG
Utekelezaji wa shughuli mbalimbali zilizopangwa zitatekelezwa vizuri katika kipindi cha mwaka
2013 – 2015. Mpango mkakati huu umeandaliwa kwa kushauriana na kushirikiana na wanachama wote wa KUMBURA TWIYAPVE GROUP-MOROGORO (KTG) na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Aidha malengo, madhumuni, mkakati na shughuli zilizomo ndani ya mpango mkakati huu zinalenga kufikia Dira (Vision) yetu ya KUMBURA TWIYAPVE GROUP-MOROGORO. Dira (vision) ya KTG. “Kuunda chama chenye uwezo na imara kitakachotoa huduma za Jamii kuanzia ngazi ya kata mpaka Taifa” Mpango mkakati huu utatumika kuongoza KTG katika mipango yake na kuomba fedha kwa kuzingatia miradi maalum kulingana na mpango mkakati huu ambapo utaiwezesha jamii kufahamu haki na wajibu wao katika kutumia, kusimamia rasilimali zilizopo na kushiriki kikamilifu katika michakato ya kujiletea maendeleo endelevu.
Hivyo madhumuni na mikakati/shughuli zilizoainishwa katika mpango zitapitiwa kila mwaka na kufanyiwa marekebisho inapobidi ili kuhakikisha tunafikia lengo/dira ya KTG.
………………………
KATIBU – KTG.
MPANGO MKAKATI WA KUMBURA TWIYAPVE GROUP 2013 – 2015
1:0- UWEPO WA KUMBURA TWIYAPVE GROUP -“ KTG”
Kumbura Twiyapve Group (KTG) ni asasi ya kiraia ambayo haitengenezi faida. Ni Asasi ambayo si ya Kidini, si ya kisiasa, si ya kikabila, haibagui rangi wala jinsia. Ni asasi ambayo inajishughulisha na mambo ya maendeleo ya jamii kwa minajili ya kukuza uwezo wa jamii kutambua na kutekeleza majukumu na wajibu wao katika jamii.
Aidha asasi ya Kumbura Twiyapve Group imesajiliwa kwa Sheri ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya mwaka 2002, chini ya kifungu cha 12 (2) cha Sheria namba 24 ya 2002 na kupewa cheti cha usajili namba 00 NGO/1984 ambacho kimetolewa tarehe 21/04/2008. kwa mujibu wa usajili huu chini ya kifungu cha Sheria cha 12(2) cha Sheria namba 24 ya 2002. Kumbura Twiyapve Group inaweza kuendesha shughuli zake mahali popote Tanzania Bara.
2:0- DIRA, MATARAJIO NA MADHUMUNI
2:1- DIRA:
Kuunda chama chenye uwezo na imara kitakachotoa huduma za jamii kuanzia ngazi ya kata hadi Taifa.
2:2- MATARAJIO:
Kuwajengea uwezo jamii kwa kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uelewa na utekelezaji wa\ sera za Taifa na kuiletea jamii maendeleo kwa kufuata sera ya MKUKUTA.
2:3- MADHUMUNI:
i) Kuinua maisha ya jamii.
ii) Kuelimisha jamii mambo mbalimbali yanayohusu haki zao na jinsi ya kushiriki kwenye miradi ya maendeleo.
iii) Kuelimisha jamii juu ya sera mbalimbali za serikali hususani utawala bora,uwazi na uwajibikaji.
iv) Kusaidia jamii inayoishi maisha hatarishi kama vile wazee,yatima,vijana,wajane,walemavu na watoto wa mitaani.
v) Kujihusisha na huduma za jamii kama vile afya na elimu.
vi) Kujihusisha na miradi mbalimbali ya kiuchumi ili kulenga hasa wanachama na jamii ya vijijini.
3:0- MCHANGANUO WA NGUVU, UDHAIFU, FURSA NA VIZINGITI.
3:1- NGUVU:
- KTG ina wanachama wenye ujuzi na taaluma mbalimbali.
- Inakubalika kwa wadau mbalimbali na wafadhili wa ndani na nje yaTanzania
- Imesajiliwa kwa mujibu wa Sheria za nchi.
3:2 UDHAIFU:
- KTG haina majengo yake binafsi ya Ofisi (inapanga)
- Inategemea ufadhili
- Wanachama kutoelewa ipasavyo haki na wajibu wao na kutekeleza ipasavyo.
- Hakuna vitendea kazi vya kutosha na vinavyo kidhi mahitaji.
3:3 FURSA:
- Uwepo wa wanajamii wa kufanyanao kazi
- Uwepo wa sera na Sheria mbalimbali zinazoruhusu KTG kufanya shughuli zake
- Mitandao na mahusiano mazuri na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini
- Uwepo wa watu wa kujitolea kufanya kazi na KTG.
- Uwepo wa Amani Utulivu nchini
3:4 VIZINGITI/VIKWAZO
- Mabadiliko ya sera za Taifa
- Kuyumba kwa uchumi (economic crisis)
- Majanga mbalimbali ikiwemo kuvunjika kwa Amani
4:0 MALENGO NA MADHUMUNI
4:1 Kupanua ofisi za Kumbura Twiyapve Group
- Ongeza vyumba vya Ofisi na kufikia idadi ya vyumba 3 (Pango la ofisi ya Mkurugenzi, Mhasibu na viongozi wengine)
- Nunua/ongeza vitendea kazi vya ofisi na samani
- Fungua matawi ya KTG katika maeneo mbalimbali nchini
4:2 Kuimarisha utawala na uendeshaji wa shughuli za KTG Ajiri watumishi wenye
taaluma kwenye vitengo vyenye mapungufu (kama vile Mhasibu n.k)
- Wape mafunzo ya kujenga uwezo wa kiutendaji watumishi wanachama pamoja na utawala.
- Fanya ziara za mafunzo katika asasi nyingine zinazofanya kazi zinazofanana na KTG.
- Fanya maboresho/marekebisho ya katiba ya KTG pamoja na muongozo wa fedha.
4:3- Kuimarisha shughuli za utafiti.
- Ajiri wataalamu wenye taaluma ya utafiti
- Wape mafunzo ya kujenga uwezo wa kufanya utafiti watumishi, utawala na wanachama.
- Anzisha uhusiano na ushirikiano wa kikazi kati ya watafiti na Asasi nyingine za utafiti wa masuala mbalimbali ya kijamii na KTG.
- Baini na buni miradi ya utafiti na washirikishe watafiti mbalimbali nje ya KTG.
4:4- Kuimarisha uwezo wa jamii wa kukabiliana na changamoto na matatizo dhidi
ya maendeleo yao yanayowazunguka.
- Toa mafunzo ya kujenga uwezo kwa jamii juu ya.
- Utawala bora
- Rushwa
- Ufuatiliaji wa maadili ya utumishi na stadi za kazi ya maisha kwa vijana
- Kufanya ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya rasilimali za umma vijijini
4:5- Kuboresha na kuimarisha uwezo wa kifedha wa Kumbura Twiyapve Group .
- Toa mafunzo ya kujenga uwezo wa uandishi wa michanganuo ya miradi na utunishaji mfuko
- Andika michanganuo ya miradi mbalimbali na kupeleka kwa wafadhili na wahisani wa ndani na nje ya nchi
- Fanya shughuli za utunishaji mfuko
- Andaa mkakati wa kuongeza misaada ya wafadhili wa ndani na nje ya Tanzania
5:0 UFUATILIAJI NA TATHMINI
Ufuatiliaji na Tathmini M&E) ndani ya Dira unaanza tangu mwanzo wa mchakato wa kupanga, kutekeleza hadi mwisho wa mpango wa shughuli iliyokusudiwa.
Lengo la kufanya Ufuatiliaji na Tathmini ni kufikia mafanikio na Ufanisi wa matokeo yaliyokusudiwa na mradi kwa kutoa mrejesho kwa utawala wa ngazi zote na wadau mbalimbali. Hii hutoa fursa kwa Kumbura Twiyapve Group kuimarisha mpango wa uendeshaji na kuchukua njia/hatua sahihi za utekelezaji. Ni mfumo unao uwezesha utawala kufahamu hali halisi ya maendeleo ya mradi na kuwaruhusu kuendelea au kufanya marekebisho ya programu na shughuli za mradi.
Shughuli ya ufuatiliaji wa programu mbalimbali na miradi katika asasi yetu ya KTG ni wa Ushirikishwaji kuanzia wakati wa kupanga hadi kwenye utekelekezaji. Taarifa za mwanzo zilikusanywa na mkutano ya mipango katika ngazi za chini tunatumia katika kuweka msingi wa lengo na viashiria katika Ufuatiliaji na Tathmini.
KIAMBATANISHO 1. MUUNDO WA UONGOZI
MWENYEKITI |
WANACHAMA WOTE
|
MHASIBU |
MRATIBU ELIMU |
MWEKA HAZINA |
KATIBU |
KIAMBATANISHO 2. JEDWALI LA MPANGO
NA. |
MALENGO |
VIASHIRIA |
|
VIASHIRIA VYA MCHAKATO (OUTPUTS) | VIASHIRIA VYA MATOKEO YA MUDA MREFU (OUTCOME) | ||
1.0 | Kupanua ofisia za Kumbura Twiyapve Group (KTG) |
|
|
2.0 | Kuimarisha Utawala na Uendeshaji wa Shughuli za KTG |
|
|
3.0 | Kuimarisha shughuli za utafiti |
|
|
4.0 | Kuimarisha uwazi wa jamii wa kukabiliana na changamoto dhidi ya maendeleoyao. |
|
|
5.0 | Kuboresha na kuimarisha uwezo wa kifedha wa Kumbura Twiyapve Group . |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
KIAMBATANISHO 3: MALENGO NA SHUGHULI ZA MPANGO
S/N. |
MALENGO |
SHUGHULI |
|
1.0 | Kupanua Ofisi za Kumbura Twiyapve Group (KTG) | 1.1 – Kuongeza idadi ya Pango la vyumba vya Ofisi |
|
|
| 1.2 – Kununua vitendea kazi (shajala, vifaa vya ofisini na samani za ofisi) |
|
|
| 1.3 – Kufungua matawi ya Kumbura Twiyapve Group (KTG) |
|
2.0 | Kuimarisha Utawala na Uendeshaji wa shughuli za KTG | 2.1 - Kupitia Katiba ya KTG na kufanya marekebisho au maboresho
|
|
|
| 2.2 – Kupitia mwongozo wa fedha wa KTG na kufanya maboresho.
|
|
|
| 2.3 – Kuajiri watumishi wenye taaluma
|
|
|
| 2.4 – Kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji utawala, wanachama na watumishi
|
|
|
| 2.5 – Kufanya ziara za mafunzo katika Asasi nyingine zinazofanya kazi zinazofanana na KTG. |
|
3.0 | Kuimarisha shughuli za utafiti | 3.1 - Kuajiri watafiti wenye taaluma
|
|
|
| 3.2 – Kuendesha mafunzo ya kujenga uwezo na kufanya utafiti kwa watumishi, utawala na wanachama |
|
|
| 3.3 – Kufanya utafiti mbalimbali wa masuala ya kijamii
|
|
|
| 3.4 – Kuanzisha mahusiano na ushirikiano na Asasi nyingine zinazofanya utafiti wa masuala mbalimbali ya kijamii
|
|
4.0 | Kuimarisha uwezo wa jamii wa kukabiliana na changamoto dhidi ya maendeleoyao. | 4.1 – Kuendesha mafunzo ya kujenga uwezo wa jamii juu ya
|
|
|
| 4.2 – Kufanya ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya rasilimali za Umma.
|
|
|
| 4.3 – Kuendesha zoezi la PETs kwa vitendo
|
|
5.0 | Kuboresha na kuimarisha uwezo wa kifedha wa Kumbura Twiyapve Group . | 5.1 – Kuendesha mafunzo ya kujenga uwezo wa uandishi wa michanganuo ya miradi kwa utawala, wanachama na watumishi |
|
|
| 5.2 – Kuandika michanganuo ya miradi mbalimbali na kuwasilisha kwa wafadhili na wahisani wa ndani na nje ya nchi
|
|
|
| 5.3 – Kuendesha shughuli mbalimbali za utunishaji mfuko.
|
|
|
|
|
|
KIAMBATANISHO 4: MPANGO KAZI
S/N |
MALENGO |
SHUGHULI | UTEKELEZAJI |
| |||
2013 | 2014 | 2015 | |||||
1.0 | Kupanua ofisi za KTG | 1.1 – Kuongeza idadi ya pango la vyumba vya ofisi
| √ | √ | √ |
| |
|
| 1.2 – Kununua vitendea kazi
| √ | √ | √ |
| |
|
| 1.3 – Kufungua matawi ya KTG
| √ | √ | √ |
| |
2.0 | Kuimarisha Utawala na Uendeshaji wa shughuli za KTG | 2.1 – Kupitia KATIBA KTG na kufanya maboresho
| √ |
|
|
| |
|
| 2.2 – Kupita mwongozo wa fedha wa KTG na kufanya maboresho
| √ |
|
|
| |
|
| 2.3 – Kuajiri watumishi wenye taaluma
| √ | √ | √ |
| |
|
| 2.4 – Kuendesha mafunzo ya kujenga uwezo wa kiutendaji | √ | √ | √ |
| |
|
| 2.5 - Kufanya ziara za mafunzo
| √ | √ | √ |
| |
3.0 | Kuimarisha shughuli za utafiti | 3.1 – Kuajiri watafiti wenye taaluma | √ |
|
|
| |
|
| 3.2 – Kuendesha mafunzo ya kujenga uwezo wa kufanya utafiti | √ | √ | √ |
| |
|
| 3.3 – Kufanya utafiti mbalimbali | √ | √ | √ |
| |
|
| 3.4 – Kanzisha mahusiano na ushirikiano na Asasi nyingine | √ | √ |
|
| |
4.0 | Kuimarisha uwezo wa jamii wa kukabiliana na changamoto dhidi ya maendeleo yao. | 4.1 - Kuendesha mafunzo ya kujenga uwezo wa jamii juu ya.
| √ | √ | √ |
| |
|
| 4.2 - Kufanya ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya rasilimalimali za umma | √ | √ | √ |
| |
|
| 4.3 - Kuendesha zoezi la PETs kwa vitendo. | √ | √ | √ |
| |
5.0 | Kuboresha na kuimarisha uwezo wa kifedha wa Kumbura Twiyapve Group . | 5.1 - Kuendesha mafunzo ya kujenga uwezo wa michanganuo ya miradi kwa utawala,watumishi na wanachama. | √ | √ |
|
| |
|
| 5.2- Kuandika michanganuo ya miradi na kuasilisha kwa wafadhili na wahisani wa ndani na nje ya nchi | √ | √ | √ |
| |
|
| 5.3 - Kuendesha shughuli mbalimbali za utunishaji mfuko. | √ | √ | √ |
| |
|
| ||||||
|
|
|
|
|
|
| |
BARAZA LA MAENDELEO YA KATA YA MLALI
WILAYA YA MVOMERO
MKOA WA MOROGORO
MACHI 30,2012
A: WASHIRIKI ÷
- MWENYEKITI WA KAMATI YA MAENDELEO KATA-DIWANI
- AFISA MTENDAJI WA KATA
- AFISA KILIMO KATA
- BIBI MAENDELEO KATA
- MRATIBU ELIMU KATA
- ELIMU KATA MWAKILISHI TARAFA
- WENYEVITI WA VIJIJI
- MAAFISA WATENDAJI VIJIJI
- WAGENI WAALIKWA MBALIMBALI
B: TAARIFA
Kikao kilifunguliwa saa 5.30 Asubuhi na mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata ambaye ni Mhe.Diwani wa kata ya Mlali,Juma Abdallah Mrangi ambapo alisisitiza kuhusiana na maendeleo ya kata ya Mlali hususan shule ya sekondari iliopo Kipera,ambapo kuna shughuli za ujenzi wa madarasa mawili pamoja na hosteli ya wanafunzi.
Alielezea umuhimu wa uwepo wa hosteli hiyo kwamba itasaidia wanafunzi wa kike kuwa salama na ulinzi wa maisha yao,aliwakumbusha wajumbe kwamba jiwe la msingi la jengo hilo la hosteli liliwekwa na Mhe Mbunge Amos Makalla(wakati huo bado hajachaguliwa kuwa mbunge mwaka 2009).
Wakati huo Amos Makalla,ambaye sasa ni Mbunge wa Jimbo la Mvomero aliahidi kusaidia mabati 100 kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo la ujenzi.
Alisisitiza kwamba zoezi la ujenzi wa hosteli hiyo uongezwe kasi ikiwa ni moja ya hatua ya kuwahamasisha wadau wa maendeleo akiwemo Amos Makalla kuweza kupata msaada wake kwa haraka bila ya kupoteza muda mwingi .
Baada ya kufungua baraza la BMK(BARAZA LA MAENDELEO YA KATA) ndipo wajumbe walipewa fursa ya kuchangia.
Wa kwanza kuchangia ni Afisa mtendaji wa kijiji cha Mlali,Mdume alianza kusoma muhtasari wa kikao kilichopita cha tarehe 16/12/2011 katika suala la uchangia wa madawati wa vijiji vyote vinane vilivyopo katika kata ya Mlali.Kwa ajili ya shule ya sekondari ya Mlali.
Katika taarifa yake iligusa madawati 1030 yaliopatikana ambayo yamechangiwa na shirika la simu ya VODA COM na mashirika mengine yaliopo katika kata ya Mlali.
Halidhalika aligusia namna ya umaliziaji wa vyumba vya madarasa mawili ambayo yaligharimu shilingi mil.5 ambazo zilitolewa na mfumo wa Jimbo.
Vile vile ilitolewa taarifa ya deni la pango la ofisi ya Afisa mtendaji wa Kata ya Mlali kiasi cha sh.laki nne(400,000/=)
Mjadala ulikuwa mkubwa na wajumbe kuhoji ni wapi pesa hizo zitapatikana,katika majadiliano hayo kikao kiliridhia kwamba kila mjumbe mmoja alitakiwa kuchangia sh.10,000/=.
Tarehe ya mwisho wa kutoa mchango huo ni 30/4/2012 ambapo zinatakiwa kuwasilishwa kwa afisa mtendaji wa kata. Wajumbe waliafiki.Hata hivyo ajenda hiyo iliendelezwa kwamba uwezo wa kulipia eneo hilo ni mdogo hivyo ilipendekezwa ofisi ya mtendaji kata ihamie katika jengo la Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mlali.mapendekelezo hayo yaliafikiwa kuwa ofisi ya mtendaji wa kata ihamie katika jengo la ofisi ya mtendaji wa Kijiji cha Mlali kupunguza gharama.
Taarifa kutoka Kila Kijiji na majadiliano
Kijiji cha Mongwe-Taarifa ya kijiji hicho imebainisha ya kuwa kuna tatizo la walimu kwamba idadi iliyopo ni wanne ambapo haitoshelezi na mahitaji halisi yaliopo katika shule hiyo ya Msingi Mongwe.
Diwani alipewa jukumu la kufuatilia katika mamlaka husika ili idadi ya walimu iongezwe katika shule hiyo kwa kuwa katika kijiji hicho wananchi wamejitahidi kujenga nyumba za walimu hivyo hakuna tatizo la nyumba za walimu wala huduma ya maji kijijini hapo.
Pia wananchi kutopatiwa chakula:Wajumbe walipendekeza kuwa kuwepo kwa chakula kwa wanafunzi ili kuboresha afya zao na maendeleo ya masomo yao yawe mazuri.
Kijiji cha Peko:katika Kijiji hicho taarifa imeonesha ya kuwa kuna tatizo la vyoo katika shule ya msingi Peko.
Matundu ya choo yaliopo ni mawili tu ! hali hiyo inatishia usalama wa afya za wanafunzi kwamba kuna uwezekano kukaibuka magonjwa ya kuhara na kutambika.
Pendekezo:Wajumbe walipendekeza wazazi na wananchi wahamasishwe kuchangia gharama za ujenzi wa vyoo vya kisasa kupitia mradi wa ujenzi wa vyoo unaendelea katika Kata ya Mlali.Wajumbe waliafiki.
Kijiji cha Manza:Taarifa ya kijiji inaonesha ya kuwa kuna baadhi ya vitendo vya ukosefu wa uadilifu miongoni mwa watendaji hasa katika mfumo wa TASAF ambapo baada ya kupatikana kwa taarifa hiyo Diwani alilazimika kwenda katika kijiji hicho na kulazimisha mhusika kurudisha haraka pesa za maendeleo ya wananchi,kwa bahati njema fedha hizo zilirejesha kiasi cha sh.80,000/= zilizodaiwa kutafunwa.wajumbe walimpongeza mhe.Diwani kwa kazi nzuri.
Pia wakazi wa Manza ambao kumbukumbu zinaonesha kuwa ni wachangiaji wakuu wa shughuli za maendeleo wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo kwa zaidi ya miaka 3,hii inatokana na kuwa na kesi mahakamani na mwananchi mmoja aliyehodhi ardhi hiyo.
Kijiji cha Homboza: Taarifa ya Kijiji cha Homboza inaonesha kuwa majengo ya shule ya msingi Homboza ni machakavu na yanahatarisha usalama wa wanafunzi wawapo shuleni.
Pendekezo:wajumbe walipendekeza na kufikia azimio kwamba kila kaya inapaswa kuchangia sh.10,000/=pia kuna tatizo la walimu katika shule ya msingi Manza ambapo ina jumla ya walimu wanne tu.
Kijiji cha Yowe:Katika taarifa ya Kijiji cha Yowe kuna uhaba wa walimu halikadhalika jengo la shule hususan vyumba vya madarasa,ofisi ya walimu havijakamilika.
Mkakati wa kuwa na zahanati:Wananchi wameshaanza kufyatua matofali 1000 kwa ajili ya mchakato wa ujenzi wa zahanati.
Kijiji cha Vitonga:kuna upungufu wa walimu,umaliziaji wa vyumba vya madarasa na ofisi ya walimu.
Aidha,kuna upotevu wa fedha kiasi cha sh.mil.1.500,000/=fedha zilizotokana na kuuzwa kwa jengo moja lililopo katika Kijiji hicho ambalo lilikuwa likimilikiwa na mamlaka ya Mkonge hapo zamani kisha kumilikiwa na Kijiji.
Kijiji cha Kipera:Katika kijiji cha Kipera kuna shule mbili ambazo ni Shule ya Msingi Lugono na Shule ya Msingi Kipera ambazo zote kwa pamoja zina mapungufu ya vyumba vya madarasa pamoja na ukosefu wa ofisi za walimu.
Mapendekezo ya utekelezaji wa sera ya Kilimo kwanza
Vocha za pembejeo zinakuja muda si muafaka na pia hazikamiliki kwa mfano mbolea ya kupandia imelewa mwezi wa tatu,wakati mbolea ya kukuzia haijaletwa.Mbegu za mahindi ni chache zinaletwa wakati wananchi wameshalima na kupanda.
Hivyo mjadala uliendelea na kupendekeza kwamba mawakala wa vocha hawana msaada kwa wakulima na kuendeleza sera ya serikali ya kilimo kwanza ambayo inasisitiza taifa liondokane na janga la njaa kwa ngazi ya familia hadi taifa.walitoa mfano mbolea ya Minjigu ina tija gani kwa mkulima.
mwisho
.................................................................................................................................
2/13/2012
KUMBURA TWIYAPVE GROUP
P.O.BOX 935,MOROGORO-TANZANIA
UTAFITI WA MMOMONYOKO WA MAADILI NA KUSHUKA KWA KILIWANGO CHA ELIMU
KATIKA SHULE YA SEKONDARI BONDWA, SHULE YA MSINGI WAMI DAKAWA NA SHULE YA MSINGI MGULASI
MKOA MOROGORO
................................................................................................
YAH: UTAFITI WA CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA KIWANGO CHA ELIMU YA SEKONDARI PAMOJA NA KUPOROMOKA KWA MAADILI, BONDWA SEKONDARI
Shule ya sekondari ya Bondwa iko katika kata ya Kasanga katika manispaa ya Morogoro,ambayo ilianzishwa mwaka 2008.
Kwa mujibu wa maelezo ya walimu shule ina walimu 17, walimu wanaume 16 na walimu wa Ke 1 hata hivyokatika idadi hiyo ya walimu walimu 6wako masomoniwaliopo shuleni walimu 11.
Shule hi ni ya mchanganyiko ya wavulana na wasichana cha kusikitisha ni kwamba kuwa na mwalimu mmoja tu kwa kike jambo ambalo halitengenezi uwiano wa walimu wa kike na wa kiume shuleni hapo.Uwiano wa walimu kijinsia una faida kubwa katika kuwaongoza wanafunzi wa kike na wa kiume.
Shule hii haina maabara kabisa.Hali hii inasikitisha kwani kwanza mitihani ya masomo ya sayansi inakuwepo shuleni hapo je wanafunzi watafaulu vipi wakati wanatakiwa wafanye masomo hayo kwa vitendo? Lakini pia tutapataje wataalamu wa masomo ya sayansi wakati hakuna maabara katika shule hii na nyingine nyingi za serikali za kata?
Shule hii hakuna walimu wa masomo ya fizikia,kemia,baolojia na somo la Kiingereza kuna mwalimu mmoja tu.ambaye anafundisha toka kidatu cha kwanza hadi cha nne.
Shule hii haina nyumba hata moja ya kuishi walumu,inabidi wapange nyumba mitaani.Shule hii ina mapungufu ya vyumba sita vya madarasa lakini pia shule haina vyoo vya walimu.
Majengo ya shule hii yamejengwa chini ya kiwango kwani simenti imeanza kubanduka na kufanya mashimo madarasani.
Shule haina jingo la ofisi ya walumu,jambo linalofanya walimu hao kutumia chumba kimoja cha darasa kuwa ofisi ya walimu.
Shule hii haina bomba la maji,hali hii ni ngumu sana kwani wakati mwingine inawalazimu wanafunzi kutumia makaratasi mara wanapokwenda chooni,maji ya kunywa walimu wananunua ndoo sh.200/= kwa kutumia pesa za mfuko wa shule.
Shule hii ina upungufu mkubwa wa vifaa vya kufundishia kwa walimu na vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi.Hali hii inarudisha nyuma maendeleo na ufahamu wa wanafunzi kwani inafikia kitabu kimoja wanatumia wanafunzi kumi.
Uwiano wa walimu na wanafunzi ;mwalimu mmoja anafundisha wanafunzi 80,hali hii bado ni mzingo mkubwa kwa walimu.
Stahiki za walumu,mishahara ya walimu inachelewa sana mara nyingine inafika tarehe 5 ya mwezi unaofuata ,fedha za likizo ni ngumu sana kuzipata unaweza kfuatilia zaidi ya miezi sita na pia isifanikiwe.Posho nyingine hawalipwi kabisa wanapouliza hawapewi jibu la kueleweka.
Walimu wa shule wana majukumu mingine Ambayo ni kugharamia shughuli za shule kama nauli kwa ajili ya kufuatilia vifaa vya shule kwenye ofisi ya elimu,hata wakati mwingine kununua chki kwa fesa zao nk.
Shule inapangiwa wanafunzi wengi mno kulingana na walimu waliopo shule za sekondari za kata.limetolewa ombi kwamba wanafunzi wengine wanapaswa kupelekwe vyuo vya ufundi.
Utoro wa wanafunzi shuleni hapo ni mkubwa kutokana na mazingira ya shule kutokuwa na uzio.
Wapo wanafunzi wa kike wachache wa kidato cha tatu waliopata mimba ila wamejifukuza wenyewe .Uongozi wa shule umejitahidi kuwafuatilia lakini hasi sasa wahajapatikana.
Shule hii ina bidi ya shule lakini bado haijaanza kufanya kazi na walimu hawajui ni kwa nini.
Sera ya elimu ya sekondari ipo lakini haitekelezwi vyema na seriklai kwani kuna mapungufu makubwa katika utekelezaji wa sera ya elimu ya sekondari likiwemo la maabara na mengine mengi.
TAARIFA YA SHULE YA MSINGI WAMI DAKAWA WILAYA YA MVOMERO
Katika shule ya msingi Wami Dakawa mahojiano yalifanyika kati ya mwalimu mkuu na wajumbe wa Kumbura Twiyapve Group kuhusu mmomonyoko wa maadili mashuleni na ukosefu wa maadili.
Mwalimu alitaka kujua iwapo serikali itatekeleza kwa vitendo na kuondoa matatizo haya ya walimu baada ya kupokea hoja na kero hizi za walimu.
Wajumbe walifafanua kuwa baada ya kazi ya kupata maoni ya walimu ripoti itapelekwa kwa katibu mkuu ofisi ya Makamu wa Rais tayari kwa utatuzi wake.
Mwalimu mkuu alifungua kikao ambapo alitoa fursa kwa mwenyekiti wa Kumbura kuelezea dhamira ya kufanya utafiti katika eneo la mmomonyoko wa maadili kwa watumishi wa Umma.
Alitoa mfano wa matatizo ya walimu ni moja ya sababu ya kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili.
Mfumo uliotumika ni swali na jibu kama ifuatavyo;
Shule inawalimu wangapi/
JIBU:Shule ina walimu 39.
SWALI:shule ina matatizo gani?
JIBU:shule ina matatizo ya vyumba vya madarasa havitoshi,vifaa vya ofisi kama viti vichache.Hivi karibuni migomo kumeibuka migomo isiyoisha pamoja na maandamano.
Matatizo ya walimu hayapatiwi ufumbuzi kwa wakati jambo ambalo linasababisha jazba kwa walimu na hatimaye migomo.
Mwalimu anahamishwa kituo cha kazi bila kupewa posho jambo linalosababisha mwalumu aiingie kazini hadi atakapopata posho,kwa hiyo viongozi wa ngazi za juu wabadilike ili matatizo haya yaishe.
Waliopo chuoni ni 6;waliopo kazini 37,Ke 28 na Me 9
Mmonyoko wa maadili tatizo ni nini?
Katika mjadala huo imebainika kwamba wajumbe wamejaribu kulinganisha hali ya siku za nyuma na jinsi ilivyo sasa wamesema zamani kila kitu kilikuwa kinapatikana shuleni lakini siku hizi hakuna huduma kama ilivyokuwa ikitolewa zamani kama vile madaftari,kalamu,vitabu,chakula nk.
Jambo hilo limeelekezwa kwa viongozi wa ngazi za juu kwa kusitisha utoaji huduma hiyo mashuleni jambo ambalo linachangia kwa asilimia kubwa wanafunzi kukosa elimu bora.
Mrundikano wa wanafunzi darasani ni mkubwa mwalimu anashindwa kuwasaidia wanafunzi pia ushirikiano wa wazazi na walimu ni mdogo hasa kutoa michango.
Mwalimu Haule:tatizo linaloniudhi ni wingi wa watoto darasani muda wa kutoka shuleni saa 11 jioni upunguzwe.
Mshahara wa mwalimu ni mdogo,mitaala inabadilishwa kila wakati ni tatizo,kufutwa kwa mitihani ya daraa la nne ni tatizo kwa wanafunzi.
Mwalimu Mkuu msaidizi:Posho za walimu ziwepo.ucheleweshwaji wa mishahara ya walimu inaonekana viongozi wa juu wanafanya vitabu kama miradi kwa sababu waandishi wa vitabu ni wengi na mada ni zile zile.
OTORO MASHULENI
Wameweza kupiga vita utoro na kufanikiwa kwa kiasi Fulani kwa sababu katika eneo hili linachangia kushuka kwa kiwango cha elimu hasa katika maeneo ya vijijini.
MIMBA
Tatizo la mimba halipo katika shule ya msingi Dakawa.
MAADILI
Wazazi “kuwacheza” watoto wao kunachangia kushusha maadili.
Marko Kasongo:Walimu wanashindwa kwenda kusoma kuongeza elimu kutokana na muda wa kukaa shuleni,kutopandishwa kwa madaraja kwa wakati.Pia hata wakati mwingine baadhi ya walimu wanapopandishwa daraja hawaongezewi mishahara.
Pia Afisa Elimu wa wilaya kuongeza muda wa saa za kazi kutoka sa 9:30 hadi saa 10:30 bila ya kutoa maelezo ya nyongeza za mishahara wa muda wa ziada.
Walimu kukosa kwenda semina kutokana na mitaala kubadilika.
Mwalimu Mkuu:idadi ya wanafunzi ni kubwa inasababisha walimu kukosa maadili na kutoa rushwa,kuvujisha mitihani ili watoto waweze kufaulu ili mwalimu aepukane na vitisho vya Afisa elimu.
Mitaala inapobadilishwa walimu wawezeshwe ili waende na wakati wa mitaala ya wakati huu.
Elias walimu wanadai lakini hawalipwi na kuna maelezo ya kutosha sababu ya kufanya hivyo.
SHULE YA MSINGI MGULASI
Shule ina walimu 33 Me 21 na Ke 12
Upungufu mkubwa wa walimu ni wa sayansi wapo 2, upungufu ni 8.katika shule hiyo imebainika ya kuwa haina maabara.
Vitendea kazi havitoshi pia uwiano mwalimu 1:60-70.
Vyumba vya madarasa 24 havitoshi upungufu 5.
Hakuna nyumba za walimu.Kuna jingo moja ambalo halijaisha.
Matundu ya vyoo Ke.8 Me 8.
Vyoo vya walimu vipo 1-1
Huduma ya Maji
Katika shule hii ina maji ya bomba.
Nakala ya sera ya Elimu ya sekondari.
Hali ya mahudhurio utoro uko kiwango cha juu sana.
Katika shule hiyo inakabiliana na changamoto ya utoro kushirikiana na wazazi kwa kutoa adhabu ndogondogo.
Mishahara inacheleweshwa malipo ya arrears,malipo ya likizo.
Kwa shughuli za ufuatiliaji wa mambo ya shule walimu huwa wanajitegemea.
Walimuwapya huwa hawalipwi stahiki zao mapema na ipasavyo upendishwaji wa madaraja kwa walimu kwa sasa haupo.Inawakatisha tama walimu kabadilisha fani.
Wanafunzi kupata mimba watano.wamerudishwa nyumbani na huwa hawarudi.
Baraza la wanafunzi lipo.
Mwalimu Ngatoluwa ambaye alikuwa mstaafu aliitwa kazini lakini amefanya kazi mwaka mmoja bila kulipwa mshahara.
Taasisi ya kumbura baada ya kufanya utafiti huo mdogo imekuja na changamoto katika maeneo yafuatao;
Swali:Tufanyeje?, Nani afanye?, Lini tufanye?