WAGENI TOKA DAILY BREAD LIFE MINISTRIES KUTOKA IRINGA TAREHE 18/11/2019
Tarehe 18/11/2019 shirika letu lilitembelewa na ugeni kutoka Daily bread Life ministries kutoka Iringa. Kiongozi wa msafara alikuwa Askofu Mpeli Mwaisumbi wa kanisa la ACT FELLOSHIP ambaye ndiye mkurugenzi na mhasisi wa Ministri hii ya Daily Bread Life Ministries. Ugeni huu ulifika kwa lengo la kuweza kuona maendeleo ya shirika letu la FUTURE FOR TODAY PRIORITIES IN TANZANIA (FUTOPTA) kwa mwaka 2019. Waliweza pia kuongea na watoto wa shirika letu waishio katika mazingira magumu ilikujua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
Ugeni kutoa DAILY BREAD LIFE MINISTRIES ulipowasiri katika ofisi za shirika letu la FUTOPTA tarehe 18/11/2010
|
Aidha walifanya ibada ya pamoja na wanakijiji ambao walifika kwa kiasi kikubwa kuwasikiliaza na kujifunza mbambo mbalimbali. Hakika ilikuwa siku yenye furaha kubwa sana kwa wanakijiji wa Inolo na vijiji jirani. Pia walishiriki chakula cha pamoja pamoja na watoto na wanakijiji wote wa eneo ilo.
Wakati wa ibada ndani ya ukumbi wa FUTOPTA iliyoendeshwa na Askofu Mpeli wa kanisa la ACT FELLOSHIP TANZANIA. 1) Pia shirika limefanikiwa kuwatia moyo watoto yatima na wale waishio kwenye mazingira hatarishi kwa mikakati mbalimbali. Aidha kuna watoto ambao wamekuwa wakisaidiwa na shirika kwa muda mrefu toka wakiwa shule ya msingi na mwaka 2019 walifahuru kujiunga na sekondari HOLONGO ambao ni jumla ya 4 na sekondari ya IWINDI ni mwanafunzi mmoja. Shirika likaamua kuwapatia zawadi kwa kufahuru kutoka darasa la saba kwenda sekondari. Watoto hao ni wanne wavurana na wawili wasichana |
Miongoni mwa watoto wanaohudumiwa na shirika letu wakiwa wemeshika zawadi zao baada ya kufanya vyema katika masomo yao kutoka shule wanazosoma ili kuwaamasisha kusoma
|