KIKAO NA ANNIE MARIE KATIKA HOTEL YA HOLIDAY IN JIJINI DAR-ES-SALAAM.
Safari ya Annie Marie kuja Tanzania yamkutanisha na Rafiki yake Prosper Maokola na Uongozi wa TEYODEN.Annie Marie ni mwanaharakati wa masuala ya vijana kutoka Canada akijishughulisha zaidi na masuala ya kambi za vijana sehemu mbalimbali za africa na marekani.
Safari ya kuja Tanzania ilikuwa na kusudio la kufanya kambi katika kituo cha vijana cha UVIKIUTA kilichopo chamazi nje kidogo,upande wa kusini wa wilaya ya Temeke.
Katika safari hii katibu mtendaji wa TEYODEN akiwa na kijana Prosper walipata nafasi ya kukutana na mwanaharakati huyu na kufanya nae mazungumzo ya namna ya kusaidia vijana katika wilaya ya Temeke.Annie alitoa ahadi kuwa atawasaidia vijana kwa kuwapatia nafsi mbalimbali hasa za kambi za vijana ili waweze kubadilishana utamaduni na uzoefu na vijana wengine kote ulimwenguni.Annie Marie kulia akiwa na mwanaharakati mwenzake kutoka Canada na Viongozi wa TEYODEN katika hoteli ya Holiday inn katika wakipata chakula cha mchana na kufanya mazungumzo kuhusu maendeleo ya vijana.