shirika limeanzishwa mwaka 2008 na kupata sajiliwa mwaka 2009 katika Ofisi za wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsi na watoto Tarehe 13/07/2009 na kupewa cheti cha Usajili chenye namba 00003269.
katika kipindi cha uhai wa shirika tumeweza kushirikiana na viongozi wa vijiji,vitongoji,kata na Wilaya katika wilaya ya mkuranga kwa kuwapatia mafunzo ya utawala Bora na haki za Binadamu.
pia shirika limewai kuomba ufadhili kwenye shirika la The Foundation For Civil Society na kuewa kiasi cha T.sh.milioni tano(5,000,000/= ili kuendesha mafunzo ya utunzaji wa mazingira katika vyanzo vya maji vya asili.
mafunzo ayo yamewanufaisha Viongozi wa kata za Mkuranga,Kiparang'anda na Mbezi pia mafunzo yamewanufaisha wananchi wapatao 50 kwa kushiriki moja kwa moja katika mafunzo ayo ambapo wao wamefundishwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa wengine kwa lengo la kusambaza zaidi elimu waliyoipata. baada ya mafunzo vijiji 13 vimeweza kutunga sheria Ndogo ndogo za utunzaji mazingira katika vyanzo vya maji vya Asili.
kwa sasa tumeomba ufadhili kwenye shirika laThe Foundation For Civil Society na tunatarajia kufanya mafunzo ya ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma katika sekta ya kilimo kwa viongozi wa kata tano za Mradi kata izo ni Kiparang;anda,Mkuranga,Pubu,Mwarusembe na Bigwa mafunzo aya yatafanyika katika kata za wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.
hata hivyo shirika linatafuta wafadhili wegine kwa ajili ya Miradi ya kuondoa ukatili kwa wanawake na watoto wa majumbani na wale wanaotumikishwa chini ya umri viwandani, mashambani,Maofisini na majumbani.