MKATABA WA KUCHIMBIWA KISIMA
Makubaliano haya yamefanywa KATI YA
Pretty Development for Poverty Reduction (PDPR), Website: www.envaya.org/pdpr
S.L.P 430, Njombe, Simu: 0754397178, 0652556833, Email: pdprngo@gmail.com…./…./2018
NA
………………………………………………………
………………………………………………………
1) Kisima kitachimbwa katika eneo la ……………………………………… ……………….
KM …………… toka Mjini, KM ………. ngapi toka barabara ya rami.
2) Maji yatatumika kwa ………………………………………………………………………
3) Unakusudia lini tukuchimbie kisima ………………………………………………………
4) Gharama za uchumbaji:
- Survey ni laki 4 kwa kila maeneo ya karibu au mkiwa wengi na kama upo mbali laki 5 ikijumlisha na usafiri, Malazi na chakula.
- Kila mita moja utalipia 45,000 pamoja na casing (PVC) kwa sehemu zisizokuwa na mwamba na elfu 70,000 kwa maeneo yenye miamba pamoja na cassing.
- Gharama ya water pump itategemeana na urefu wa kisima ila ni kati ya Milioni 1 hadi 3 kufuatana na aina ya pump na urefu wa kisima.
- Umeme 1m,
- Diseal 2m – 2.5m,
- Solar 3m hadi 6m,
5) Mteja atawajibika kufanya malipo ya awali 50% ya gharama ya uchimbaji bila pump ambapo mitambo ikiwa imefika site kwake kuanza kazi au anapokabidhiwa kuondoka nayo kwa site zilizo mbali kwa ajili ya ununuzi wa PVC, Mafuta, usafiri na tahadhari za kutatua changamoto zinazojitokeza, na malipo yaliyo baki pale wanapo malizia kuchimba tu, na anaye hitaji pump atawajibika kulipa hela yote kwa mkupuo mmoja ili ikanunuliwe na kufungiwa.“Malipo yote yatakayo fanywa hakikisha umepata receipts na usifanye kwa mafundi au mtu yeyote ambaye hujaambiwa na ofisi haita husika. Kazi yako haitaanza kabisa mpaka ulipe 50% ya gharama na kama ukishindwa ndani ya masaa 3 mitambo itaweza kuondoka kwenda eneo lingine,
6) Mteja anaweza kujinunulia vifaa ambavyo vinahitajika kwa ajili ya kisima chake kama PVC pipe, pump, bomba na vifaa vingine kama atataka vya utofauti au ubora wa hali ya juu na bei kubwa.
7) Kisima kitakamilika ndani ya siku moja hadi 7 kufuatana na eneo na miamba.
8) Kama mteja atakuwa na fedha pungufu ataweza ingia mkataba na PDPR na ardhi yenye kisima itatumika kama dhamana na hataruhusiwa kuuza au kukopea tena na akikiuka mari nyingine zinaweza shikiliwa kwa niaba ya kufidia deni, deni la ndani ya miezi 4 halina riba na baada ya miezi 4 utalipia 7% ya kiasi kwa mwezi. Na mkopaji hatakiwi awe na deni sehemu nyingine na asiwe aliwahi kufanya usumbufu sehemu nyingine, na Kisima chenye mita 120 na kuendelea ndicho chenye sifa za mkopo wa 20% na Mteja akishindwa kulipa PDPR inauwezo wa kuteua Dalali wa kusaidia kukusanya deni na kuuza dhamana.
9) Mteja anaombwa kushirikiana au kuhakikisha ulinzi wa mitambo ikiwepo kazini kwake kwa kutoa ushauri wa kiusalama.
10) Kila upande utahusika na makubaliano yaliyomo kwenye mkataba huu mpaka kila upande utakapo jitosheleza/pata haki yake.
11) Kama survey hatujafanya sisi hatutahusika na kutokupatikana kwa maji na utatakiwa kulipa 70% ya gharama zote za uchimbaji kabla uchimbaji haujaanza (Kutokana na surveyor wengine kuwa na vifaa vya kizamani, wavivu, kuwa na ujuzi mdogo na kusahau point zenye maji), na kama tutakuwa tumefanya sisi tutapima upya na kuangalia uwepo wa maji na kuchimba upya na mteja ataombwa afidie kiasi cha mafuta lita 200 au laki 6 tu.
12) Mdhamini wa Mteja 1: Jina …………………………..wa ………………………………..
NO: ya simu……………………………………. email: …………………………………
13) Mimi /sisi………………………………………tumesoma na tumekubaliana namashariti na tupo tayari kuchukuliwa hatua kama tutakiuka au kushindwa kulipa sahihi……………………. Nimelipa………. Deni ……………Risiti …………………
Cheo ……………………..Tarehe ………………………..
14) Mkataba huu umefanyika mahali……………………………..tarehe …………/…../2018
ZINGATIA:
a) Malipo ya survey hulipwa mara moja na si kwa awamu la sivyo Survey Report zao zitakuwa Pending mpaka utakapo lipa.
b) Hatuna dalali na dalali hahusiki na mwenye shamba ndio anatambulika kwetu,
c) Hundi (Cheque) hatupokei ni malipo ya pay in slip direct kwenye account na cash tu,
d) Visima vya chini ya mita 200 tunatumia mashine Ndogo za diesel zinazo bana matumizi ya mafuta na zaidi ya mita 200 tunamalizia na magari.
e) Wateja wenye tabia zinazo ashilia usumbufu, tabia mbaya au asili ya utapeli watalipa 90% ya gharama za uchimbaji ndio kazi zao zianze. (Walioshindwa kulipa gharama za survey kwa wakati, kutoa taarifa za uongo, kuwa na madeni mengi nk)
f) VIKUNDI, MAKAMPUNI na TAASISI Zimekuwa zikiongoza kwa usumbufu wa kutolipa kwa wakatia au kutolipa kabisa na kukosa mtu anaye wajibika moja kwa moja kwa hiyo Mtu mmoja tu atachukua wajibu wa kuwawakilisha wenzake na atawajibika yeye kama yeye na watatakiwa kulipa 70% ya gharama za uchimbaji kazi inapo anza tu.