Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

COMMUNITY SUPPORT INITIATIVES - TANZANIA added a News update.

$
0
0

Matokeo chanya ya mradi wa haki ardhi kwa wafugaji Asili (Pastoralist Project) uliokuwa ukitekelezwa katika wilaya ya Babati na shirika la COSITA Mwaka 2013-2014 na 2015-2016.

kwa ufadhili wa Irish Aid kupitia  CARE International,mradi ulitekelezwa katika kata 9 na vijiji 24 vya wilaya ya Babati, Mradi ulikuwa unalenga kuwajengea wafugaji asili uwezo wakufahamu haki za ardhi, madiliko ya tabia ya nchi na usawa wakijinsia.

wafugaji asili waliweza kuwa na uongozi kwa ngazi ya wilaya hadi vijiji vikundi hivyo vilikuwa vinaitwa vikundi vya umoja wa wafugaji na kupata usajili halmashauri ya wilaya. 

mradi huu uliweza kuleta mabadiliko makubwa kwa wafugaji asili kwa vipindi vyote vya utekelezaji wafugaji waliweza kufanya utetezi na ushawishi wa raslimali zinazowahusu wafugaji asili kama maeneo ya malisho, njia za mifugo kupita(mapario), majosho pamoja na kufahamu haki za ardhi.

Kutokana na vikundi vilivyoundwa wafugaji asili katika wilaya ya Babati waliweza kulinda maeneo yao ya malisho na kuweza kushinda baadhi ya kesi zilizokuwa zinahusu kubadilishwa matumizi ya maeneo ya malisho na kuwa ya kilimo.  


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles