Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

PRETTY DEVELOPMENT FOR POVERTY REDUCTION (PDPR) updated its VISIMA KUKU NYUKI MITI page.

$
0
0

 

MKATABA WA KUCHIMBIWA KISIMA

 

Makubaliano haya yamefanywa   KATI YA

 

Pretty Development for Poverty Reduction (PDPR), Website: www.envaya.org/pdpr

S.L.P 430, Njombe, Simu: 0754397178, 0652556833, Email: pdprngo@gmail.com…./…./2017

 

                                                            NA

………………………………………………………

………………………………………………………

 

1)      Kisima kitachimbwa katika eneo la ……………………………………… ……………….

KM …………… toka Mjini, KM ………. ngapi toka barabara ya rami.

2)      Maji yatatumika kwa ………………………………………………………………………

3)      Unakusudia lini tukuchimbie kisima ………………………………………………………

4)      Gharama za uchumbaji:

  • Survey ni laki 4 kwa kila maeneo ya karibu au mkiwa wengi na kama upo mbali laki 5 ikijumlisha na usafiri, Malazi na chakula.
  • Kila mita moja utalipia 50,000 pamoja na casing (PVC) kwa sehemu zisizokuwa na mwamba na elfu 60,000 kwa maeneo yenye miamba raini na 70,000 kwa miamba migumu kwa PVC ya nchi 4 kwa visima ambavyo havikidhi vigezo vya mradi wa “Water for All”. Na kwanaokidhi kila mita 35000/= kwenye udongo na miamba 50,000/=.
  • Gharama ya water pump itategemeana na urefu wa kisima ila ni kati ya Milioni 1 hadi 3 kufuatana na aina ya pump na urefu wa kisima.
    • Umeme 1m,
    • Diseal 2m – 2.5m,
    • Solar 3m hadi 6m,

5)      Mteja atawajibika kufanya malipo ya awali 50% ya gharama ya uchimbaji bila pump ambapo mitambo ikiwa imefika site kwake kuanza kazi au anapokabidhiwa kuondoka nayo kwa site zilizo mbali kwa ajili ya ununuzi wa PVC, Mafuta, usafiri na tahadhari za kutatua changamoto zinazojitokeza, na malipo yaliyo baki pale wanapo malizia kuchimba tu, na anaye hitaji pump atawajibika kulipa hela yote kwa mkupuo mmoja ili ikanunuliwe na kufungiwa.“Malipo yote yatakayo fanywa hakikisha umepata receipts na usifanye kwa mafundi au mtu yeyote ambaye hujaambiwa na ofisi haita husika. Kazi yako haitaanza kabisa mpaka ulipe 50% ya gharama na kama ukishindwa ndani ya masaa 3 mitambo itaweza kuondoka kwenda eneo lingine,

6)      Mteja anaweza kujinunulia vifaa ambavyo vinahitajika kwa ajili ya kisima chake kama PVC pipe, pump, bomba na vifaa vingine kama atataka vya utofauti au ubora wa hali ya juu na bei kubwa.

7)      Kisima kitakamilika ndani ya siku moja hadi 7 kufuatana na eneo na miamba.

8)      Kama mteja atakuwa na fedha pungufu ataweza ingia mkataba na PDPR na ardhi yenye kisima itatumika kama dhamana na hataruhusiwa kuuza au kukopea tena na akikiuka mari nyingine zinaweza shikiliwa kwa niaba ya kufidia deni, deni la ndani ya miezi 4 halina riba na baada ya miezi 4 utalipia 7% ya kiasi kwa mwezi. Na mkopaji hatakiwi awe na deni sehemu nyingine na asiwe aliwahi kufanya usumbufu sehemu nyingine, na Kisima chenye mita 120 na kuendelea ndicho chenye sifa za mkopo wa 20% na Mteja akishindwa kulipa PDPR inauwezo wa kuteua Dalali wa kusaidia kukusanya deni na kuuza dhamana.

9)      Mteja anaombwa kushirikiana au kuhakikisha ulinzi wa mitambo ikiwepo kazini kwake kwa kutoa ushauri wa kiusalama.

10)  Kila upande utahusika na makubaliano yaliyomo kwenye mkataba huu mpaka kila upande utakapo jitosheleza/pata haki yake.

11)  Kama survey hatujafanya sisi hatutahusika na kutokupatikana kwa maji na utatakiwa kulipa 70% ya gharama zote za uchimbaji kabla uchimbaji haujaanza (Kutokana na surveyor wengine kuwa na vifaa vya kizamani, wavivu, kuwa na ujuzi mdogo na kusahau point zenye maji), na kama tutakuwa tumefanya sisi tutapima upya na kuangalia uwepo wa maji na kuchimba upya na mteja ataombwa afidie kiasi cha mafuta lita 200 au laki 6 tu.

12)  Mdhamini wa Mteja 1: Jina …………………………..wa ………………………………..

NO: ya simu……………………………………. email: …………………………………

13)  Mimi /sisi………………………………………tumesoma na tumekubaliana namashariti na tupo tayari kuchukuliwa hatua kama tutakiuka au kushindwa kulipa sahihi……………………. Nimelipa………. Deni ……………Risiti …………………

Cheo ……………………..Tarehe ………………………..

14)  Mkataba huu umefanyika mahali……………………………..tarehe …………/…../2017

 

ZINGATIA:

a)      Malipo ya survey hulipwa mara moja na si kwa awamu la sivyo Survey Report zao zitakuwa Pending mpaka utakapo lipa.

b)      Hatuna dalali na dalali hahusiki na mwenye shamba ndio anatambulika kwetu,

c)      Hundi (Cheque) hatupokei ni malipo ya pay in slip direct kwenye account na cash tu,

d)     Visima vya chini ya mita 200 tunatumia mashine Ndogo za diesel zinazo bana matumizi ya mafuta na zaidi ya mita 200 tunamalizia na magari.

e)      Wateja wenye tabia zinazo ashilia usumbufu, tabia mbaya au asili ya utapeli watalipa 90% ya gharama za uchimbaji ndio kazi zao zianze.

f)       VIKUNDI, MAKAMPUNI na TAASISI Zimekuwa zikiongoza kwa usumbufu wa kutolipa kwa wakatia au kutolipa kabisa na kukosa mtu anaye wajibika moja kwa moja kwa hiyo Mtu mmoja tu atachukua wajibu wa kuwawakilisha wenzake na atawajibika yeye kama yeye na watatakiwa kulipa 70% ya gharama za uchimbaji kazi inapo anza tu.


Usiwe mnyonge wa kiuchumi kutana na wataalamu wa PDPR wenye uwezo wa kubadili maisha yako kwa muda mfupi katika uanzishwaji wa miradi na ushauri mbali mbali wa kiutalaam na wewe uwe sehemu ya mabadiliko..

Asasi ya PDPR inasaidia uanzishwaji wa miradi ya mashamba ya mbao na matunda mbali mbali kuanzia hatua ya kwanza hadi ya mwisho kwa gharama nafuu na ufanisi wa hali ya juu na utafika kutembelea shamba darasa zetu za miti ya matunda na mbao na ufugaji kuku, samaki, nyuki pia tunauza chakula cha kuku, mizinga, vifaranga, na tunachimba visima kwa bei nafuu.

HUDUMA YA MITI

  1. Utengenezaji wa kitalu cha miti (Nusuries of trees)
  2. Uhamishaji wa miche kwenye viriba (Tubes)
  3. Mafunzo ya kilimo cha miti ya mbao na matunda na vitabu.
  4. Ushauri wa uandaaji wa kitalu cha miti mbali mbali na uhudumiaji na pamoja na kitabu.
  5. Ushauri wa upandaji wa miti mbali mbali shambani na uhudumiaji.
  6. Huduma ya utunzaji wa miti na masoko.
  7. Pia kama unahitaji kununua au kuuza shamba eneo lolote unasaidiwa kulipata kwa gharama nafuu zipo hadi ekari kwa TSH: 70,000/= kwa kilimo cha miti na matunda mbali mbali.
  8. Tunauza mashamba ya miti ya mbao ya mwaka mmoja laki 4.5, miaka miwili laki 6, miaka 3 laki 9 plot zipo eneo la kifanya, lupembe na ninga.

 

 

UANZISHWAJI WA MIRADI YA UFUGAJI NYUKI.

Tunasaidia uanzishwaji wa mradi wa ufugaji nyuki na taaluma zingine zinazoendana na upatikanaji wa eneo la ufugaji na asali na nta yako yote ya ziada itanuliwa na PDPR.

HUDUMA YA

  1. Mafunzo ya ufugaji nyuki na kitabu.
  2. Mafunzo ya utengenezaji wa mizinga ya mbao, udongo, kisasa (commercial) na uuzaji
  3. Mafunzo na huduma ya ujenzi wa nyumba ya nyuki.
  4. Mafunzo ya ufungasahaji mazao ya nyuki.
  5. Mafuzo ya uongezaji wa thamani mazao ya nyuki.
  6. Huduma ya masoko "Kutafutiwa muuzaji au mnunuzi wa mazao ya nyuki"
  7. Mafunzo ni kwa vitendo na nadharia.
  8. Kutembelea shamba darasa letu la Nyuki (Kutalii)
  9. Tunauza mizinga ya ubao wa juu kwa 45000, na commercial kwa 110,000/= pia kwa mateja atakaye nunua zaidi ya mizinga 25 atajengewa nyumba ya nyuki(Bee house) bure tu ataanda vifaa.

 

UFUGAJI KUKU NA UANZISHWAJI WA MIRADI.

PDPR ina uzoefu wa miaka 4 katika utotoleshaji wa vifaranga na ufugaji wa kuku na imesaidia uanzishwaji wa miradi mikubwa na midogo ya ufugaji kuku wa aina mbali mbali na wanatoa huduma ya.

Mafunzo ya ufugaji kuku na kitabu.

  1. Utotoleshaji.
  2. Utengenezaji wa incubator za mafuta ya taa na umeme.
  3. Utengenezaji wa dawa za asili za kuchanja kuku za mimiea 6
  4. Ujenzi wa banda la kufugaji kuku na kulelea vifaranga.
  5. Uongezaji wa thamani mazao ya kuku.
  6. Huduma ya masoko ya mazao ya kuku kwa anayeuza au kununua "Kuku, mayai, vifaranga"
  7. Ushauri wa uanzishwaji wa mradi wa kuku na utotoleshaji.
  8. Utembeleaji wa mashamba yetu ya kuku "Kutalii"
  9. Tunauza vifaranga kwa 1200 vipo vya kienyeji, chotara, mayai, kroiler na kenbro na incubator ya bei ndogo ni Laki 2.5 ya mayai 60.

 

UFUGAJI SAMAKI NA UANZISHWAJI WA MIRADI.

PDPR inauzoefu wa ufugaji samaki na ina mabwawa yake ya shamba darasa na inahamasisha uanzishwaji wa miradi wa ufugaji samaki

HUDUMA YA.

  1. Mafuzo ya ufugaji samaki na kitabu.
  2. Ushauri elekezi wa uanzishaji na uendelezaji.
  3. Mafunzo na huduma ya uchimbaji bwawa na ujenzi.
  4. Mafunzo ya utengenezaji wa chakula cha kuku.
  5. Mafunzo ya uongezaji thamani mazao ya samaki.
  6. Uuzaji wa vifaranga vya samaki vya aina mbali mbali.
  7. Huduma ya masoko "Kuwaunganisha wauzaji na wanunuzi wa bidhaa za samaki"
  8. Kutembelea bwawa la samaki "Kutalii"

 

 

MAELEZO YA AWALI YA UCHIMBAJI VISIMA:

 

1)      Gharama za uchumbaji:

  • Kwa kila mita tunachimba kwa Tsh: 30,000/=, na gharama ya casing (PVC) kwa kila mita Tsh: 5000/= na water pump ni kati ya Tsh: 700,000/= hadi 1,500,000/= kutegemea na urefu wa kisima na muuzaji, kamba Tsh: 30,000/= na wire cable: Tsh: 50,000/=,
  • Upembuzi yakinifu: (Feasibility study): Tsh: 300,000/=
  • Utatakiwa kuandaa mfuko mmoja wa cement na tofari ndogo au za wastani 60 kwa ajiri ya kujengea mfuniko wa kisima,
  • Maji lita 1000 (Elfu Moja) ya kuchimbia, Kokoto ndogo mifuko 50 Tsh: 50,000/=

2)      Mteja atawajibika kufanya malipo ya survey pale atakapokuwa amefanyiwa tu, na malipo ya awali robo ya gharama atakazokuwa amekadiliwa siku ya kwanza pale Mitambo yote ikiwa imefika eneo lake la kazi na tayali kwa kuanza kumuhudumia na si vinginevyo na malipo mengine yanafanyika wanapomalizia kuchimba na kuweka PVC,

3)      Anaye hitaji pump atawajibika kulipa hela yote kwa mkupuo mmoja ili afungiwe,

4)      Kisima kitakamilika ndani ya siku moja hadi nne kutegemeana na mwamba na urefu.

5)      Kisima kina uwezo wa kutoa zaidi ya lita 4000 hadi 7000 kwa saa.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles