MALENGO YA JUMLA YA ASASI NA KAZI ZAKE;-
- Kutoa huduma za afya kwa jamii hususan vijijini.
- Maeneo yasiyo na shule tutapeleka huduma hiyo, sh/msingi, sekondari na sh/ za ufundi.
- Utoaji wa elimu ya hifadhi ya mazingira.
- Utunzaji wa misitu ya asili & vyanzo vya maji milimani.
- Upandaji miti na kuzuia uchomaji moto misitu.
- Kutoa elimu ya kilimo.
- Utengenezaji wa mabwawa ya maji kwa uvunaji maji ya mvua.
- Kilimo cha umwagiliaji na ufugaji bora.
- Kuwasaidia walemavu wa viungo & albino.
- Kuwasaidia yatima na watoto wa mitaani kutokana na mahitaji yao.
- Kusaidia wazee na wale wenye mahitaji maalumu.
- Kutoa elimu ya uzalishaji chakula na utunzaji.
- Kupunguza umasikini vijijini kwa kuanzisha miradi ya uzalishaji mali.
- Kuondoa tofauti za udini na ukabila.
- Kushughulikia upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa.