CHANIKA TUAMKE YOUTH ORGANIZATION (CTYO)
S . L .P ……………. Simu na.+255718586804/+255713849524/+255621153354
Chanika Wilaya ya Ilala Dar es Salaam
Utangulizi Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO) Ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa rami tarehe 13/03/2005 likijulikana kama Tuamke Arts Group na kusajiliwa tarehe 15/01/2015 katika Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia na Watoto na kupata namba 00NGO/00006839 . Shirika linatekeleza shughuli zake katika Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es salaam. Lengo kuu la CTYO ni kuwawezesha vijana kushiriki katika mipango,kusimamia na kuitekeleza ili kuleta maendeleo katika jamii. CTYO Inafanya shughuli za Ushawishi na Utetezi katika kuhakikisha utekelezaji wa haki ya Afya ya uzazi kwa vijanauzingatiwa wa maadili,malezi na huduma rafiki kwa vijana unazingatiwa.Shirika hili pia limelenga kufanya uchambuzi wa sera mbali mbali za vijana na kusimamia utekelezaji wake na Kutoa elimu ya Ujasiliamali kwa vijana. |
Kanuni za maadili
Muundo wa Uongozi
|
Usajili CTYO imesajiliwa chiuni ya sheria ya NGO NA. 24 ya mwaka 2002 kama iivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005.namba ya usajili 00NGO/00006839. Eneo utendaji kazi CTYO imesajiliwa kwa ngazi ya taifa na eneo la utendaji kazi Tanzania Bara ila kwa sasa tumeanza kufanya kazi katika kata mbilli za manispaa ya Ilala nazo ni; kata ya Chanika naZingiziwa . |
Dira ya Asasi Kuwa na vijana bora wanaoweza kupanga mipango, kuisimamia na kuitekeleza ili kujiletea maendeleo chanya. Dhamira Kufanya ushawishi na utetezi kuhakikisha kuwa vijana wanapata Afya,Maadili, Malezi na Huduma bora ya rafiki kwa vijana katika jamii na serikali kwa ujumla na kuchambua sera mbalimbali za vijana kuhakikisha kuwa sera hizo zinakwenda na wakati na kufanyiwa kazi. |
Malengo ya CTYO
Kuhakikisha kuwa vijana wanapata maslahi yao katika ngazi zote za serikali jamii kiujumla. Walengwa
|
Baadhi ya Mafanikio; ü Kuisajili Asasi kwa taratibu za sheria za NGO ü Kufungua Akaunti katika benki ya KCB ü Kufanya semina mbalimbali za Afya ya uzazi ü Tumefanikiwa kufanya mabonanza manne 4 ya Afya ya Uzazi kwa vijana ü Kujengewa uwezo na AMREF juu ya ü Kuandaa mpango kazi ü Kuandaa Bajeti ü Kuandaa taarifa ya utekelezaji na uwasilishaji ü Namna ya Uelimishaji wa jamii ü Namna ya Kuendesha Asasi. ü Kuviunganisha baadhi ya vikundi vya Bodaboda |
Baadhi ya Changamoto: ü Rasilimali Fedha ü Uhaba wa vitendea kazi ü Upungufu wa waelimishaji Rika ü Ukosefu wa wafadhili wa kufadhili shughuli za CTYO ü Kuibiwa baadhi ya vitendea kazi Mipango Endelevu ü Kuendelea kutoa Elimu ya Afya ya uzazi kwa vijana ü Kuendea kupambana na Makundi hatarishi kama ü Wafanya biashara ya ngono ü Vikundi vinavyo tumia dawa za kulevya ü Vikundi vya kamali na Bodaboda |
ü Kujengea uwezo vikundi mbalimbali vya kijamii katika suala zima la kujikwamua kiuchumi. ü Kuendelea kutoa elimu ya VVU na Ukimwi na kuamasisha jamii upimaji kwa hiari ü Kuendelea kupambana na Ukatili zidi ya watoto na wanawake ü Kufanya Ushawishi na Utetezi kuhakikisha kuwa kuna kuwa na Uwazi,Uwajikaji,na Utawala bora katika sekta ya Afya. Njia zinazotumika kuwafikia walengwa ü Semina ü Midahalo ü Vipeperushi ü Sanan Shirikishi ü Kutembelea vituo vya serikali vinavyo toa huduma kwa jamii kama: ü Vituo vya Afya vya Serikali ü Vituo vya Elimu ya Serikali ü Ofisi za serikali za Mitaa,kata,wilaya,Mkoa na Taifa ü Kujengea Uwezo jamii kutambua haki za mteja katika kupata huduma ya Afya katika vituo vya afya vya serikali. ü Kufanya Ushawishi na Utetezi kuhakikisha kuwa vijana wanapata masilahi yao katika jamii na serikali kwa ujumla. ü Kuwajengea uwezo vijana kujikwamua kiuchumi,kutoa elimu ya Ujasilia mali,kuwaunganisha vijana kuwa pamoja katika maamuzi na kuhakikisha kuwa tunaingiza agenda za vijana WDC ü Vyombo vya Habari Mawasiliano/Mitandao ya kijamii kama ü Sms kampeini ü Facebook ü Twitter ü What’s App ü Instagram
|
|