HISIA CULTURAL TROUPE-HCT
February 8, 2017 Iringa
HCT ni asasi iliyosajiliwa na Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) kwa usajili namba BST/2365 na inajishughulisha na uelimishaji wa jamii kwa njia ya sanaa za maonyesho. Sanaa hizo ni kama vile maigizo shirikishi, vichekesho, utambaji wa hadithi na ushairi.
Aidha asasi yetu inaelimisha jamii katika maeneo mbalimbali kama vile kinga dhidi ya UKIMWI, athari za madawa ya kulevya, afya ya uzazi na ujinsia, utawala bora, utafiti, ukuzaji wa vipaji, michezo, elimu rika, utunzaji wa mazingira na uhamasishaji wa utalii wa ndani.
Sasa Asasi yetu inapokea vijana kwa ajili ya kufanya field. Vijana hao wawe na sifa zifuatazo:-
- Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
- Awe na uwezo wa kuandika proposal
- Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 35
- Awe na nidhamu, mwaminifu na mbunifu
Kwa mawasiliano zaidi piga namba zifuatazo:-
0754 439740
0786 439740
0715 474527
0652 600002
hisiaone@gmail.com