UTANGULIZI
Mwela theatre group ni kikundi cha Vijana kilichoanzishwa tarehe 28/1/2003 ni muunganiko wa vijana kutoka vikundi vingine vya Vijana vya kujitolea na wengine wametoka kwenye mazingira magumu na watumiaji wa dawa za kulevya wote hawa waliunda dira ya pamoja kuwa na Jamii watanzania wanaoheshimu misingi ya Utawala Bora. Mwela theatre group imepata usajiri wake tarehe 7/3/2005 chini ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)ikiwa na wanachama 15 wanawake 6 na wanaume 9
Mwela theatre group mwaka 2003 hadi mwaka 2005 ilikuwa ikifanya kazi katika kata 5 za Manispaa ya Temeke ilipata usajiri wa NGO tarehe 30/1/2008 na kuongeza wigo wa kufanya kazi katika mikoa mitatu mkoa wa Dar-es-salaam,Mkoa wa pwani na Mkoa wa Tanga
Katika Mkoa wa Dar-es-Salaamu mwela inafanya kazi mkoa nzima.
Kwa Mkoa wa pwani inafanya kazi katika wilaya ya Mkuranga,Rufiji,Kisarawe na Kibaa
Katika mkoa wa Tanga inafanya kazi katika wilaya ya Lushoto
Mpaka sasa kikundi kimeweza kufanya shughuli mbalimbali za kiserikali
na taasisi zisizo za kiserikali,manispaa ya Temeke,
Mwela iliweza kufanya shughuli hizi sehemu mbalimbali ndani ya manispaa ya temeke na nje ya manispaa ya temeke
mwela ilishawishika kujiingiza katika maswala ya kuelimisha jamii kutokana na jamii
Kutoelewa maswala mbalimbali yanayowahusu na matatizo mbalimbali yanayowakumba
Kumetokea vijana wengi kutojitambua wao ni nani? na wanatakiwa kufanya nini? Na wanamajukumu gani katika jamii yao inayowazunguka baada ya kukaa na kuilaumu serikali kama sisi hapo mwanzoni tulivyokuwa tukifanya
Vijana wengi wamejikuta wakiingia katika makundi mabaya ya kutumia dawa za kulevya kutokana na kutojitambua wamekuwa wakichanganya dawa kwa wakati mmoja
Hivyo uleta madhara mara mbli kwa zile dawa zinazo poozesha mwili,zinazofanya mwili kuchangamka na zile zinazotoa tafsiri potofu hivyo vijana wengi wamejikuta wakichanganya na kuleta tafsiri tofauti na hata wakati mwingine uchanganyikiwa katika ubongo na kuchanganyikiwa akili kutokana na hali zao za kiafya,mazingira wanayotumia dawa hizo na lishe wanayoipata
Mwela inasaidia serikali kuzifafanua sera mbalimbali kwa jamii kutokana na jamii
Yetu waliokuwa wengi upenda sanaa na michezo kuliko kujisomea vitabu mwela
Imekuwa mstari wa mbele kusoma sera mbalimbali na kuzitengenezea nyimbo,ngonjera,mashairi,maigizo na ngoma ili jamii inayopenda sanaa zaidi au hata wale ambao hawajui kusoma na kuwandika nao upata hujumbe
Tunapotumia sanaa tunapata walengwa wengi zaidi wale ambao tayari wameshaathirika na wale ambao hawajaathirika lakini pia tunawapata elimu watoto ambao wanajengeka kimaadili mapema na kupata taarifa sahihi mapema kabla hawajakuwa na mitazamo potofu kuhusu dawa za kulevya
Utumia bend katika maeneo ambapo uwa wakati mwengine hawapendi ngoma na maigizo.
Utumia wataalamu(wawezeshaji na wakaguzi) mbalmbali ndani ya kikundi na nje ya kikundi pindi tunapotaka kuendesha mafunzo na kuendesha shughuli zetu kwa ujumla. mwela inaamini kuwa ikiwa tutawapa watu uelewa juu ya dawa za kulevya tutaweza kupunguza madhara ya VVU/UKIMWI kwa watumiaji kuchangia sindano moja,kupunguza homa ya Ini lakini pia tutapunguza madhara ya afya kwa watumiaji ambao katika eneo letu wanatumia sehemu pachafu,wanaiba,kupora na vitendo vya uharifu kitu ambacho sio sifa ya dawa za kulevya hila ndio mitazamo ya watumiaji wa dawa za kulevya na kusababisha kero na maafa katika jamii
Mwela theatre group wamekuwa wakielimisha jamii juu ya Utawala bora ngazi ya kaya na kuleta mitazamo chanya kwamba kiongozi ni mtumishi wa wananchi na hivyo wananchi wafahamu kuwa viongozi lazima wawajibike kwao na pale wanapoenda tofauti wawajibishwe kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi na sio kuchukua hatua mkononi au kulalamika tu kitu ambacho kinasababisha viongozi wasio waadilifu kupata nafasi ya kaa madarakani bila kuleta mafanikio yoyote kwa wananchi
Mwela katika utawala bora imejikita zaidi katika kuhamasisha jamii kushiriki katika mikutano ya serikali za mitaa/vijiji na kuhoji/kudai mapato na matumizi ya serikali yao na kodi wanazozitoa
Mwela katika utawala bora imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za kujitolea katika maeneo yao ili kuleta mafanikio ya haraka na kujiletea maendeleo wao wenyewe
Mwela katika utawala bora inahamasisha jamii kushiriki katika upangaji wa mipango ya kijiji/kata na utekelezaji wake na kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara na mwisho kufanya tathimini ya miradi hiyo
mwela theatre group imekuwa mstari wa mbele katika kuelimisha jamii juu ya haki za binaadamu,haki za wanawake,haki za watoto,haki za walemavu na makundi yaliyo pembezoni kama vile watumiaji wa dawa za kulevya,watu wanaoishi na vvu/ukimwi na wazee