Afya ya Uzazi kwa Vijana:
Kwanini tunawalengo sana vijana
- Kwanza kabisa ndiyo Walengwa wa Asasi ya Chanika Tuamke Youth Organization{CTYO}
- Vijana ndiyo wanao kumbwa na Matizo mbalimbali kutokana na mabadiliko ya kimaumbile kama.
Ujana hatarishi unaazia na:
Ujana balehe
Ujana balehe ni kipindi cha mpito,kutoka utotoni hadi utu uzima.Kwenye umri huu kijana hukua haraka kimwili,kiakili na kihisia.
Kwa tafsili ya Shirika la Afya (WHO) Umri wa kijana ni kati ya miaka 10 -20
Kwa tafsili ya Umoja wa Nchi za Mataifa umri wa kijana ni miaka 10 -24
Kuna hatua tatu3 za Mabadiliko wakati wa Ujana .Hatua hizo ni:
Umri wa kati ya miaka( 10 – 13)
Kubalehe na kukua haraka,tabia ya kujaribu,anaanza kufikiria kinadharia,Utashi wake unakua mkubwa zaid hadi nje ya familia yake,tabia yake uvuka nje ya mipaka ya familia yake,anathamina sana watu maarufu na vijana wa rika lake wanaokubalika.
Umri wa kati ya miaka( 14 – 16)
Anaendelea kukua kimwili na kiakili.Anabadilisha tabia na kuangalia kama anakubalika kwa wazazi,anakua na stadi za Uchambuzi na uelewa wa matokeo ya tabia,anashawishiwa zaidi na rika katikakuiga tabia na mwenendo,anavutiwa zaidi na wanarika wa jinsia tofauti nay eye.
Umri wa kati ya miaka( 17 – 19)
Anafikia ukomo wa kukua kimwili na kijinsia,uwezo wa kutatua matatizo anakua mkubwa zaidi,uhusiano wa kirika unapungua,unaungana tena na familia yake,uhusiano wa karibu unakua muhimu zaidi kuliko uhusiano wa makundi,kuongezeka uwezo wa kuchagua mambo kiutuuzima na kuingia katika ya kufanyakazi.
Mambo yanayochangia mabadiko ya kitabia katika ujana
- Majukumu ya kijinsia
- Mgawanyo wa kazi uliowekwa na jamii kwa mwanaume na mwanamke.
- Mila,Desturi na taratibu zilizopo mahali anapoishi kijana.
Shinikizo la kundi rika (Wanarika)
- Kijana huiga tabia zinazo kubalika na zenye kuletamadhara mfano,kutumia madawa ya kulevya,kuvuta bangi.
- Kupoteza malengo yake ya Maisha
- Kukatisha Masomo
Uhusiano wa wazazi/Jamii,
- Namna wazazi wavyomlea kijana – Mfano kutomfuatilia tabia yake
- Jamii inavyowachukulia vijana.
Msimamo wa kijana
- Kijana kutojiamnii na Kujitambua
- Kushindwa kuwa na mahusianomazuri na marafiki,ndugu na hata jamii
TABIA HATARISHI KWA VIJANA
Wakati wa ujana kuna tabia mbailimbali ambazo zinaweza kuhatarisha maisha ya kijana,tabia hizo ni,:
Tabia hatarishi za kimaumbile
- Ukosefu wa chakula cha kutosha na chenye lishe kamili huathiri ukuaji wa kijana
- Magonjwa kama kuharisha,magonjwa yanayo ambukizwa kwa njia ya hewa ya mara kwa mara yasiyotibiwa ipasavyo huathiri ukuaji,saikolojia na maendeleo ya vijana.
- Kitendo cha ukeketaji kwa baadhi ya wasichana ambao wamefanya,huweza kuathiri ukuaji na hisia tofauti kwenye ujinsia na afya ya uzazi kwa vijana.
Tabia hatarishi za kihisia
- Mabadiliko ya ukuaji pamoja na vichocheo inaongeza matatizo ya kiafya ya kiakili wakati wa balehe.
- Kuumizwa kwa ujinsia na matusi kutoka kwa watu wazima {hali ambayo kijana hawezi kuzuia}
Tabia hatarishi za hali ya kiuchumi
- Ukosefu wa upatikanaji wa fedha, wana mahitaji makubwa yanayoishia kwenye hatari za afya kama vile maambukizo ya magonjwa.
- Vijana wapo katika hali ngumu ya kimaisha ambayo huweza kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya
- Wasichana ukumbwa na tatizo la unyanyasaji wa kijinsia kwani husabishwa na mgao usio sahihi wa chakula na huduma za afya.Uwepo mdogo wa ushawishi kufanya ngono salama.
Sababu za tabia hatarishi
Kijana hupambana na tabia mbalimbali ambazo humweka hatarini kwa sababu zifutazo:
- Mabadiliko ya kimaumbile,kihisia na ujinsia yanayotokea
- Uhusiano wa rika,kifamilia na kijamii
- Udadisi na msukumo utokanao na kundi rika lenye uzoefu mbalimbali.
- Mila na desturi ambazo zinahitaji kijana kuokoka na kuwa mbali na familia yake anapokua
- Mila na desturi katika baadhi ya familia yake anapokua
- Mila na desturi katika baadhi ya jamii zinazomsukuma kijana kujiingiza katika hatari za ujinsia kama njia ya kuonesha/kuonekana mwanaume.
Aina za Tabia hatarishi.
- Uamuzi wa haraka bila kutafakari
- Kutenda kitu kwa pupa
- Ubishi,ubishani wa kutaka kujaribu ili kujilinganisha na kundi rika au watu wazima
- Utumiaji wa dawa za kulevya kwa majaribio,
- Kufanya tendo la ndoa isiyo salama
Mambo muhimu yanayo husiana na tabia hatarishi
Tanzania ina utajiri wa Mila mbalimbali mila nyingine ni nzuri lakini nyingine za hatari,hasa kwa vijana walio katika balehe,
Mila na desturi za makabila mbalimbali
Mfano mila za kuwatukuza wavulana na kuwachochea kuonesha uanaume wao huwapeleka katika mienendo ya kuhatarisha afya zao.
- Hali tofauti za kibinadamu
- Msukumo wa kijamii
- Mahitaji na upatikanaji wa vitu,
- Umri sahihi wa kuelewa hatari
Athari za Tabia hatarishi
Tabia hatarishi humfanya kijana kuishia kwenye matatizo mengi baadhi ni kama haya yafuatayo:
- Kuumia kama Majeraha
- Matatizo ya kilishe kuzidi au lishe pungufu(malnutrition)
- Upungufu wa damu hasa kwa wasichana kwani hupungua kutokana na hedhi
- Upungufu wa Vitamini A na kalsium
- Wasiwasi na msongo wa mawazo
- Utumiaji wa dawa za kulevya.
Njia za kuzuia athari zitokanazo na tabia hatarishi
- Kupata habari sahihi na Elimu kuhusu haki za Afya ya uzazi kwa vijana
- Kushawishi jamii ili kutokomeza tabia zilizo na madhara mfano ukeketaji
- Kuwafundisha vijana stadi za maisha ili wazitumie katika maisha yao ya kila siku
- Kutoa Elimu na ushauri juu ya ulaji wa chakula bora chenye kutosheleza mahitaji ya mwili