UCHAGUZI MKUU 2015 (Tangazo la Redio)
JE DIWANI WAKO WA SASA, ANATIMIZA WAJIBU WAKE?
SIKILIZA,
Mojawapo ya wajibu na kazi za diwani ni Kuhakikisha kuwa fedha na mali nyingine za Halmashauri zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ya kuleta maendeleo na kuboresha huduma.
Fedha za halmashauri ni pamoja na michango ya wananchi, mapato kutoka vyanzo vya ndani kama ushuru, faini na kodi mbalimbali; pamoja na ruzuku kutoka serikali kuu na fedha kutoka wafadhili.
Kuna madai kuwa halmashauri zetu za wilaya, miji, manispaa na majiji kuna MCHWA unaotafuna fedha. Mkazi wa mkoa wa mbeya tambua kuwa mchwa huu unaweza kukomeshwa kwa kuwepo madiwani mahiri, makini na waadilifu.
Tafakari kwa makini, iwapodiwani wako wa sasa katimiza wajibu wake huo, kama amefanya hivyo, huyo ni mfano wa kiongozi bora, mshawishi agombee tena. Lakini Kama unadhani hajatimiza wajibu wake, jitathimini kisha jitokeze kuwania nafasi hiyo au mshawishi mtu unayedhani anaweza kutekeleza wajibu huo. "
Kusikiliza audio bonyeza HAPA au kiunganishi http://vocaroo.com/i/s1sEwBhBlQW5