NAFASI ZA KAZI KWA MAAFISA MASOKO
MAAFISA MASOKO WAANDAMIZI 70 NA MAAFISA MASOKO 200 WANAHITAJIKA Asasi ya Pretty Development for Poverty Reduction (PDPR) inayojihusisha na kutoa huduma za jamii, mafunzo, ushauri, ufugaji wa kuku, samaki na nyuki inazo nafasi za kazi kama ifuatavyo;
Maafisa masoko waandamizi 70.
Asasi ya Pretty Development for Poverty Reduction inataka kuajiri Maafisa masoko waandamizi wenye ujuzi na wachapakazi. Bidhaa zinazouzwa na huduma zinazotolewa na kampuni ni pamoja na mashine za kutotolea vifaranga vya kuku, mizinga ya nyuki, vifaranga, miche ya matunda na mbao, Ushauri wa biashara, semina za ujasiriamali, kuandaa michanganuo,fursa za kilimo biashara na ufugaji wa kuku, samaki, nyuki, sungura, na mikopo ya mashine na vifaa vingine.
Kazi zake;
1.Kuandaa mikakati ya mauzo na malengo ya mauzo kwa kampuni
2. Kutafuta masoko na kuuza bidhaa za kampuni
3. Kutangaza bidhaa za kampuni na kutafuta wateja.
3. Kusimamia na kuongoza maafisa masoko walio chini yake.
4. Kuandaa semina.
Sifa za muombaji;
Awe na shahada ya Biashara mchepuo wowote.
Siyo lazima kuwa na uzoefu kazini lakini akiwa na uzoefu wa kufanya kazi hizi kwa muda wa kuanzia mwaka mmoja na zaidi atafaa zaidi.
Mshahara;
Mwombaji atakayepata ajira atalipwa asilimia 20% ya mauzo atakayofanya kwa mwezi.
Maafisa masoko 200.
Asasi ya Pretty Development for Poverty Reduction inataka kuajiri Maafisa masoko wenye ujuzi na wachapakazi. Bidhaa zinazouzwa na huduma zinazotolewa na kampuni ni pamoja na mashine za kutotolea vifaranga vya kuku, mizinga ya nyuki, vifaranga, miche ya matunda na mbao, Ushauri wa biashara, semina za ujasiriamali, kuandaa michanganuo,fursa za kilimo biashara na ufugaji wa kuku, samaki, nyuki, sungura, na mikopo ya mashine na vifaa vingine.
Kazi zake;
1. Kutafuta masoko na kuuza bidhaa za kampuni
2. Kutangaza bidhaa za kampuni na kutafuta wateja.
3. Kuandaa semina
Sifa za muombaji;
Awe na elimu ya Kidato cha nne na kuendelea, mwenye kujituma ambaye anaweza kuuza .
Akiwa na cheti au shahada ya Biashara mchepuo wa masoko atatufaa zaidi.
Siyo lazima awe na uzoefu katika kazi lakini kama ana uzoefu wa kufanya kazi katika makampuni ya usambazaji wa bidhaa atatufaa zaidi.
Mshahara;
Mwombaji atakayepata ajira atalipwa asilimia 15% ya mauzo atakayofanya kwa mwezi.
Kwa maelezo zaidi piga simu 0754397178 au tuma maombi kwa email; pdprngo@gmail.com
IMMA SALINGWA
MKURUGENZI MTENDAJI PDPR Njombe. www.envaya.org/pdpr