Sakale Development Foundation katika kipindi cha tangu kuandikishwa rasmi imejitahidi kutekeleza miradi mbalimbali kwa kadri ya kiasi cha fedha zilizo patikana.
"Miradi iliyotekelezwa"
Mradi waupanuzi wa bustani ua miche ya miti,
Mradi huu ulitekekelezwa mwaka 2008 kwa ufadhiuli wa shirika moja la Kimarekani linaloitwa Friends of Tanzania, katika mradi huu shirika lilifanikiwa kukuza miche ya miti 50,000 ambayo baadaye tuliigawa kwa wanavijiji mbalimbali ili waweze kuipanda katika maeneo ya mashamba yao.
Mradi wa mafunzo juu ya utawala bora,
Mradi wa mafunzo juu ya utawala bora katika ngazi ya kijiji ulitekelezwa na SADEF katika mwaka 2009, mradi huu ulihusisha wajumbe wa halmashauri za serikali za vijiji kutoka katika vijiji vya mbomole, Sakale, Kwemwewe na Shambangeda katika kata ya misalai wilaya ya Muheza. Ulitekelezwa kwa ufadhili wa shirika la The foundation for civil society la Mjini Dar es salaam.
Mradi wa Elimu juu ya utawala bora
Mradi wa mafunzo juu ya utawala bora katika ngazi ya vijiji ulitekelezwa na SADEF katika mwaka 2010, mradi huu ulihusisha wajumbe wa halmashauri za serikali za vijiji kutoka katika vijiji vya Kisiwani, Mikwinini, Mlesa na Mashewa katika kata ya Kisiwani wilaya ya Muheza. Ulitekelezwa kwa ufadhili wa Ofisi ys Raisi, Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma,Mfukuko wa Uadlifu,Uwajibikaji na Uwazi.
Mradi wa utafiti juu ya mtazamo Rushwa
Mradi huu ulitekelezwa na shirika linaloitwa ForDIA la Mjini Dar es salaam katika mikaoa kadhaa nchini Tanzania.SADEF tulikuwa asasi mwenyeji wa ForDIA na tukashirikiana nao kutekeleza mradi huu katika wilaya Saba za mkoa wa tanga ambazo ni Lushoto,Muheza, Pangani, Korogwe,Mkinga Kilindi na Tanga mjini. mradi huu ulifadhiliwa na shirika the Foundation for civil society
Mradi wa Raia Makini 2010 [Elimu ya Mpiga kura]
Mradi huu ulitekelezwa katika mikoa 14 ya Tanzania bara shirika la ForDIA ndio walikuwa watekeleza wakuu, SADEF tulishirikiana na ForDIA kuutelekeza mradi huu katika mkoa wa Tanga ambapo tulihusika katika wilaya za Lushoto,Korogwe, Mkinga, Muheza na Tanga mjini. mradi huu ulifadhiliwa na UNDP
Mradi wa Kuwajengea Uwezo Wanachama wa SADEF
Mradi huu umetekelezwa na SADEF katika Kipindi cha Desemmba 2010 hadi February 2011. katika mradi huu wanachama wa SADEF walijifunza jinsi ya kuendesha asasi zisizokuwa za kiserikali, Utunzaji wa fedha na Kumbukumbu mbali mbali za asasi, Kubuni na kuendesha miradi ya asasi na namna ya kutengeneza mpango Mkakati wa Asasi. Mradi huu ulitekelezwa kwa ufadhili wa shirika la The Foundation for civil society la Mjini Dar es salaam.
Mradi wa ufugaji wa nyuki wa Asali
Mradi huu umeanza utekelezaji wake April 2011. unatekelezwa kwa ufadhili wa shirika la kimarekani linalojulikana kwa jina la Friends of Tanzania [FOT]
Mradi wa Kujenga Uwezo wa Mabaraza ya Usuluhishi Ngazi ya Vijiji na Kata.
TAARIFA YA SHUGHULI ZILIZOTEKELEZWA KATIKA MRADI WA MABARAZA YA KATA.
UTANGULIZI:
Mradi wa mafunzo ya kujenga uwezo wa Mabaraza ya Usuluhishi ngazii ya vijiji na Kata umetekelezwa na Sakale Development Foundation katika Kata za Mbomole, Amani, Kisiwani, Zirai na Misalai Wilayani Muheza.
Mradi huu umetekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la The Foundation for Civil Society ambapo ulifadhiliwa kiasi cha Tshs. 43,815,870/=.
Mradi ulinzinduliwa na kuanza shughuli zake tarehe 24/9/2012.
Afisa Elimu wa Wilaya ya Muheza akizindua mafunzo ya Kujenga Uwezo Wa Mabaraza Ya Kata kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza.
Lengo la mradi ilikuwa ni kuboresha utendaji kazi wa Mabaraza ya usuluhishi ngazi ya vijiji na Kata ili yafanye kazi zake kwa kuzingatia taratibu, kanuni kama zilivyoainishwa katika sheria No. 7 ya mwaka 1985.
Aidha mradi ulilenga kuongeza matumizi ya mabaraza haya. Kwa maana ya idadi ya wananchi wanaotumia mabaraza katika kutatua migogoro miongoni mwao. Mradi ulikuwa na hatua mbalimbali za utekelezaji na kwamba kwa kuzingatia hatua hizo za utekelezaji mradi ufikie matokeo tarajiwa ambayo yalikuwa ni MABARAZA YA USULUHISHI NGAZI YA VIJIJI NA KATA YAMEELEWA WAJIBU NA MAJUKUMU YAO na JAMII/ WANANCHHI WAMETAMBUA UMUHIMU WA KUTUMIA MABARAZA YA KATA KATIKA KUTATUA MIGOGORO YAO, hayo yalikuwa ni matokeo ya awali na MABARAZA YA USULUHISHI NGAZI YA VIJIJI NA KATA YANATOA HUDUMA KWA KUZINGATIA SHERIA NAMBA 7 YA MWAKA 1985 ifikapo July 2013 ndio lilikuwa tokeo kuu tarajiwa. Ambapo viashiria vya kufikia matokeo hayo vilitajwa kuwa ni IDADI YA MASHAURI YANAYOSIKILIZWA NA KUTOLEWA MAAMUZI YA HAKI na KUPUNGUA KWA IDADI YA MASHAURI YASIYOKUWA YA JINAI YANAYOFUNGULIWA KATIKA VITUO VYA POLISI NA MAHAKAMA walengwa wa mradi walikuwa wajumbe 115 wa Mabaraza ya usuluhishi ngazi ya Vijiji na Kata.
Afisa Tarafa ya Amani Bw. Hashimu Msagati akimsindikiza mgeni rasmi kuelekea kwenye ukumbi wa mkutano.
SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
Afisa Elimu wa Wilaya Muheza Ndugu Said Kondo alizindua Mradi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza tarehe 24/9/2012 katika ukumbi wa FINIDA uliopo Amani Nature Reserve. Katika hotuba yake kwa washiriki wa mafunzo na wageni waalikwa aliwaasa washiriki wa mafunzo kujifunza kwa bidii ili watakapotoka hapo waweze kutoa huduma nzuri kwa jamii.
Aidha aliwahidi wananchi kuwa kupitia mkutano huu amesikia kilio cha Afisa Tarafa kwamba kituo cha Polisi cha Amani kina Askari wanne tu atamweleza Mkuu wa Wilaya ili aweze kuongeza Askari Polisi katika kituo hiki, pia aliwaasa na kuwaomba viongozi wa dini waliohudhuria uzinduzi huu washirikiane na mabaraza ya usuluhishi katika kuhakikisha uwepo wa Amani katika maeneo yetu na kwamba kusiwepo na watu ambao wanatumia dini kama kichaka cha kujificha wakati wakiwa ni watenda maovu ndani ya jamii.
Akizungumza katika siku ya uzinduzi wa mradi huu Afisa Tarafa bwana Hashimu Msagati alitoa shukrani nyingi kwa Asasi ya Sakale Development Foundation kwa kuleta mradi huu katika Tarafa hii kwani kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa wananchi ambazo zinazodai mabaraza ya usuluhishi katika kata zote yanajihusisha na vitendo vya kukosesha haki za watu kupitia utendaji mbovu na upokeaji rushwa.
Aidha aliwapongeza viongozi wa dini kushiriki katika shughuli hii kwa kuwa wenyewe ni wadau muhimu katika kuhakikisha haki na Amani inadumu miongoni mwa jamii. Pia alisema kwamba Tarafa ya Amani kuna mahakama moja ambayo inafanya kazi kwa wiki mara 2 lakini wakati mwingine inaweza isifanye kazi katika wiki, hivyo kusababisha mlundikano wa mashauri mahakamani.
Hivyo kuyajengea uwezo mabaraza yetu ya usuluhishi kutatusaidia sana katika kusimamia haki za wananchi wetu, aidha Afisa Tarafa aliwatambulisha waandishi wa habari waliokuwepo katika uzinduzi huo ambapo aliwataja William Mngazija kutoka ITV na Steven William kutoka gazeti la Mwananchi. Pia alimtambulisha Afisa Maendeleo Wilaya Bi. Heriet Nyangasa na Bi. Aziza Almasi Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania (CCM) katika Wilaya ya Muheza.
MAFUNZO BAADA YA UZINDUZI WA MRADI
Mafunzo yalianza kwa kutengeneza kanuni zitakazotawala wakati wa kipindi chote cha mafunzo ambapo zifuatazo zilikuwa ndio kanuni (1) kushirikiana
(2)simu zizimwe au ziwe katika mtetemo (3) kuchangia mawazo (4) kujali muda (5) Kuhesshimu mawazo ya mwingine .
Aidha washiriki walitoa hofu zao ambapo hofu zifuatazo zilibainishwa (1) washiriki kutoka mbali na wanasafiri kwa miguu (2) kutopata chakula .
Hata hivyo mwenyekiti wa Sakale DeveopmentFoundation aliwatoa hofu kwamba kuna fedha watapewa washiriki kwa ajili ya malazi na kutakuwa na chai ya saa 4, chakula cha mchana na usiku ambacho kitakuwa cha kushiba.
Washiriki, wawezeshaji na viongozi wa Sakale Development Foundation walitengeneza ratiba ya jumla ya muda wa kuanza mafunzo na kufunga mafunzo kwa kila siku, ambapo ilikubalika mafunzo yaanze saa 3:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 Jioni.
Baada ya makubalianohayo muwezeshaji alibainisha mada ambazo zitajadiliwa katika siku ya kwanza akazitaja kama ifuatavyo;-
- Sheria ya mabaraza ya kata namba 7 ya mwaka 1985.
- Sheria ya ardhi ya mwaka 1982 na ikafanyiwa marekebisho mwaka 2005 ambapo alianza na mada ya 1 kwa kutoa mhadhara mfupi na kisha kuwagawa washiriki katika kazi za makundi, baadaye washiriki waliwasilisha kazi za makundi yao na kuzijadili kwa pamoja. Kisha washiriki walienda kupata chai ilipofika saa 4:30 na kurejea tena darasani ilipotimu saa 5:20.
Mada ya pili iliwasilishwa na mwezeshaji kwamba ni sheria ya ardhi ya mwaka 1982 iliyofanyiwa maboresho mwaka 2005, alitoa mhadhara mfupi kisha kuwagawa washiriki katika kazi za makundi, ambazo zilianza saa 6:00 hadi saa 7:00 na washiriki walienda kupata chakula cha mchana kutoka saa 7:01 hadi saa 8:00 waliporejea waliendelea na kuwasilisha kazi za makundi hadi saa 9:00 Alasiri na baada ya hapo mwezeshajii alitoa majumuisho ya mada nzima hadi ilipofika saa 9:45 kwa kuwa muda ulikuwa unakaribia kumalizika mwezeshaji alimkabidhi mratibu wa mradi na uongozi wa Sakale Development Foundation waweze kushughulikia maswala ya utawala.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo kata ya Kisiwani
SIKU YA PILI
Baada ya washiriki kujisajili mafunzo ya siku ya pili ambapo mada za siku hiyo zilikuwa;-
- Muundo na uongozi, mchakato wa kupata wajumbe wa baraza la kata.
- Sifa za wajumbe, uendeshaji wa mashauri na utatuzi wa migogoro ya ardhi.
- Kufungua jalada, kusikiliza, ushahidi, maamuzi na hukumu.
Mada hizi zilijadiliwa kwa mtindo uleule wa mhadhara mfupi kutoka kwa mwezeshaji na kisha washiriki kufanya kazi katika makundi na baadaye kuziwasilisha katika darasa la pamoja kwa mijadala mipana na maboresho kufanywa.
SIKU YA TATU
Washiriki wa mafunzo katika siku ya tatu walijifunza / kujadili mada zifuatazo-
- Mamlaka na uwezo wa mabaraza kimadai na kijinai, mahusiano ya WDC na baraza la Kata.
- Tafsiri ya mtoto.
- Haki za binadamu na haki za mtoto.
- Utambuzi wa urahisi wa kuathirika kwa mtoto.
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika kazi za vikundi
SIKU YA NNE
Washiriki walijifunza juu ya mada zifuatazo;-
- Mfumo wa utendaji kazi wa Serikali za mitaa na mabaraza ya Kata.
- Taasisi ya Mahakama Tanzania na muundo wake.
- Huduma ya ustawi wa jamii.
- Haki na wajibu wa mtu katika utekelezaji na usimamizi wa sheria zinazolinda ustawi wa watoto.
Mshiriki akiwasilisha kazi ya kikundi
SIKU YA TANO
Washiriki walijifunza mada zifuatazo;-
- Sheria na utaratibu wa kumiliki mali.
- Sheria ya ardhi na umilikaji mali Tanzania.
- Sheria ya ardhi na umikaji mali Tanzania.
- Kutengeneza mpango kazi wa baraza la kata yao.
Baada ya mafunzo ya siku tano kukamilika tarehe 28/9/2012 kundi la pili la washiriki 23 kutoka kata za Mbomole na Misalai lilianza mafunzo tarehe 1/10/2012 hadi 5/10/2012. Mada zilizojadiliwa katika kundi la kwanza ambalo lilihusisha washiriki kutoka Kata za Amani na Kisiwani zilijadiliwa kwa Mtindo uleule hata katika kundi hili la pili.
Katika shughuli hii ya mafunzo kulinunuliwa mwongozo wa utendaji kazi kwa mabaraza ya usuluhishi kata ambapo nakala 115 zilizonunuliwa ziligawiwa kwa wajumbe wa mabaraza ya usuluhishi ili waweze kufanya rejea wakati wakishughulika na usuluhishi wa migogoro katika jamii.
Aidha kundi la mwisho la wajumbe wa mabaraza ya usuluhishi ngazi ya vijijini na kata lenye washiriki 23 liliwahusu wajumbe wa kutoka katika Kata ya Zirai, wao pia walipata mafunzo ya siku 5 wakijifunza mada zilezile walizojifunza makundii manne (4) yaliyotangulia na kwa mtindo uleule.
Washiriki wa mafunzo wakimsikiliza mwezeshaji wa mafunzo
II: MIKUTANO YA HADHARA KWA WANANCHI
Katika mpango kazi wa mradii kulikuwa na shughuli ya kufanya mikutano ya hadhara katika kata za mradi yenye lengo la kuwahamasisha wananchi kutumia mabaraza ya usuluhishi ngazi ya vijiji na kata katika kutatua migogoro miongoni mwao. Hii ilifanywa kwa imani kwamba baada ya wajumbe wa mabaraza ya usuluhishi ngazi ya vijiji na kata kupata mafunzo na kuelewa wajibu na majukumu yao wataweza kutoa huduma bora kwa wananchi hivyo wananchi hawa waambiwe juu ya jambo hili ili wasiendelee kufuata huduma hizo polisi na mahakamani ambako ni sehemu iliyombali na makazi ya wananchi waliowengi jambo ambalo linawachukulia muda mwingi ambao wangetumia katika shughuli za uzalishaji mali.
Mkutano wa hadhara kwa wananchi wa kata ya Mbomole ulifanyika katika Kijiji cha Sakale ambapo wananchi wa kata hiyo walipewa ufafanuzi mbalimbali kuhusu kazi za mabaraza ya usuluhishi ngazi ya vijiji na kata yanavyopaswa kufanyakazi zake, umuhimu na faida za kutumia mabaraza haya katika kutatua migogoro mbalimbali katika jamii. Aidha walifahamishwa kwamba mabaraza ya usuluhishi ngazi ya vijiji na kata yao ya Mbomole wamepewa mafunzo juu ya wajibu na majukumu yao katika kutoa huduma ya usuluhishi na utatuzi ambayo inajitokeza katika jamii.Aidha wananchi kupitia mkutano huu walipata ufafanuzi kuhusu ugonjwa wa UKIMWI ambapo mshauri nasaha na muuguzi kutoka katika hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza aliwaeleza wananchi mambo mbalimbali kuhusu UKIMWI.
- UKIMWI ni ugonjwa gani, unapatikana kwa namna gani, namna ya kujikinga na kujihadhari na ugonjwa wa UKIMWI, umuhimu wa kutumia kinga, faida za kupima afya na kutumia dawa za kufubaza ugonjwa huu. Na pia hasara na madhara yatokanayo na ugonjwa huu kwa Taifa na mwisho aliwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika vituo vya Afya na hospitalini kupima ili kujua afya zao. Mkutano huu ulifanyika tarehe 9/03/2013.
Mkutano wa aina hii ulifanyika katika Kata ya Amani tarehe 10/3/2013 ambapo wananchi wa kata hii walikusanyika katika Kijiji cha Mlesa kwa ajili ya mkutano ambao maudhui yake ilikuwa kuwahimiza kutumia mabaraza ya usuluhishi ngazi ya vijiji na kata ili kupata suluhu ya migogoro inayojitokeza miongoni mwao.
Hivyo kilichofanyika katika kata ya Mbomole ndicho kilifanyika katika kata ya Amani. Aidha kupitia mikutano hii Sakale Development Foundation waligawa vipeperushi mbalimbali vyenye ufafanuzi mbalimbali kuhusu maswala ya sheria, utawala bora, ugonjwa wa kifua kikuu na UKIMWI.
Kutokana na mvua kubwa kunyesha katika Tarafa ya Amani mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika tarehe 11/3/2013 katika Kata ya Kisiwani uliahirishwa.Lakini ulikuja kufanyika tarehe 13/32013 siku ambayo katika ratiba ya awali ilikuwa ndio siku ya mwisho ya kufanya mikutano na wananchi. Katika mkutano huu, pia ilifanyika kama ilivyofanyika kata zilizotangulia.
Tarehe 14/3/2013 mkutano wa hadhara ulifanyika katika kata za Misalai katika kijiji cha Mgambo na hoja zilikuwa ni zilezile zilizojadiliwa katika mikutano ya kata za Mbomole, Amani na Kisiwani.
Tarehe 17/3/2013 mkutano wa hadhara ulifanyika katika kata za Zirai ambapo makutano yalikuwa katika Kijiji cha Vungwe. Kama ilivyokuwa ikifanyika kata zilizotangulia na hapa ilifanyika hivyohivyo. Huu ulikuwa ndio mkutano wa mwisho wa hadhara na wananchi.
Baadhi ya wananchi walioshiriki mkutano wa hadhara
UFUATILIAJI NA TATHIMINI
Shughuli hii ililenga katika kuona ufanisi wa shughuli na matokeo mazuri ya mradi huu, hapa tuliangalia kama shughuli zinaenda kwa kadri ya mpango uliowekwa.
Taarifa ya ufuatiliaji na tathmini itaonesha hali ilivyo katika eneo hili. Kwani kulifanyika ufuatiliaji wa marakwa mara baada ya mafunzo na kisha ufuatiliaji baada ya mikutano ya hadhara na wananchi.
MAFANIKIO YALIYOFIKIWA
- Mradi umefanikiwa kuwapatia mafunzo wajumbe wote 115 wa mabaraza ya usuluhishi ngazi ya vijiji na Kata wa kutoka kata za Mbomole, Amani, Zirai, Kisiwani na Misalai Wilayani Muheza.
- Mradi umefanikiwa kununua na kugawa nakala 115 za miongozo ya utendaji kazi wa mabaraza.
- Mradi umefanikiwa kufanya mikutano ya hadhara mitano katika kata zote 5 za mradi (kila kata mkutano mmoja).
- Mradi umefanikiwa kuyatembelea na kuona utendaji kazi wa mabaraza ya usuluhishi katika kata.
- Mradi umefanikiwa pia kutoa elimu juu ya UKIMWI kwa wajumbe na wananchi wa kata za mradi.
Mafanikio mengine ni pamoja na ushirikiano na wadau wengine katika kufanikisha shughuli za mradi huu, ambapo asasi ilishirikiana na wadau wafuatao;-
- Maafisa watendaji kata wa kutokakata za mradi ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kutupatia orodha sahihi za wajumbe wa mabaraza ya usuluhishi ngazi ya vijiji na Kata.
- Viongozi wa dini wa kutoka katika kata za mradi ambao shughuli yao kubwa ilikuwa ni kushawishi na kuhamasisha waumini wao kutumia mabaraza ya usuluhishi wakati wa kutatua migogoro baina yao ili kudumisha amani na utulivu katika maeneo yao.
- Vyombo vya habari kama magazeti ya majira, mwananchi na ITV kwa
kutangazana kuandika habari juu ya mradi huu.
- Idadi ya mashauri yanayofunguliwa katika mabaraza ya usuluhishii ngazi ya vijiji na kata imeongezeka kutoka mashauri 547 ya mwaka 2012 hadi mashauri 1,863 ya mwaka 2013 hii inathibitisha kwamba wananchi wameona umuhimu na faida za kutumia mabaraza ya usuluhishi ngazi ya vijiji na kata.
CHANGAMOTO
Wakati wa utekelezaji mradi huu kulikuwa/jitokeza changamoto mbalimbali kama zifuatazo;-
- Madiwaniwa kutoka kata za mradi walihitaji kuhakikishiwa posho, malipo ya ushiriki wao katika kushiriki uzinduzi wa shughuli za mradi, wakati asasi ilikuwa haina bajeti juu ya Madiwani hao.
- Kupanda kwa gharama za bei ya vyumba vya kulala washiriki wa mafunzo kutoka Tshs. 10,000/= tuliyokuwa tumepanga katika bajeti yetu hadi Tshs. 12,000/=.
- Hali ya hewa/mvua kubwa kunyesha katika maeneo ya mradi wakati wa kuendesha mikutano ya hadhara kwa wanavijiji.
NAMNA TULIVYOKABILI CHANGAMOTO
Changamoto namba 1, tuliwafahamisha Madiwani kwamba hakukuwa na fungu la kuwahudumia wao na kwamba asasi imefanya kazi ambayo ilipaswa kufanywa na Halmashauri ambayo wao ndio wahusika, kwa kuwa wanadai hawana fedha asasi inawasaidia kwa hiyo wanapaswa kushukuru na kushiriki bila kinyongo wala kudai malipo. Madiwani hawakushiriki katika uzinduzi wa mradi kwa kuambiwa ukweli huo.
Changamoto No.2, kutokana na hali hiyo asasi iliamua kumpatia kila mshiriki malipo kwa mujibu wa bajeti iliyokuwepo ili ajitafutie mwenyewe mahala pa kulala badala ya asasi kulipa moja kwa moja katika nyumba ya wageni/ Guest.
Changamoto No.3, ililazimisha Asasi kuendesha mikutano bila ya kuzingatia ratiba iliyopangwa awali na hivyo kufanikisha mikutano yote kufanyika.
HITIMISHO.
Kupitia utekelezaji wa mradi huu Sakale Development Foundation imejifunza mambo mbalimbali kutoka kwa wananchi lakini pia kutoka kwa watu wenye dhamana ya uongozi na utendaji katika mamlaka ya chini na kati katika eneo la mradi kwa maana ya vijiji, Kata, Tarafa na Wilaya.
Kwa kiasi fulani zipo mamlaka nyingine zinatumia vibaya mamlaka yake mfano Maafisa watendaji wa kata wamekuwa wakitumia nafasi zao katika kuingilia utendaji kazi wa mabaraza ya usuluhishi jambo ambalo lilikuwa linadhoofisha mamlaka na uwezo wa kiutendaji wa chombo hiki muhimu.
Tunategemea baada ya mradi huu kutekelezwa na wakati wa ufuatiliaji tumeona tabia ya Maafisa Watendaji kata kwa sasa imebadilika na kuyaacha huru mabaraza ya usuluhishi, tunaamini hali hiyo ikiendelea kuwa hivyo mabaraza ya usuluhishi yataendelea kuwa kimbilio la wanyonge katika kutatua migogoro miongoni mwa jamii.
Aidha tunalishukuru Shirika la The Foundation for Civil Society kwa kuufadhili mradi huu muhimu ambao umesaidia na utaendelea kuisaidia jamii katika kipindi kirefu mbele.
INTREPRENEURSHIP & BEEKEEPING
BEEKEEPING PROJECT IMPLEMENTATION REPORT FOR 30 YOUTHS IN MBOMOLE WARD OF MUHEZA DISTRICT DECEMBER 2014 |
REPORT OF THE ACTIVITIES IMPLEMENTED
INTRODUCTION
Beekeeping and entrepreneurship skills project was implemented by Sakale Development Foundation, the project involved 30 from Mbomole ward in Muheza District. ILO through The Foundation forCivil Society funded the project where a sum of 15,838,900 Tsh was given as project fund
The project is to establish businesses based on biodiversity conservation. It involves training in entrepreneurship skills and beekeeping. The project is to impact skills which will enable the establishment of businesses (self-employment) utilizing locally available free natural resources there by avoiding huge capital requirements.
The project passed through various implementation stages, it is through those stages where the expected outcomes of the project had to be seen/ revealed:
The expected results were:
- 30 young beneficiaries who have started beekeeping have appropriate knowledge and entrepreneurship skills
- 30 businesses of beekeeping established with proper supervision and backstopping
- 180 Jobs created through 30 beekeeping business
The indicators of expected result where:
- establishment of businesses
- increasing in number of youths who conducted beekeeping
The project targeted group was 30 youth from Mbomole ward
ACTIVITIES CONDUCTED / IMPLEMENTED
- OPENING OF AND BEGINNING OF TRAINING COURSE
The forest officer of Muheza district Mr. IssaMsumari opened the training course on 4/10/2013 where in his speech he insisted that there are terms and condition which must be proper decision which will have positive effects in the future
Terms and conditions he mentioned were:
- To consider opinions and various perceptions before reaching conclusion
- To find proper way of implementing before reaching proper decision
- Process of making decision
- Important states in making decision
- Proper speculation of decision intended to be reached
- To make innovative decision
- mindset changing
- He also insisted on collection of information for purpose of delivering decisions by considering important stages, bringing new thoughts through critical as well as proper uses of ways for bringing thought. He also suggested various challenges which faces youth in making decisions.
- Lastly, he insisted that youths are responsible to decide on how their future life will be in economic, social, political and educational aspects
The forest officer of Muheza district Mr. IssaMsumari opened the training course on 4/10/2013
Also during the opening of the course, village leaders promised to cooperate with SADEF as well as targeted group (youths) in order to success / reach the project objectives
FOREST OFFICER PHOTO WITH MBOMOE WARD LEADERS IN Y2Y PROJECT OPENING DAY
2: ENTERPRENEUR TRAINING COURSETO 30 YOUTHS
The training course began course letting trainees making guidelines that will be used throughout five days of the course. Also trainees and facilitator together suggested a time table for everyday of the course.
Thereafter, facilitator mentioned topics which will be presented to trainees in those five days
The topics were:
- reason for starting businesses
- qualities of a successful business man/ woman
- business plan
- license and tax payment procedures
- market
- business management and leadership
(A PHOTOGRAPHY SHOWING TRAINEES AT THE ENTERPRENEURSHIP TRAINING)
Y2Y PARTICIPANT IN ENTERPRENEURSHIP TRAINING COURSE
- BEEKEEPING TRAINING COURSE
During training course, participants learned various things related to beekeeping by considering the following factors
- Types of bees
- Characteristics of beekeeping farm
- Equipment which are used in beekeeping activity
- Modern ways of beekeeping activity
- Factors to be taken into consideration in harvesting, preserving and packaging of quality honey
FACILITATOR SHOWS TO TRAINEES THE WAY OF MAKING BEEWAX AND HOW TO USEBEEWAX.
BEEKEEPING TRAINING FACILITATOR SHOWING TRAINEES HOW TO USE BEEKEEPING UNIFORM
(A PHOTOGRAPHY SHOWING Y2Y BEEKEEPING TRAINEES AT THE BEE SITE FOR PRACTICAL LEARNING)
BEEKEEPING FACILITATOR WITH Y2Y TRAINEES IN SITE VISITING)
- LINKING YOUTHS WITH FINANCIAL INSTITUTIONS
After the training course being delivered , youths were able to be linked or connected to financial institution for the purpose of acquiring loans so as to get capital for beekeeping activity.
Those financial institutions includes MUHEZA VIJANA SACCOS and Youth Self Employment Foundation (YOSEFO).
- BUSINESS BACKTOPPING :
Beekeeping expert from Amani forest nature reserve together with officers from Sakale Development Foundation visited youths beekeepers for the purpose of observing their progress as well as giving them advice and consultation so as to improve their beekeeping activities.
- MONITORING AND EVALUATION:
This activity aimed at observing directly what was going on and whether the activities carried out adhere to strategic plan and project mission
Monitoring and evaluation not only helped to correct various matters had to weaken implementation of the project but also reach/ meet the expected outcomes of the project.
(VARIOUS PHOTOS OF “MONITORING AND EVALUATION EVENT”)
JULIA JOHN Y2Y BENEFICIARY IN PICTURE TAKEN INTO HER NEW OFFICE OF TAILORING, THIS WAS A RESULT OF PARTICIPATING IN INTERPRENEURSHIP TRAINING ORGANISED BY SAKALE DEVELOPMENT FOUNDATION.
THIS PICTURE WERE TAKEN IN KWEMWEWE VILLAGE SHOWS THE BENEFICIARY OF Y2Y PROJECT WHO RECEIVE BEEKEEPING TRAINING, HERE SHE PREPARE BEEWAX.
KWEMWEWE Y2Y BENEFICIARIES IN PICTURE, THESE ARE THE NINE BEEHIVES THEY BOUGHT FOR THEIR PROJECT.
BENEFICIARY OF Y2Y PROJECT FROM SKIMU VILLAGE IN SITE LOOKING FOR THE BEEHIVE.
PICTURE OF BEEHIVES IN SITE, TAKEN AT SAKALE VILLAGE WERE BENEFICIARIES OF Y2Y PROJECT ARE DEALING WITH BEEKEEPING. (it is dangerous to reach near the area without the beekeepers uniform that’s why group of beneficiaries were not shown)
PROJECT SUCCESSFUL STORIES:
- The project gave beekeeping training course to 30 youths from Mbomole ward
- The project enabled youths from Mbomole ward to form five groups of beekeepers which are still doing beekeeping activity.
- The project attracted many villagers from Amani divisionto engage in beekeeping, where four (4) groups o beekeepers from neighboring wards (Misalai, Zirai and Amani) were formed
- The project enable to youths to start their own tailoring business after attending entrepreneurship training course
- Kwemwewe village government gave youth a plot of land for conducting beekeeping activity
- Three groups out of five formed are in the final procedures/ process of acquiring loan from “MuhezaVijanaSaccos” for the purpose of buying beekeeping tools/ equipment like beehives etc.
- The project led to linkage of youth with their village government
Other successful stories include:
- Good cooperation (socialization) with various development stakeholders like village chairman and village executive offices of Mbomole ward for their mutual support to ensure that the project objectives are attained
- Forest and bee department of Muheza district for tirelessly consultations from our youths
- Muheza district council which gave 100 bee hives as their mutual support to join hands with the youths
LESSON LEARNT
We as SADEF through the implementation of this project we have learned various matters from the youths and society as whole. The lessons we have learnt were;
- there is the number of opportunities out there ( in our society ) but most of us either by knowing or by being lazy in thinking fall to discover/ recognize and utilize them for our betterment and community as whole.
- It is higher time now for our leaders and community as whole to recognize that problems are important part towards attainment of development so long as we have working on them to find better solutions, here we should take/ consider problems as opportunity
CHALLENGES
- Poor infrastructure (roads), during monitoring and evaluation , poor infrastructure posed a threat for us to reach some area where beekeeping was taking place.
- Presence of few SACCOS (financial institutions) in the area of project delayed the acquirements of loan to youth at Mbomole ward
- Difficult terms and condition applied for acquiring loan contributed to delays in buying beehives and other equipment
- Shortage of beekeeping uniforms hindered practical training, only few trainers had uniforms
CONCLUSION
SADEF calls for government, NGOs and Intellectuals to work on changing people’s mindset towards life challenges (problems) and that people should take their problems as an important part in bringing economic, social, cultural and political changes.
This project gained much support from the community of Amani division; this is due to the fact that there is shortage of land for agricultural activities at Amani because a large part of the land is being preserved as “natural reserve” and presence of big plantation of tea. Therefore we believe, by cooperating with society other stakeholders we will continue promoting the society to work hard.