Ongezeko la idadi ya shule katka jamii linapaswa kwenda sambamba na ongezeko la ubora wa huduma kwa watoto. Ukubwa wa tatizo la waalimu linaweza kukwamisha kwa kiasi kikubwa ufanisi wa sera na mipango ya maendeleo ya kielimu. Tunashauri serikali iboreshe mazingira ya walimu kwa kuwapatia makazi na huduma za kijamii ktk maeneo ya shule wanazopangiwa ili waweze kubaki vituoni. Kwa mtazamo wetu, chanzo cha uhaba wa walimu wa sayansi ni mazingira mabovu ktk shule za serikali kwani ktk shule za sekta binafsi hakuna uhaba huu kwa mujibu wa tafiti mbali mbali zilizofanywa. Inaonekana shule za serikali zinaongoza kwa kukosa waalimu wa masino ya sayansi kwani wengi wanakimbilia huko ambako wanapata huduma bora na kuwa na furaha kyk kazi zao. Ikumbukwe kuwa lengo la maazimio ya mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania ni mwanachama ni kuhakikisha kila binafamu anapata elimu stahiki na si kuongeza idadi ya wanafunzi tu.
Mwisho shirika linatoa wito kwa wazazi kuona umuhimu wa kuwakarimu waalimu wapya ili waweze kujisikia vizuri wawapo kwenye jamii zao. Tunaomba tuwaunge mkono vijana hawa ili waweze kutufundishia vijana wetu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI TEMOA.
↧