Kuwa mjasiriamali wa Jamii (Be social entrepreneur).
Mara nyingi utakutana na vijana wengi wakitafuta kazi au wakisema wanataka kuanzisha biashara na miradi mbalimbali ila swali la muhimu la kujiuliza ni wito wa kufanya kazi au kuwa wafanyabiashara? Jibu lake halisi ni kuwa wamekosa kipto cha kujikimu, wamechoka kuwategemezi kwa familiaa zao, au kipato chao cha saasa hakiwatoshi, na maamuzi haya huwapata tu wanapo jiuliza swali hili "Nitapata pesa wapi za kunitosheleza?” na huamua kutafuka kazi za kuajiriwa, jitolea au kuanzisha biashara mbalimbali, Naamini kila mmoja anatamani kuishi maisha ya utoshelevu kwa kila kitu. “Ni mara ngapi unapohisi kwamba huna pesa za kutosha?”
Toka nilipopata maono ya kuanzisha Asasi ya PDPR na kufanikiwa kuendesha miradi kadha kiufanisi iliyonijengea jina ndani na njee ya nchi, Nikaanza kupokea barua zaidi ya 4 kwa siku za maombi ya kujitole (Volunteerism) kila muombaji niliyemuuliza kwanini ameamua kuchukua maamuzi hayo Majibu yake yalikuwa ni Hana kazi ya kufanya asubuhi hadi jioni, Anahitaji kipato au kipato cha ziada, anahitaji uzoefu na kuna wengine walikuwa na saababu zenye msingi kama za kuleta mabadiriko katika jamii yao kwa kutumia muda wao wa ziada au mapumziko. Sasa wewe toka uhitimu masomo yako umepata ajira, nafasi ya kujitolea au kuutumia ujizi wako kujiingizia kipato? Lahasha kama bado waweza ambatana nasi na utakuwa sehemu ya mabadiliko na watu wa mfano na kujivunia katika jamii yako.
PDPR ikaona ni vyema kuitumia rasirimali hii inayotafuta ajira, kipato na nafasi za kujitolea kuijengea uwezo na ikafanye miujiza kokote itakako kuwa si tu kuwapa nafasi ya kijitolea (Volunteer) bali kuwapa ujuzi, stadi na mbiu za kuiwezesha jamii kijikwamua na umasikini huku nao wakijiiingizia kiato. Ndipo ilipo anzisha WING OF CHANGES CAMPAIGN na SOCIAL ENTERPRENEUR INCUBATOR PROGRAM.
Wing of changes Campaign - hii ni kampeni inayofanywa na rafiki wa PDPR kwa ajiri yaa kusaidia miradi ya PDPR na jamii inayoizunguka, pia inasaidia upatikanaji wa fursa mbalimbali za kujitole, ajira, kulea, kuendeleza, kuwezesha, kufadhili na kuzamini hii inafanyawa sana na marafiki, wanaojitolea a washirrika waliopo njee za nchi.
Social Entrepreneur Incubator Program– ni mradi uliobuniwa kuwaendeleza vijana wa kitanzania wanaohitimu elimu ya sekondari na vyuo kuweza kuziona, kuvumbua, thubutu kuzitumia fursa mbalimbali zinazowazunguka hasa za kijamii, Matatizo na changamoto ni fursa kwa mtu mwenye ujuzi unaozitatua, PDPR inatoa elimu, mafunzo, ujuzi kwa walengwa na baada ya hapo inawaweka kambini na kuwapa stadi zingine za kuwawezesha kutimiza ndoto zao za kuisaidia jamii na wao kujikwamua kiuchumi na kisha kila wahusika wawili hadi watano wanapewa vitendea kazi na kuanza kutekeleza shughuli mbali mbali za kijamii wakisaidiwa na PDPR kwa mwaka mmoja kwa kupata mahitaji ya kimradi. Mradi huu sasa kila mwezi unasajiri zaidi ya watu 10 walio jitoa kuitumikia jamii. Je vifaa, gharama za kuendesha zinatoka wapi? Zinatoka katika mradi wa Wing of Changes Campaign. Walengwa wote walio tayari wanasaidiwa kuanzisha asasi zao, vyama vya kijamii, vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa, vikundi vya kiuchumi, kupata mafunzo ya utengenezaji bidhaa za kijasiriamali kama batiki, vikoi, sabuni, mishumaa, ushonaji. PDPR kwa sasa inashirikiana na Msazi community Organization ya Malawi kupitia Mkurugenzi wake Hastings Phiri wa Mzimba kutafuta fursa mpya na masoko wa mradi huu. Wanufaikaji wanapewa cheti, kitambulisho, vitendea kazi na wanunganishwa na wa bia wa maendeleo wa PDPR.
Fursa zipi za kijamii zinapewa kipaumbele kwa sasa?
1) Mobile ICT training,
2) Kuwajengea uwezo wakulima juu ya kilimo cha kisasa, ujasiriamali, utunzaji wa kumbukumbu.
3) Kuwaelimisha vijana juu ya HIV/AIDS, kilimo, ufugaji kuku na fursa za kibiashaa na uwekezaji.
4) Nishati endelevu, (Renewable energy) tuna wabia wetu wanfundisha utengenezaji wa wind turbine, biogas, nk.
5) Kilimo cha matunda, mbogaamboga, usindika naa ufungashaji.
6) Utengenezaji wa mashine ndogo ndogo kupitia PDPR Development center.
7) Kusaidia uanzishwaji wa SACCOSS, VICOBA, makampuni NK.
8) kuwasaidia kuanzisha mradi wa uchimbaji wa visima vya maji na ufugaji wa kuku na samaki.
Wabia wa mradi huu ni kampuni ya MABOMA, Tanzania care, ARUPA, wafadhili wa mradi ni wanachama wa WING OF CHANGES CAMPAIGN.
“Anza leo kutaka kufanikiwa na kesho bado utajishangaa mwenyewe ukisha fanikiwa”
Karibu sana uwe sehemu ya mabadiliko.
Mfunzo na huduma zinatolewa bure.
MRADI WA KUVIJENGEA UWEZO VIKUNDI VYA KIUCHUMI
PRETTY DEVELOPMENT FOR POVERTY REDUCTION (PDPR).
S.L.P 430, Njombe. Simu: 0754397178, 0652556833,
Barua pepe: pdprngo@gmil.com,Tovuti:www.envaya.org/pdpr
Utangulizi
Pretty Development for Poverty Reduction (PDPR) ni Asasi ya kiraia isiyotengeneza faida yenye dhumuni la kuikomboa jamii ya Vijijini kuepukana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kushirikiana na wabia mbalimbali wenye malengo yanayoendana na yake wa ndani na njee ya nchi. PDPR Imesjiliwa na kupata No. 000NGO/006208 toka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
PDPR – inatekeleza mradi kuvijengea uwezo vikundi vya kijamii na kiuchumi katika mkoa wa Njombe, Mbeya, Ruvuma, Rukwa na Iringa , morogoro, Kilimanjaro na katavi.
kwa kutoa mafunzo ya ujasiriamali, biashara, kilimo endelevu, uongozi, ufugaji wa kuku, samaki, mikopo ya vifaranga vya kuku, vitotozi, mizinga ya nyuki, mashine za kuchomelea, kufyatulia tofari na wauauza vitabu na miche ya matunda mbalimbali.
HUDUMA.
1) Kifaranga kimoja kinauzwa kati ya Tsh 1,500 hadi 3500/=
2) Incubator (Vitotozi). PDPR inauza na kukopesha vitotozi vya mafuta na umeme manual na automatic. Kuanzia mayai 30 hadi 4000/=
3) Welding mashine(kuchomelea) 450,000/=
4) Mashine ya tofari 450,000=
5) Mzinga wa nyuki 28,000/=
6) Vifaranga vya samaki vinauzwa kwa Tsh: 200/=
8) Miche ya kisasa ya parachichi, embe, machunga yanauzwa kwa mia 2500 inazaa ndani ya miaka mitatu.
Vikundi vyote vinavyohitaji egg Incubator, mizinga, mashine za kuchomela, vifaranga vya samaki vitapokea ndani ya wiki 2 baada ya kujaza fomu na kulipa malipo. Na vitawajibika kulipa ada ya 15000/= kwa ajili ya mafunzo, vitabu, ushauri elekezi kwa miezi 12.
VIGEZO VYA KUKOPA NA TARATIBU.
1) Kikundi/mtu ajaze fomu na alipe malipo ya awali walau 40% ya bei ya bidhaa yake.
2) Kiwe na cheti cha cha usajiri wa BRELA, Halmashauri ya wilaya, au barua ya serikali za kijiji na katiba au mwongozo wa uongozi.
3) Vikundi vikubali kutengeneza mtandao wao wa vikundi vitano au zaidi.
5) Vikundi viwe tayari kukaguliwa, kuchunguzwa na kutoa taarifa za ziada itakapo bidi.
6) Malipo yote makubwa yafanyike Bank au M-Pesa
PDPR – itaweza kujitambulisha kwa wabia/wafadhili wake kupitia kikundi chenu.
Sasa mikopo inatolewa na kwa watu binafsi.
“Kuwa sehemu ya madadiliko na PDPR, Jikomboe sasa mwainchi”
TAARIFA ZA VIKUNDI KWA AJIRI YA MIKOPO YA VIFAA
Jina …………………………………..Annuani ………………… ………………………..
Tarehe ya Kuanzishwa ………………No ya usajiri ………………….
Idadi ya wanachama ……………….. Viongozi ………………………
Dhumuni la kuanzishwa kikundi …………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
Shuguli za kikundi …………………………………………………………………………
Mwenyekiti wa kikundi ……………………….. …Simu…………………Sahihi……….
Katibu …………………..........................................Simu …………………Sahihi………
Mhazini ……………………………………………Simu …………………Sahihi………
Mlezi .……………………………………………..Simu …………………Sahihi………
Mali za kikundi …………………………………………………………………………….
Gharama ya deni …………. mdai……………………………………………………….
Kiasi Bank …………Tasilimu …………Wanachama wanaodaiwa idadi……kiasi………
Kikundi kidhamini……………………………….Annuani…………………………
Mwenyekiti …………………………………Simu ……………………Sahihi …………
Katibu …………………………..………… Simu……………………..Sahhi………….
Malengo ya kikundi ya miaka miwili..……………………….…… …………… ………. ……………………………………………………………………………………………...
Mhanitaji kopo wa Vifaa/mashine…………………………………………………………
Mnaweza kulipa kianzio ndiyo/hapana ……….
Mtahitaji mkopo wa fedha shingapi? …………… kwa ajiri ya …………………………..
Wanakikundi wanakikundi wanaujuzi gani? ………………………………………………
Wana elimu juu ya mradi wanao ombea mkopo? ………………………………………….
ZINGATIA
Kikundi kiambatanishe kati ya cheti cha usajiri wa BRELA, Halmashauri, au barua ya mwenyekiti wa kijiji na kitongoji yalipo makao makuu ya kikundi/sehemu ya kukutania.
Fomu na barua zote zigongwe mhuri.
Malipo yote yafanyike Bank ya CRDB Mabibo Hostel Branch, A/C No: 0152275186800, Jina: Pretty Development for Poverty Reduction (PDPR) au kwa M-Pesa 0754397178 na watunze SMS kwa ajiri ya kuchukulia receipt na kumumbuku.
MRADI WA KUPUNGUZA UMASIKINI MAENEO YA VIJIJINI
PRETTY DEVELOPMENT FOR POVERTY REDUCTION (PDPR).
P.O.BOX 430, NJOMBE. SIMU: 0754397178 / 0652556833
E-Mail: pdprngo@gmail.com / isalingwa@gmail.com . www.envaya.org/pdpr
Maswali muhimu ya kujiuliza kwa mtu anayetaka kufanikiwa mjasiriamali
1) Mafanikio ni kwa bahati au uchaguzi?
2) Mafanikio kwa kanuni au neema?
3) Mafanikio kwa bahati au kufanya kazi kwa bidii?
Ndani ya somo hili tutajifunza kwa undani juu ya –
1) Vyanzo vya umasikini wako/kushindwa kwako.
2) Fursa mpya za kiuchumi na kuzitumia kujikomboa na umasikini.
“Mafanikio huandaliwa na kila mtu ni wa tofauti na amezaliwa kuleta utofauti”
“Huwezi kuwa mfanyabiashara mpaka umiliki biashara na huwezi kuwa mjasiriamali mpaka uwe mbunifu na uthubutu kwa tahadhari kutengeneza faida kubwa”
UTANGULIZI WA UJASIRIAMALI.
Ujasiriamali- ni uwezo wa mtu kuona, kugundua, kuvumbua fursa mbali mbali za kiuchumi na kuziongezea ubunifu ama thamani kwa kuziwekea utofauti kisha kuthubutu na kuzifanya fursa kwa lengo la kutengeneza faida/kipato.
a) uwezo wa kugundua, kuona na vumbua
b) fursa za kiuchumi (kilimo, elimu, biashara, utamaduni)
c) kuziongezea thamani kwa kuongeza ubunifu (ubunifu ktk vionjoo, ufungashaji, masoko)
d) uthubutu wa kufanya kwa tahadhari (kuanza na mtaji/uzalishaji mdogo ukilenga wateja wengi)
e) Tengeneza faida kubwa (maximize profit)
AINA ZA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI.
1) Mafunzo ya taaluma nzima ya ujasiriamali.
2) Mafunzo ya kanuni ya miradi ya kijasiriamali (kutengeneza sabuni ya magadi, ushonaji, ufugaji).
MWANZO WA UJASIRIAMALI:
1) Wazo mahususi(specific idea).Linalo kidhi mahitaji ya jamii(linatatua matatizo ya jamii)
2) Utafiti (ukubwa wa soko na bei“market share”, tabia za wateja, kipato cha wateja namna ya uzalishaji, gharama za uzalishaji, washindani, sehemu ya biashara “location”)
3) Malengo na Mipango (plan) (jinsi ya kuzalisha, wakati, mahali, kupata soko, kupanga bei, kukuza mradi)
4) Mchanganuo ni taarifa zote zinazo hususiana na mradi zinaweza kuwa nzuri au mbaya).
5) Mtaji (watu, fedha, ujuzi, umaarufu)
6) Weka ubunifu (innovation) utofauti (katika) masoko, wazo, ufungashaji, wakati wa uzalishaji).
7) Mwanzo wa mradi.
SIFA ZA MRADI WA KIJSIRIAMALI.
A) Ni endelevu kwa kuwa na mipango na mfumo wa utawala ulio wazi (anakufa mmiliki na si mradi).
B) Unatatua matatizo / changamoto za jaimii.
C) Unatumia rasirimali chache (watu, mtaji, ardhi,muda) na una faida kubwa kwa mapema au mara kwa mara.
D) Unasoko kubwa na ushindani mdogo kutokana na ubunifu, wakati wa uzalishaji au sehemu)
MJASIRIAMALI MZURI (mambo ya kuzingatia)
1) Elimu rasimi na siyo rasimi juu ya mradi.
2) Ujuzi wa mambo utumiaji wa elimu uliyoipata ama uliyo nayo.
3) Huruka ya kupata mafanikio halali. (uthubutu, ubunifu, mvumilivu na jasiri, wepesi wa kuona au kuiga, jitahidi kufanya kazi kwa faida jituma)
4) kujiwekea malengo kila hatua, anashaurika na anabeba majukumu,
5) Nidhamu ya kazi, fedha, rasirimali, kuipenda kazi yake.
6) Hakimbii changamoto.
7) Anatunza kumbu kumbu
8) Kupata taarifa za mradi kila inapo bidi na kufanya tathimini.
9) Amechochewa au mwenye vichocheo vya kuendelea kiuchumi kwa kutafuta njia mpya za kujikwamua au kufanya jambo.
MISINGI YA UJASIRIAMALI.
1) Elimu ya ujasiriamali na kujifunza. Kujifunza mambo tofauti ya miradi yake.
2) Ubunifu na uvumbuzi. Kuingiza bidhaa mpya katika soko na zinazo kidhi matakwa ya jamii.
3) Kukua na kupanuka. Kuwa na mipango ya kuendeleza au kukuza biashara yake kiutawala, bidhaa, huduma au uzalishaji.
4) Kujaribu na kudhamiria. Si mwoga wa kutumia fursa anayo iona.
Kabla ya kuanzisha mradi au kubuni wazo la biashara unapashwa kujiandaa kiakili na hisia kuzifuata ndoto zako na kuifanya kazi utakayo ipenda, kujivunia na kuweza kuizungumzia mbele ya jamii.
MAONO (VISION) Nini? matarajio yako baada ya kutekeleza wazo/mradi wako (future plan).
(MISSION) SABABU-ya kufanya mradi huo na si mingine (statement of purpose) lazima ionyeshe kutatua tatizo au kutumia fursa iliyopo.
MALENGO- ni mambo unayotaka kuyafikia au kuyapata pia unaweza kuweka na wakati.
MFUMO WA MALENGO.
.1) Mahususi (specific) 2) Yanapimika (measurable) 3) Yanafikika na changamoto (attainable and challangable) 3) Uhalisia (realistic) 4) Muda maalumu (time fram)
NJIA ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA.
A) Tumia ujuzi ulionao. Mf, fundi magari anaanzisha gereji yake.
B) Nini kinakosekana mtaani kwako? Kitu kinacho leta usumbufu (haba,hafifu) na kinakuletea kupoteza muda au wakati mwingi. Huduma zipi hazipo mtaani kwako na muhimu? Ni kitu gani,wewe, ndugu,majirani huwa wanakilalamikia sana mtaani kwako?
C) Tumia mabadiliko ya Technologia. M-pesa, online service.
D) Uwepo wa taasisi kubwa au matukio (shule, hospitali, ujenzi, harusi)
E) Kuwa wakala wa bidhaa.
F) Nakili ubunifu wa watu wengine toka sehemu nyingine.
G) Nunua biashara iliyopo.
H) Tumia kipaji chako (ngoma za asili, mziki)
MCHANGANUO WA BIASHARA.
Ni maelezo ya kina yanayohusiana na mradi yanaweza kuwa mazuri au mabaya. Ni taarifa muhimu ya kuwavutia wawekezaji na watoa mikopo kama mabenki.
1) wazo lako ni nini?
2) Utalifanyia wapi?
3) Kwanini umelichagua na kwanini ni hapo? (statement of need)
5) Mbinu, mikakati ya utekelezaji.
6) Faida unayo tegemea.
7) Ukikosea utapataje hasara.
8) Washindani
9) Umahiri wako katika fedha,usimamizi, ujuzi, utawala.
10) Mgawanyo wa ukuaqji wa mradi (soko,walengwa) market segment and target.
Tathimini binafsi (swot analysis).
> Strength (uimala) wanakujua, mtandao.
> Weakens (uzaifu) wako
> Opportunities (fursa zilizopo)
>Threat (vizuizi).
SUMMARY.
|
CHANGAMOTO KWA WAJASIRIAMALI WACHANGA.
1) Uhaba wa mbinu shindani.
2) Uelewa mdogo juu ya stadi za maisha na uhalisia wa maisha.
3) Imani potofu
4) Elimu hafifu juu ya mradi, kuendesha.
5) Uaminifu mdogo.
6) Kulalamika kuliko vuka mipaka.
7) Uhaba wa soko.
8) Vyombo vya usimamizi.
JINSI YA KUPATA MTAJI NA NAMNA YA KUTUMIA.
Mtaji. Ni kitu chochote ambacho unaweza kutumia katika kuzalisha kitu kingine kwa lengo la kupata faida. Biashara yoyote lazima ianze na mtaji.
AINA ZA MTAJI.
- Fani au taaluma fulani.
- Human capital (binadamu mwenyewe). Elimu, ujuzi, na kufanya kazi kwa bidii.
- Mtaji wa fedha (financial capital).
- Jamii (social network capital) kufahamika au ushirikiano.
MBINU ZA KUPATA MTAJI.
Kuna njia mbili za kupata mtaji ambazo zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni chanzo cha ndani na chanzo cha nje.
Chanzo cha ndani (internal sources of capital)
1) uwekaji wa akiba hii ni njia bora. Uwekaji wa akiba ni njia inayoonekana ngumu kwani inahitaji nidhamu ya fedha ya hali ya juu. Hauna budi kujiuliza matumizi ya fedha yako yakoje? Ni yapi yamekuwa matumizi ya msingi na yapi si yansingi? Kwanini usipunguze au kuacha matumizi yasiyo ya msingi. Kaa chini na utafakari juu ya mapato na matumizi yako na angalia ni kwa namna gain unaweza kuweka sehemu ya mapato kama akiba ya mtaji.
2) Kuingia ubia (partinership) ni njia inayowakutanisha watu ambao mahitaji yao yanafanana.
3) Kutoka kwa ndugu wa failia au marafiki.yafaa kutafuta namna bora ya kukaa na ndugu na marafiki ili kuweza kumshawishi ni kwa namna gain akusaidie.
4) mtaji toka kwa mjasiriamali mwenyewe.huu ni mtaji ambao mjasiriamali anakuwanao kabla hujaanza biashara.huu ni mtaji bora sana kwani humilikiwa na mjasiriamali mwenyewe (nyumba, shamba,gari).
5) Mtaji ambao unapatikana wakati biashara inajiendesha. Faida inayopatikana katika biashara au shughuri zingine inaweza kutumika kama mtaji. Njia hii ndio huchangia kukua kwa biashara.
Chanzo cha nje (external sources of capital).
1) Mikopo kutoka taasisi za kifedha au watu binafsi. Yafaa mjasiriamali kujiuliza baadhi ya maswali, lengo kuu la kujiuliza maswali haya ni kuweza kujifanya tathimini kama kweli unahitaji kukuza mtaji kwa njia ya mkopo.
> Swali 1 jiulize, je una malengo gain na fedha unazokopa? Je malengo uliyonayo juu ya mkopo unaoomba yana vihatarishi vipi?
> Swali 2 kujiuliza, je unahitaji kiasi gani cha fedha? Kuna wajasiriamali ambao huenda lakini hawajui wanahitaji kiasi gani, hawajajipanga. Wanachojua wanataka kukopa tu, mambo mengine baadae.
> Swali 3 ni lini hasa unahitaji mkopo huo? Wapo ambao wanakopa kwanza halafu baada ya kupata mkopo ndio wanakaa chini kupanga mipango.
> Swali 4 je unahitaji mkopo huo kwa muda gani?
> Swali 5 na la msingi ni juu ulipwaji wa mkopo, ukiomba mkopo na kupewa je utaulipaje? Je una vyanzo gani vya mapato ambavyo unaweza kuvitumia katika kuhakikisha mkopo unarejeshwa pamoja na garama zake (riba) kwa muda uliopangwa.
> Swali 6 ikiwa mambo yataenda mlama, nini kitafanya mkopo ubaki salama? Hapa wakopeshaji wengi huhitaji dhamana za mkopo (collateral) ili kuweza kulinda mkopo uliotolewa ili ubaki salama, kulipika.
2) kupewa zawadi.
ANDIKO LA MRADI.
Ni maelezo yanayoelezea mradi husika kwa kujibu maswali ya vihatarishi vya mradi, fursa zilizopo, rasilimali na jinsi zitakavyo tumika, mpangilio mzima wa kuutekeleza mradi ikiwa ni pamoja na usimamizi, mpango endelevu wa mradi kwa hapo baadaye kwa upande wa kitaasisi na kifedha.
(mradi huo unaitwaje? utakuwa eneo gani? Utafanyika kwa muda gani, garama ya mradi? Wafadhili wa mradi, namba ya mradi kama ipo na kipindi cha kuanza na kumalizika kwa mradi.)
1) majumuisho ya mradi (executive summary) unaelezea tatizo, fursa, malengo, shughuli, matokeo, muda, gharama.
2) Hali iliyopo(current situation).Kwa nini tuwe na mradi huu, kaika eneo hili, na kwa wakati huu?
3) Malengo, lengo kuu na madhumuni ya mradi
4) Shughuli za mradi na utatekelezwaje?. Lazima yapangwe kimantiki na kwa matarajio yenye kufikia lengo.
5) Mahitaji ya mradi. (fedha, mashine, ardhi, watu.)
6) Utawala na tathimini ya mradi (utasimamiwa na nani? Au watu wangapi? na nafasi viashiria vya kufanikia au kushindwa kwa mradi)
7) Mahali na muda wa mradi.
8) Matokeo ya mradi. (faida, kipato, hasara)
MPANGO MKAKATI.
Mpango mkakati ni taarifa iliyoandikwa kwa lugha rahisi kueleweka yenye kuonyesha dira ya taasisi husika na mambo gani yatawekwa kipaumbele katika kipindi cha miaka 3 hadi mitano ijayo. Taarifa ya mpango mkakati ni lazima pia ionyeshe rasilimali fedha, watu na vitu vitakavyotumika kufikia maono au dira
Wakati gani mpango mkakati unatakiwa
Ni pale tu taasisi inapotaka kufukia kwa ufanisi lengo fulani au pale taasisi haifanyi vizuri kwenye matumizi ya muda, fedha, watu na vitu na pia imebainika wazi kuwa malengo hayataweza kufikiwa. Hii inaweza kufahamika tu kama taasisi itaamua kujitathimini.
HATUA ZA KUANDAA MPANGO MKAKATI.
Hatua ya kwanza
A: Uchambuzi yakinifu wa mahitaji
Watumiaji wakuu wa mpango mkakati ni taasisi husika. Kama mshauri na mtaalam unatakiwa kufanya uchambuzi wa mahitaji ya msingi. Katika hili zoezi utagundua hasa wadau wako wanahitaji nini?
Namna ya kufanya uchambuzi
- Kutumia madodoso ili kupata maoni ya wadau wa taasisi
- Vikao vya faragha na viongozi muhimu
- Mkutano na wadau wote
Hatua ya Pili
B: Ukusanyaji wa taarifa/takwimu na kazi katika vikundi
Kutengeneza Maono, Wito, Malengo mahsusi, Maadili ya msingi, viashiria vya ufanisi, Tadhimini nk Kazi hii itafanywa kupitia uwezehswaji na kazi za vikundi
Hatua ya Tatu
C: Kuandika Rasimu ya Mpango Mkakati
Kazi hii ili iende haraka inatakiwa kuandikwa na mtaalamu kwa kutumia taarifa zilizopatikana kutoka kwa wahusika wenyewe
WATEJA WANATAKA NINI KUTOKA KWA WAFANYA BIASHARA?
1) wanahitaji suluhusho la matatizo yao,yaani wapate kile wanachokihitaji na ndicho kile kinacho waleta kwako.
2) Wanataka kuona unawaona maalumu. (SPECIAL).
a) Speed and time (jali muda wa mteja wako)
b) Personal interaction with customer (shirikiana na mteja wako katika mambo ya kibiashara, mpaka anakuwa huru)
c) Expectation. (timiza matarajio ya mteja wako kwa kumpa huduma anazohitaji)
d) Courtency and competence (acha ubabaishaji, jua unacho fanya)
e) Information and keeping the customer informed. (wape taalifa)
f) Attitude and customer liason (jua tabia za wateja wako na ujue namna ya kuishi nao).
g) Long term relationships (tengeneza uhusiano wa muda mrefu na wateja wako)
KWANINI UNAPOTEZA WATEJA.
1) Unapokuwa huwajali.
2) Unapowadanganya.
3) Kutoa lugha chafu.
4) Unapokuwa hupatikani eneo la biashara mara kwa mara.
5) Usipowasikiliza wateja.
6) Bidhaa au huduma duni.
7) Bei zisizo eleweka,.
8) Bei kubwa.
MAMBO YA KUKUSAIDIA KUKUZA NA KUBORESHA BIASHARA.
1) Fikiria changamoto za biashara unayofanya na tafuta namna ya kutatua kasoro hizo.kila biashara ina matatizo yake, kama utakuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto hizo basi ni heri kwako.
2) Kama una mtaji mkubwa, tengeneza mpango wa kupanua biashara yako.kwa kufanya utafiti wapi usogeze huduma kwa wateja wako kwa kuweka ktk sehemu utakayopata wateja wengi.
3) Jenga mawazo mengi ya namna ya kukuza biashara yako.weka bidhaa/huduma mpya ambazo zitawavutia wateja kwani wanahitaji vitu vipya kila siku.
4) Tafakari na ujue kama unahitaji msaada wa kifedha. Mpango wa kibiashara unahitaji fedha,unapaswa kujiuliza je unahitaji mkopo?, je unahitaji kiasi gani cha fedha?, je wewe binafsi tayari una kiasi gani cha kukuwezesha kufanya biashara uliyopanga?,
5) Jenga madhari m,azuri ya biashara yako.(usafi,utulivu,vifaa).
6) Hakikisha wafanyakazi/wasaidizi wako wana ujuzi wa kazi wanazofanya.
VITU VYA MASOKO (MARKETING TOOLS)
1) Bidhaa/huduma (product) inayokidhi mahitaji ya jamii.Ubora (quality), Sifa au wasifu (Feature), Jina (Brand name), ufungashaiji (packing), Kipimo (size), huduma (service).
2) Bei (price). Punguzo la bei (discount), Muda wa malipo (payment period), masharti ya mkopo (credit terms), allowance (motisha).
3) Mahali (Distribution place). Wateja wanapenda bidhaa nyingi iwepo karibu na walipo. Njia ya usambazaji (chanel of distribution), Ukubwa wa eneo (coverage), usafiri, inventory (akiba ya bidhaa), mahali (location).
4) Ukuzaji wa soko (promotion). Matangazo (Advertising), Personal selling (watu wa mauzo), Machapisho(publicity),Ukuzaji mauzo(sales promotion “free goods,after sale services, sample, )
NJIA ZA KUPANGA BEI.
1) Gharama za uzalishaji/manuuzi (unaweza jumlisha asilimia 10 hadi 25k ama faida katika gharama).
2) Bei za washindani wako.
3) Uhitaji uliopo (Demand). Kutegemeana na aia ya uhitaji wa bidhaa/ huduma uliopo sokoni kama ni mkubwa kuliko kiasi kilichopo sokoni (supply).
TABIA ZA WATEJA ZINATEGEMEA.
1) Utamaduni wa eneo alilopo.
2) Jamii aliyopo (social).Watu/makundi aliyonayo karibu/kumshauri.(kazini,familia,daraja alilopo)
3) Mtu mwenyewe(personal factors). Umri,kazi,kipato,mfumo wa maisha.
4) Psychological factors. Mtazamo,vichocheo, mwitiko, maono.
NJIA ZA KUONGEZA FAIDA.
1) Kuzalisha kwa wingi.
2) Kutumia technologia rahisi.
3) Kuuza kwa mtindo wa aina ya uhitaji wa bidhaa kama ni wa muhimu au si wamuhimu.
4) Kupunguza gharama zisizo muhimu.
5) Weka ubunifu na kuwa wakipekee (monopoly)
MAMBO YANAYOWEZA KUKUFANYA KUWA MBUNIFU.
1) Ondoa uwoga. Usiogope kuwa wazo lako litakuja kushindwa.
2) Usijilinganishe na watu wengine waliokutangulia au wenye mafanikio.
3) Zingatia upekee. Upekee utakuletea maana katika ubunifu wako, angalia wengine kwa kujifunza na kuona mapungufu yao na si kwa lengo la kufanya kama wao.
4) Zingatia kukidhi mahitaji ya binadamu. Ubunifu wako hautakuwa na maana kama haukidhi mahitaji ya binadamu; Hivyo njia rahisi ya kuanza ubunifu ni kuisoma jamii, kuangalia matatizo yanayoikabili.
MFUMO RASMI WA UENDESHAJI BIASHARA.
Unahusisha kusajiri jina la biashara na umiliki wake kama kampuni (business name and ownership)
11) Miongoni mwa faida za mfumo rasmi wa uendeshaji biashara ni kuwa na mfumo rasmi wa kiutawala na uliowazi na utunzaji wa kumbukumbu za kimahesabu.
12) Usalama wake mkubwa.
13) Ukuaji wake ni mzuri (mikopo).
14) Urefu wa uhai wake ni mkubwa.
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UANZISHAJI WA BIASHARA.
A) Bidhaa/huduma unayotaka kuuza upatikanaji wake
B) Idadi ya washindani
C) Matakwa ya wateja katika eneo husika na idadi yao.
D) Gharama za uendeshaji wa biashara husika.
E) Taratibu za ulipaji ada/kodi
F) Hali ya hewa,utulivu na mwenendo wa maisha ya wakazi.
MISINGI YA UJASIRIAMALI.
- Elimu ya ujasiriamali na kujifunza. (elimu rasmi na sirasimi) Vitendo na nadharia.
- Ubunifu na uvumbuzi (kuboresha utendaji wake).
- Kukua na kupanuka. (kimaslahi,kimtaji,kiutendaji,kimahusiano,mipango).
- Kujaribu na kudhamiria. (anaona fursa na kutathimini) sio muoga.
MAENEO YA KUTENGENEZA MTANDAO KWA MJASIRIAMALI.
A) Washindani wako (ushindani sio uadui,mshindani wako anaweza kuzidiwa na oda akakuletea wateja).
B) Vyombo vya habari, fahamiana na watu wanomiliki au kufanya kazi katika vyombo hivyo.
C) Kuwa sehemu ya jamii, kwa kuhudhuria sherehe na matamasha na kutumia fursa hizo kujijenga.
AINA YA BIASHARA UNAZOWEZA KUZIANZISHA BIRA YA KUWA NA MTAJI / MTAJI KIDOGO SANA.
Watu wengi hujiona hawana chakufanya kinacho weza kuwaingizia fedha kwani hamini mwanzo wa biashara yeyote ni mtaji fedha (financial capital) kitu ambacho si kweli kwani aina nyingine za mutaji tulizo ziona zinaweza kuchukua nafasi kubwa katika uanzishaji na ustawi wa biashara, hasa ukijikita katika utoaji wa huduma (service) ni rahisi sana kufikia lengo lako la kutengeneza fedha nzuri tena kwa muda mfupi.
1) Kuwa wakala wa bidhaa /huduma mbali mbali. Kwa miaka ya sasa kutokana na soko huria kumekuwepo na makampuni ya kigeni yakitafuta watu wa ndani ya nchi wawasaidie kuuza bidhaa zao pia kuna makampuni ya ndani yamekuwa yakihitaji mawakala wa mikoani na wilayani wa kuwasaidia kuwafikia wateja nafasi ni yako sasa.
2) Uandishi wa makala, Vipeperushi, Stori na Move script. Katika maisha yetu ya kila siku kuna vitu vingi vinatokea na hivyo unaweza kuviweka katika mfumo unao elewaka na kivutia na kuuanda na kuwapelekea wazailishaji wa majarida na magazeti au wamiliki wa mitandao ya kijamii na unaweza ukauza kwa bei ndogo kwa mara ya kwanza na baadae ukala matunda yako.
3) Huduma za kuandika michanganuo ya biashara (business plan) na Andiko la mradi (project proposal). Kuna wafanyabiashara wengi hawajui uandishi wa mchanganuo wa biashara na wanapotaka kwenda kukopa hurazimika kuwatafuta watalaamu wa kuwasaidia pia kuna utitili wa Asasi za kiraia na vyama vya kijamii vinavyoanzishwa kila siku na havina watalaamu wa kuandika Maandiko ya miradi na kulazimika kuwatafuta watu wa njee kuwasaidia kazi hiyo.
4) Mshauri wa mambo ya biashara. Kuna makampuni yalianza kwa mtaji wa wanachama tu wenye utaalamu wa biashara na mpaka sasa yamekuwa makubwa na yanafanya kazi ya kushauri mambo ya biashara na hutengeneza fedha nyingi kwani hulipwa kwa mwezi au kwa kazi fulani.
5) Mshauri ya masoko. Wafanyabiashara wengi wahajui kitu gani kinahitajika sokoni na kwa bei gani pia hawajui njia za kuwafikia wateja walengwa (potential buyer) na namna ya kukidhi mahitaji yao ili waweze kupata soko na kulimiliki na litumike kuingizia huduma nyingine na wao hutumia watu wenye ujuzi huo kuwafanyia utafiti na maamuzi.
6) Kutoa huduma ya kuandaa na kuendesha matukio (Event management) kuna makampuni/mashirika yanayoanya sherehe, warsha na mikutano mbali mbali amabyo huhitaji watu wa njee kuandaa au kuleta (supply) bidhaa mbali mbali kama mziki, vinywaji na chakura.
7) Kuandaa vitabu vya mahesabu. Wafanya biashara na kampuni ndogo ndogo hazina utalaamu wa kuandaa vitabu vya kila siku na mwisho wa mwaka na unaweza kufanya kazi hiyo kwa mkataba.
8) Kuanzisha tovuti / blog kwa huduma tofauti. Nchini Nigeria kuna watu wanaendesha maisha kwa kumiliki tovuti ambazo zimekuwa zikipata ufadhili kutoka katika mashirika tofauti hata hapa Tanzania zipo Blog zenye ufadhili maka Mjengwa, Issa michuzi NK.
9) Kutafiti fursa mpya za biashara. Kuna watu wana fedha hawajui wafanyie nini ila wanamalengo ya kuwekeza au kupanua biashara zao.Unaweza ukawauzia wazo lako la biashara(business idea)
10) Kutoa huduma ya kuandikisha majina ya kampuni, Asasi, SACCOS NK. Kama unazijua hatua za kufuata kuandikisha majina ya biashara unaweza kuifanya kazi hii na kutengeneza faida.
MAKASHABRASHA NA MENGINEYO.
Ujasiriamalii ni stadi kama stadi zingine na ni muhimu kuwa na taaluma yake kwa mtu yeyote haijarishi upo katika fani ipi na uwekeza au umeajiliwa, kwani hata mfanyakazi unapaswa unapaswa kuwa na malengo yako ya kujiendeleza kiuchumi au kuboresha. Kwani mfanyakazi mutimiza malengo na maono ya mwajiri wake japo hulipwa ujira ambayo inaweza kuwa ni hatua moja ya kuelekea katika kujiajiri kama utaweza kuweka akiba na kuanzisha kitega uchumi kinacho tengeneza faida inayo rudisha gharama za uendeshaji (fixed cost & variable cost) na faida kubaki ambayo inaweza kujumuishwa katika mtaji na kuwekezwa tena na kuzarisha faida nyingine.
Watalamu wengi wanashauri kutenga zaidi ya asilimia 40% kwa ajiri ya kuwekeza katika biashara. Na wanapengekeza kuweka (save) kabla ya matumizi hi ni njia ya kwanza inayoweza kukusaidia kupata kiasi ulicho kuwa una malengo nacho kwa ajiri ya kuwekeza au kukuza mtaji wa biashara yako.
FAIDA ZA KUZALISHA KWA WINGI
1) Gharama za masaoko hupungua 2) Muda 3) Usafiri 4) Matumizi ya technologia ya kisasa 6) Matangazo 7) Vibarua mishahara 8) Uhifadhi 9) Soko la jumla
NITAJIKOMBOAJE NA UMASIKINI ?
Umasikini ni hali ya kushindwa kupata mahitaji yako yote muhimu au kupata kwa kiasi kidogo.
1) Jiulizee kwanza wewe nani? Kijana, mlezi, mzee, au mzazii
2) Nataka kuwa nani kiuchumi au kijamii? kasha tafuta mtu wa mfano wako (role model)
3) Kuwa na hulka ya kufanikiwa (shauku au nia ya dhati)
4) Jifunze vitu mbalimbali na tafuta taarifa zaidi na na shirikisha wengine juu ya wazo lako.
5) Anza kufanya unavyoweza katika mazingira yako na mtaji au ujuzi ulio nao.
6) Jitathimini na ona udhaifu wako na changamoto zilizopo badilisha kuona kwako na buni tena upya.
7) Itafute fursa mpya nyingine ichunguze na uitumie nayo kiubunifu kutengeneza kipato.
8) Simamia mauzo na rasilimali zote vizuri na Panua miradi yako.
UJASIRIAMALI NI MAMBO 7
1) Wazo mahususi 2) Rasiriimali (Taarifa, ujuzi, ardhi, pesa na watu) 3) Ubunifu (Utofauti) 4 ) Fursa (Uhitaji, miundimbinu, wateja, matatizo katika jamii, mazingira yako) 5) Fanya 6) Mawasiliano (Lunga nzuri na ushirikiano na jamii) 7) Ona matokeo makubwa.
SABABU ZA KUTOFANIKIWA.
1) Uvivu (Wafanya kazi wa wastani, wasiofanyakazi, wavivu, wafanya kazi kwa bidii)
2) Mawazo yasiyosahihi au mtazamo hasi 3) Kuiga kwa watu wengine (Kila mtu wa kipekee) 4)kutosheka na hali uliyonayo au kushindwa na kukata tamaa.
5) Ujinga wa vipawa na uwezo wa vitu unavyoweza kuvifanya (Karama).
6) Ukosefu wa maandalizi na mafundisho sahihi 7) kukosa nguvu ya maamuzi
7) Kufanya kitu siosahihi, mahali siosahihi, wakati siosahihi na watu sahihi.
8) Kutegemewa kuajiriwa na si kujiajiri 9) Mipango mibaya (Ukishindwa kupanga umepnga kushindwa)
PRETTY DEVELOPMENT FOR POVERTY REDUCTION (PDPR).
S.L.P 430, Njombe. Simu: 0754397178, 0652556833,
Barua pepe: pdprngo@gmil.com,Tovuti:www.pdprngo.blogspot.com
UFUGAJI BORA WA KUKU (mradi wa kupunguza umasikini)
Idadi ya wanyama wanaofugwa kwa chakula imezidi ile ya binadamu zaidi ya mara mbili kote ulimwenguni. Kuna maelfu ya wanyama kote duniani ilihali ni wachache tu wanaoweza kufugwa. Kati ya hawa wanyama, ni aina nne (Ng'ombe, kondoo, mbuzi na kuku) wanaochukua asilimia 95% ya wanyama wote wanaofugwa. Wanyama hawa hupatikana katika nchi za hari kwenye nyanda za chini. Lakini kati ya mifugo hawa, kuku ni maarufu katika nchi za hari na hata kote ulimwenguni.
Lengo la makala haya ni kutoa maelezo ili kusaidia wafugaji wa kiwango kidogo katika nchi zinazostawi, katika kupunguza umaskini. Sehemu ya kwanza (I) itatoa maelezo kuhusu ufugaji na hasa ufugaji wa kuku, Sehemu ya pili (II) itaangazia maswala yafuatayo katika kuinua hali ya uchumi kwa kufuga kuku:
1. Kuendeleza ufugaji wa kuku za kienyeji kwa kutumia njia zisizohitaji gharama nyingi.
2. Kutafuta mbinu na njia muafaka za kuzalisha viwango vya kuku bora kwa njia ya kiasili.
3. Matumizi ya njia za kiasili au zile zisizo gharimu pesa nyingi kutibu na kuzuia magonjwa ya kuku.
SEHEMU YA I: MAELEZO KUHUSU UFUGAJI WA KUKU KATIKA NCHI
ZINAZOENDELEA
NAFASI YA MIFUGO
Licha ya kukosa mashamba makubwa ya kuendeleza ufugaji wa ng'ombe, jamii nyingi katika nchi za hari (tropics) hupata nafasi ya kufuga kuku kwa kiwango kidogo. Idadi ya wanyama wanaofugwa huongezeka sambamba na ile ya watu. Idadi ya watu inapoongezeka ndipo ile ya mifugo huzidi. Idadi kubwa ya watu huhitaji chakula kingi na matumizi huongezeka, hivyo basi watu hufanya bidii kuzalisha chakula na mapato kutoka kwa shamba.
Ufugaji wa ng'ombe na wanyama wanaohitaji lishe kwa wingi huhitaji kiasi kikubwa cha shamba ili kupanda mimea na lishe la mifugo. Ukilinganisha na ufugaji wa kuku, utahitaji mabaki ya vyakula na sehemu ndogo ya shamba. Ufugaji wa kuku umeweza kunawiri hata pasipo fedha.
Katika nchi za hari ufugaji wa kienyeji hautahitaji kazi nyingi, kazi hii hufanywa na akina mama na watoto. Kwa kawaida katika nchi hizi kazi nyingi za nyumbani hutekelezwa na mama. Vyakula vya kuku vyaweza kutoka kwa: 1) Mabaki ya chakula, 2) Mabaki ya mimea, 3) Mabaki kutoka jikoni na 4) Vyakula vya kujitafutia (kwa mfano kwekwe, mbegu, wadudu, nyongonyongo, n.k). Mfumo wa kufuga kuku kwa njia ya kienyeji hutumia viungo vinavyopatikana kwa urahisi na kuimarisha hali ya kiuchumi na chakula bora kwa jamii. Ni muhimu sana kufuga mifugo hata ikiwa ni kwa kiwango kidogo kwa sababu ya 1) Chakula bora na kuongeza mapato ya jamii kwa viwango vya kuridhisha; 2) Mifugo ni hakiba au banki, faida yake huzaana tu kama riba ya benki; 3) Mifugo yaweza kuuzwa ili kugharamia karo ya wanafunzi, malipo ya hospitali, gharama nyingine za nyumbani na hata shambani; 4) Kwa matumizi ya kijamii (kwa mfano kulipia mahari, shughuli za kidini, n.k); 5) Mifugo husaidia katika kukabili wadudu,
kwekwe na kuimarisha rutuba kutokana na mbolea ya kinyesi. Ni bayana kwamba mifugo ni muhimu sana kwa mkulima yeyote yule.
UMUHIMU WA UFUGAJI WA NJIA YA KIENYEJI
Ufugaji wa kuku katika nchi zinazostawi waweza kugawanywa mara mbili: 1) Ufugaji wa kitamaduni au kienyeji pasipo kuwepo gharama, na 2) Ufugaji wa kisasa unaohitaji fedha nyingi. Ufugaji wa viwango vikubwa kwa kuzingatia mfumo wa kisasa ni maarufu katika kuzalisha kuku wa nyama na wale wa mayai. Mfumo huu hujumuisha asilimia ndogo sana ya aina ya ufugaji. Itafahamika kwamba mfumo wa kisasa haujaadhiri ule wa kienyeji. Idadi kubwa ya watu katika nchi za hari hutegemea mfumo wa kienyeji kwa nyama na mayai. Mfumo wa kisasa huhitaji pesa nyingi za kununua vyakula vya kuku. Aidha mfumo wa kisasa huhitaji kazi nyingi ili kutekeleza. Mfumo wa kisasa
umefaulu katika nchi zilizostawi kutokana na hali nzuri ya kiuchumi katika kuzalisha (kuku wa hali ya juu, kuangua vifaranga kwa stima, vyakula vilivyo na madini mengi, vifaa na zana za mashine, utaalamu wa hali ya juu n.k). Haitafaa sana kuanzisha mfumo kama huu katika vijiji vya mataifa yanayostawi. "Mageuzi" katika ufugaji (kuambatanisha mfumo wa kisasa pamoja na ule wa kienyeji) yamefanyiwa majaribio katika mataifa yanayostawi tangu miaka ya 1950. Matokeo ya kuku wapatao 200 hadi 300 kwa shamba moja hayajawai kufaulu. Hasara imepatikana na waweza kuona nyumba zilizokuwa na kuku bila chochote, pesa nyingi zimepotea na kuku hawapo.
Mfumo wa kienyeji ni bora (Katika hali ya kiuchumi) iwapo idadi ya kuku haitazidi kuku 50. Ni rahisi kuweza kuwatunza kuku, kwani hakuna gharama nyingi. Iwapo vyakula au zana za kisasa zitanunuliwa, basi haitakuwa kwa viwango vikubwa. Mazao ya nyama na mayai yataleta faida. Sehemu nyingi katika mataifa yanayostawi hakuna stima, katika nchi za hari, ufugaji kwa kiwango kidogo umeweza kufaulu na kuimarisha uchumi.
FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU KWA NJIA YA KIENYEJI
Faida za uzalishaji kuku ili kuimarisha uchumi kwa njia hii zimepuuzwa na viongozi na wafadhili. Kuku huleta faida kwa jamii kama tulivyoona katika sehemu ya I. Zaidi ya hayo, ufugaji wa kuku waweza kuimarishwa pasipo gharama nyingi ukilinganisha na mifugo wengine.
- · Hutupatia fedha kwa kuuza nyama na mayai
- · Mayai ni chakula kilicho na madini muhimu na kisicho ghali katika soko lolote. (madini kama methionine na cystine), madini haya ni muhimu sana kwa afya ya watu hasa watoto wachanga. Pia hutupatia protini.
- · Kinyesi cha kuku ni mbolea safi
- · Kiwanda asilia cha kutotoa vifaranga
- · Gharama za kuanzisha na kuendeleza ni nyepesi
- · Kitoweo chepesi na rahisi kwa wageni, kitoweo hakihitaji hifadhi hutumika mlo mmoja au miwili na kumalizika
- · Jogoo hutumika kama saa inapowika
- · Manyoya ya kuku hutumika kutengenezwa mapambo mbalimbali, mito na magodoro
- · Kuku wanahisimu wadudu waharibifu
Kuku ndiye mnyama wa kipekee anayeweza kuishi mahali popote hapa ulimwenguni bila kuadhiriwa na viwango vya hali ya hewa. Ufugaji wa kuku ndio shughuli inayofanyika kwa wingi duniani kuliko ufugaji wa aina yeyote. Kuku hunawiri vyema katika nchi za hari kutokana na uwiano uliopatikana wakati wa mwanzo binadamu alipofuga Asian jungle fowl aina ya kuku-mwitu. Mayai pia yaweza kuhifadhiwa kwa urahisi na huchukua nafasi ndogo kuliko aina ya bidhaa zozote za mifugo. Mayai yaweza kuwekwa mahali kwa muda mrefu bila kuhitaji barafu. Hautahitaji kuhifadhi kuku kwa njia yoyote, kwani nyama yake hupatikana pale unapohitaji kwa kuchinja.
Upungufu wa kuku wa kigeni ukilinganisha na wale wa kienyeji ni kama ufuatao:
• Kuku wa kigeni hawawezi kukalia na kuangua mayai, hivyo basi wahitajika kununua vifaranga (gharama);
• Vifaranga wa kigeni huhitaji utunzaji maalum na vyakula maalum (gharama);
• Kuku waliozalishwa kwa njia ya kisasa huhitaji chakula kingi ili kutaga mayai (gharama);
• Kuku wa kisasa huhitaji zaidi kuchanjwa dhidi ya magonjwa (gharama)ukilinganisha na wa kienyeji (japo nao huhitaji chanjo);
• Kuku wa kutaga mayai huhitaji mwangaza wa stima (saa 14 kwa siku) ili kutaga mayai (gharama)
Kwa kuongezea, rangi ya nyama na mayai ya kuku wa kienyeji huvutia kuliko ile ya kuku wa kisasa.
Hivyo basi jaribu kuendeleza na kuhimiza ufugaji wa kuku za kienyeji.
Iwapo mkulima ana jogoo mmoja na kuku kumi na mbili, basi kila mwezi waweza kupata kuku akikalia mayai 10-12 kwa mwezi (mayai yote kwa wakati mwingi hayataanguliwa) kuna hakikisho la kupata vifaranga vinne kila mwezi. Kuku mzima atachukua miezi minne kuchunga vifaranga walioanguliwa. Kwa hivyo, kati ya kuku wote kumi na mbili kila mara kutakuwa na kuku wane wakitunza vifaranga, huku wale wengine wanane wakitaga mayai.
Kuku waliofugwa kwa njia ya kitamaduni hupata vyakula vyao kwa kutafuta mbegu, wadudunyongonyongo, n.k; Lakini kuku hawa hukosa vyakula vya kutosha vilivyo na nguvu ili waweze kutaga mayai. Vyakula vya kutoa nguvu daima huwa ni haba.
Waweza kuwalisha kuku kwa nafaka ili wapate chakula cha nguvu (mfano kilo moja ya nafaka iliyopondwa kila siku kwa kuku 10), nafaka hii yapaswa kuwa kavu. Vifaranga wapewe kiasi kidogo cha nafaka au mchele wiki za kwanza. Kuku wanaolishwa nafaka baada ya kujitafutia chakula nje huongeza idadi ya mayai (kutoka asilimia 20-25% hadi 40-50%). Kuna umuhimu wa kuhifadhi nafaka kama lishe badala ya kuuza kwani utapata mayai mengi ambayo baadaye utaweza kuuza.
Hautahitaji kununua vyakula vya protini kwani kuku hujitafutia lishe la protini.
Ikiwa hauna nafaka, waweza kutumia vyakula vya mzizi au ndizi. Vyakula vya aina hii hata hivyo, huwatatiza kuku wanapovitonogoa, kiwango cha mayai sio kikubwa kama cha wale wanaolishwa nafaka.
Kwa kuwalisha kuku kwa nafaka utapata hakikisho la mayai manne kwa siku kutoka kwa wale kuku wanane. Iwapo hakuna nafaka, kati ya kuku wanane wanaotaga utapata mayai mawili tu kwa siku.
Ni bora kutumia nafaka hii kama lishe kuliko kuuza na hatimaye kununua vyakula vya dukani.
Kuku kumi na mbili na jogoo mmoja wanaolishwa kwa kilo moja ya nafaka kila siku waweza kuelezwa hivi:
• Waweza kuuza kuku wanne kila mwezi na kujaza pengo hilo na wale vifaranga (vifaranga wanne huanguliwa kila mwezi) na
• Dazani kumi za mayai kila mwezi (mayai manne kila siku).
Kwa mwaka mmoja waweza kukadiri ile faida utakayopata na vile hali ya kiuchumi yaweza kuinuliwa katika mataifa yanayostawi.
Hata hivyo faida hii haitaafikiwa iwapo magonjwa hayatazuiwa au kukabiliwa kama ifuatavyo.
TEKELEZA UTARATIBU WA KUZUIA MAGONJWA
Magonjwa ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko kuponya. Kinga yaweza kutolewa mara kwa mara (kila baada ya miezi mitatu) dhidi ya magonjwa
yafuatayo:
Ugonjwa wa Newcastle
Ugonjwa huu ndio huadhiri kuku na kusababisha hasara katika nchi za hari. Virusi vya ugonjwa huu huenea kwa kasi na rahisi kiasi cha kusababisha vifo kwa asilimia 100%. Dalili za kwanza ni shida ya kupumua na kung'amua hewa, sauti kama ya kikohozi na kutokwa mate. Kinyesi chaweza kuwa na rangi ya kijani kibichi. Hadi sasa hakuna dawa.
Waweza kuzuia ugonjwa huu kwa kutoa chanjo. Dawa za chanjo hupatikana kote ulimwenguni hata katika nchi za hari kwenye vipimo vya vitone mia moja. Madawa haya yaweza kuhifadhiwa kwa muda. Waweza kuweka kwa wiki moja mbali na jua au joto kali (Chanjo hii ni ya kipekee, kwani aina nyingine ya chanjo huwekwa kwa friji). Waweza kutoa chanjo kwa kutia vitone kwenye mdomo. Kuku wote (wakubwa kwa wadogo) wapaswa kupewa chanjo baada ya kila miezi mitatu.
Minyoo
Minyoo kama chango (roundworms) na tegu (tapeworms) huadhiri kuku wa kienyeji. Kuku hukosa hamu ya chakula, mayai hupungua na magonjwa mengine hushambulia. Ni bora basi kutoa minyoo.
Mchanganyiko wa madawa ya aina tatu ndio hutumiwa kuangamiza minyoo, madawa haya ni piperazine, phenothiazine na butynorate. Madawa haya hupatikana kama vidonge (tumia kidonge 1 kwa kuku mzima na 1/2 kwa vifaranga). Iwapo hautapata dawa hii, waweza kutumia Panacur au dawa nyingine ya kuangamiza minyoo. Wapatie kuku dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu.
Wadudu
Wadudu kama chawa au utitiri husumbua kuku katika ufugaji wa kienyeji. Chawa au utitiri husababisha harara ya ngozi, kuku walio adhiriwa hupata shida na kukosa usingizi. Hali hii hupunguza kiwango cha mayai na uzito wa kuku.
Tumia asilimia 5% ya unga wa malathion kwa kupulizia kuku (puliza kwa chupa uliyo toboa mashimo) pulizia kila kuku ili kuzuia chawa na utitiri (kilo moja ya unga huu yaweza kutibu kuku 150). Pulizia dawa hii baada ya kila miezi mitatu, waweza kupuliza kwa wakati mmoja wa kutoa chanjo na dawa zilizotajwa hapo juu. Puliza unga huu pia kwenye viota vya kuangulia mayai. Waweza kutayarisha 5% ya malathion kwa kuchanganya 25% ya unga wa malathion (kiwango cha kilimo) na sehemu nne za jivu kutoka jikoni.
Magonjwa ya mapafu
Magonjwa ya mapafu huadhiri njia inayopitisha hewa na kuambatanisha mate na sauti kama ya kikohozi. Ugonjwa huu huenea polepole. Uambukizanaji pia hutokea kwa polepole na vifo sio kwa wingi. Hata hivyo, kutaga mayai na uzito hupungua. Shida hii yaweza kusambaa hata kutoka mahali vifaranga huanguliwa hadi pale walipouzwa.
Tylosin19 ndio dawa inayoweza kutibu magonjwa ya mapafu. Kiasi cha 35mg ya tylosin hutosha kuku mmoja (kiwango hiki hufaa kuku na hata vifaranga) dawa hii husimamisha madhara kutokana na magonjwa ya mapafu. Tibu kuku kila baada ya miezi mitatu, waweza kutekeleza kwa wakati
mmoja wa kutoa kinga na kuangamiza minyoo. Tylosin hupatikana kwa pakiti ndogo ya 4gm. Waweza kutayarisha dawa hii kwa kutumia maji na 35gm ya tylosin (gramu nne kwa vikombe viwili vya maji), kiasi hiki chaweza kutolewa kwa vitone kwa kila kuku.
KWA UFUPI (SUMMARY)
Kabila za Kuku Si rahisi kupata kabila halisi (pure breed) au kizazi halisi (pure line) za kuku wa kienyeji kutokana na mwingiliano wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao. Lakini hata hivyo baadhi ya kuku wa kienyeji wanaweza kutambuliwa kutokana na maumbile yao kwa mfano
1. Kuchi
- Warefuna wenye kusimama mgongo ukiwa wima
- Wana manyoya machache mwilini na vilemba vyao ni vidogo
- Majogoo huwa na wastani wa kilo 2.5 na mitetea kilo 1.8
- Mayai gram 45
2. Ching'wekwe (Umbo dogo)
- Hupatikana zaidi Morogoro na umasaini
- Majogoo kilo 1.6
- Mitetea kilo 1.2
- Yai gram 37
- kuku hawa wanafaa sana kwa biashara ya mayai kwa kuwa hutaga mayai mengi sana.
3. Umbo la Kati
- Majogoo kilo 1.9
- Mitetea kilo 1.1
- Mayai gramu 43
- Hukua upesi na hupata kinga upesi baada ya kuwachanja dhidi ya ugonjwa wa Mdondo (New Castle)
4. Singamagazi
- Hupatikana zaidi Tabora
- Majogoo wana rangi ya moto na mitetea rangi ya nyuki
- Majogoo kilo 2.9
- Mitetea kilo 2
- Mayai gramu 56
5. Mbeya
- Wanapatikana Ileje Mbeya na asili yao ni Malawi
- Mjogoo kilo 3
- Mitetea kilo 2
- Mayai gramu 49
- Uwezo wao wa kuatamia mayai na kuangua ni mdogo sana ukilinganisha na kuku wengine
6. Pemba
- Maumbo ya wastani na miili myembamba
- majogoo kilo 1.5
- mitetea kilo 1
- mayai gramu 42
7. Unguja
- Hawatofautiani sana na wa Pemba
- Vilemba vyake ni mchanganyiko- vidogo an vikubwa
- Majogoo kilo 1.6
- Mitetea kilo 1.2
- Mayai gramu 42
SIFA WA KUKU WA KIENYEJI
- Wastahimilivu wa Magonjwa
- Wana uwezo wa kujitafutia chakula
- Huatamia, kutotoa na kulea vifaranga
- Wanastahimili mazingira magumu(ukame, baridi n.k)
- Nyama yake ina ladha nzuri
KATIKA KUWAENDELEZA KUKU WA KIENYEJI NI VYEMA
- Wajengewe nyumba bora
- Wapewe kinga dhidi ya ugonjwa wa Mdondo (New Castle), Ndui (Fowl Pox) pamoja na kinga ya minyoo.
- Malezi bora ya vifaranga
- Kuwapatia chakula cha ziada pamoja na maji ya kunywa ya kutosha.
NYUMBA BORA
Eneo inapojengwa nyumba au banda la kuku liwe
- Linafikika kwa urahisi
- Limeinuka juu pasituame maji
- Pasiwe na pepo zinazovuma
Vifaa kama miti, nyasi, makuti, fito, udongo mabanzi ya miti, cement, mabati n.k
Sifa za Nyumba Bora ya Kuku
- Paa imara lisilovuja
- Kuta zisiwe na nyufa
- Sakafu isiwe na nyufa
- Madirisha ya kutosha kupitisha hewa
- Iwe na mlango wa kuingia kufanya usafi
- Iwe na ukubwa (nafasi) unaolingana na idadi ya kuku. Wastani wa kuku 10-15 kwa mita moja mraba
Mambo muhimu ndani ya nyumba
- Chaga za kulalia kuku
- Sakafu iwekwe maranda (wood shavings), makapi ya mpunga, n.k
- Viota vya kutagia mayai sentimita 35x35x35 na idadi ya viota iwe nusu ya idadi ya kuku waliofikia hatua ya kutaga na viwekwe sehemu iliyojificha (faragha)
UATAMIAJI WA MAYAI
Kuna njia 2
- Njia ya kubuni (incubators)
- Asili
Kumuandaa kuku anayeatamia
- Weka maranda au majani makavu ndani ya kiota
- Anapokaribia kuatamia toa mayai ndani ya kiota pamoja na maranda, hakikisha mikono haina manukato
- Nyunyiza dawa ya kuua wadudu (viroboto, utitiri n.k) ndani ya kiota, pia mnyunyizie dawa kuku anayetarajia kulalia mayai
- Rudisha mayai kwenye kiota ili kuku aanze kuatamia
- Kwa kawaida kuku hulalia mayai yake kwa muda wa siku 21 ndipo huanguliwa
ULEAJI WA VIFARANGA
Kuna njia mbili
- Njia ya kubuni
- Njia ya asili
Njia ya ASILI
Kuku mwenyewe hutembea na vifaranga akivisaidia kutafuta chakula. Ni vizuri kumtenga kuku mwenye vifaranga katika chumba chake pekee ili vifaranga wasishambuliwe na kuku wengine hali kadhalika kuwalinda na wanyama na ndege wanaoshambulia vifaranga.
Njia ya KUBUNI
Vifaranga huwekwa kwa pamoja kwenye chumba maalum na kupatiwa joto maalum, chakula pamoja na maji. Tumia taa ya kandili (chemli), umeme au jiko la mkaa na hiyo taa iweke kwenye mzingo(mduara) walipo vifaranga. Pia kuna kifaa kinaitwa Kinondoni Brooder ni kizuri kwa kutunzia vifaranga. Kwa kutumia kifaa hiki kuku wanaweza kunyang'anywa vifaranga vyao mara tu baada ya kutotoa na kuviweka kwenye hii brooder na hao kuku wakaachwa bila vifaranga vyao, baada ya majuma matatu au manne, kuku hao huanza tena utagaji na kuendelea na uatamiaji hadi kutotoa tena. Kwa mtindo huu kuku anaweza kutotoa mara 5-6 badala ya kama ilivyo sasa mara 2-3 kwa mwaka. Vifaranga vikae ndani ya brooder majuma 3-4 na baadaye fungua milango ya brooder kuruhusu vifaranga vitoke na kuzungukazunguka chumbani bila kuvitoa nje kw kipindi cha mwezi mmoja au zaidi kutegemeana na mazingira.
KULISHA KUKU WA KIENYEJI
Kuku mkubwa huhitaji gramu 120 za chakula kwa siku, ni vizuri kuku wanaofugwa huria (free range) kupatiwa chakula cha ziada gramu 30 kila siku nyakati za jioni.
Kuku walishwe
- Mizizi-mihogo, viazi vitamu, mbatata, magimbi, n.k
- Nafaka-mahindi, Mpunga, Mtama, Ulezi na Pumba za nafaka zote
- Mboga-Mikundekunde, nyanya, milonge, majani ya mapapai
- Matunda-Mapapai, maembe, n.k
- Mbegu za Mafuta-Karanga, ufuta, mashudu ya pamba, alizeti, n.k
- Unga wa dagaa
- Maji
KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU
- Pumba.............kilo20
- Mashudu ya Pamba n.k...kilo 3
- Dagaa iliyosagwa.........kilo 1
- Unga wa majani uliokaushwa kivulini na kusagwa........kilo 2
- Unga wa Mifupa ..........kilo 0.25
- Chokaa ya mifugo ........kilo 0.25
- Chumvi........................gramu 30
- Vichanganyio/Premix...gramu 25
KUPANDISHA
- Uwiano wa mitetea na jogoo ni mitetea 10-12 kwa jogoo mmoja
- Sifa za mtetea ni mkubwa kiumbo, mtagaji mayai mengi, muatamiaji mzuri na mlezi wa vifaranga
- Sifa za jogoo ni awe mkubwa kiumbo, miguru imara na yenye nguvu, mrefu, upanga/kilemba kikubwa, awe na uwezo wa kuitia chakula mitetea na awe na tabia ya kupenda vifaranga
- Jogoo huanza kupanda akiwa na umri wa miezi 7-10 na kuendelea hadi miaka mitatu na asipande watoto wake
- Mitetea huanza kutaga wakiwa na miezi 6-8
MAGONJWA YA KUKU
1. Mdondo/New castle
Virus vinavyosababisha ugonjwa huu huenezwa kwa hewa
Dalili
- Kuhalisha choo cha kijani na njano
- Kukohoa na kupumua kwa shida
- Kupinda shingo kwa nyuma
- Kuficha kichwa katikati ya miguu
- Kukosa hamu ya kula na kunywa
- Idadi kubwa ya vifo hadi 90%
Kinga
- Chanjo (New Castle vaccine) kwa mpango wa siku 3, wiki 3, miezi 3
- Epuka kuingiza kuku wageni
- Choma au fukie mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa
- Zingatia usafi wa mazingira
NDUIYA KUKU/ FOWL POX
Virus huambukizwa kupitia jeraha au mbu
Dalili
- Vidonda vyenye utando wa kahawia/purple kwenye sehemu zinazoonekana
- Kukosa hamu ya kula
- Vifo vingi
Kinga
- Chanja vifaranga wanapofikia mwezi 1-2 kwa kutumia chanjo ya Fowl pox vaccine
- Epuka kuingiza kuku wageni
- Zingatia usafi wa mazingira
HOMA YA MATUMBO/FOWL TYPHOID
- Kuharisha kinyesi cha kijani na nyeupe
- Kuku hukosa hamu ya kula
- Kuku hukonda
- Vifo hutokea kidogo kidogo kwa muda mrefu
- Kinyeshi hushikamana na manyoya
Tiba
Dawa aina ya antibiotic, sulfa na vitamini
Kinga
- Usafi
- Fukia mizoga
- Usiingize kuku wageni
- Chinja kuku wote mara ugonjwa huu ukiingia na safisha banda, pia pumzika kufuga kwa miezi 6
MAFUA YA KUKU/INFECTIOUS CORYZA
Hutokana na bakitelia na hushambulia hasa kuku wakubwa
Dalili
- Kuvimba uso
- Kamasizilizochanganyikana na usaha unaonuka
- Macho huvimba na kutoa machozi na pengine upofu
- Hukosa hamu ya kula
- Mbawa huchafuka na kutoa harufu mbaya
Tiba
Dawa za Antibiotic, sulfa na vitamini
KUHALISHA DAMU/COCCIDIOSIS
Husababishwa na vijidudu vya Protozoa
Dalili
- Kuharisha damu
- Manyoya husimama
- Hulala na kukosa hamu ya kula
MINYOO
Dalili
- Kunya minyoo
- Hukosa hamu ya kula
- Hukonda au kudumaa
- Wakati mwingine hukohoa
Tiba
Dawa ya minyoo/Pipeazine citrate kila baada ya miezi mitatu
WADUDU
Viroboto, chawa, utitiri
Dalili
- Kujikuna na kujikung'uta
- Manyoya kuwa hafifu
- Rangi ya upanga kuwa hafifu
- Ngozi kuwa nene, ngumu na yenye magamba yanayodondoka kama unga
Kuzuia
- Ziba mipasuko sakafuni na kwenye kuta za banda
- Fagia banda mara mbili kwa wiki
- Nyunyiza majivu au chokaa mara moja kwa wiki mara baada ya kufagia
- Choma masalia ya mayai yaliyoanguliwa
- Nyunyiza dawa kwenye viota
- Weka maranda, majani makavu, makapi ya mpunga ya kutosha sakafuni ndani ya banda la kuku
- Fuata kanuni za chanjo
- Tenga kuku wagonjwa wakae mbali na kuku wazima
UPUNGUFU WA VIINI LISHE KWENYE CHAKULA
Dalili
- Kuku hupungua damu, uzito na kudumaa
- Mifupa huwa laini na kutokuwa imara
- Hutaga mayai yenye gamba laini na madogo
- Huwa na manyoya dhaifu