Umoja wa wazee na maendeleo Tanzania ni muunganiko wa wazee wote wenye umri kuanzia miaka 50 kuendelea wenye makusudi ya pamoja yakusaidiana na kukabiliana na changamoto mpya kabla na baada ya kustaafu.Umoja huu ulianza baada ya kugundua kuwa hakuna taasisi inayotetea maslahi ya wazee hivyo kuwa wapweke na mara kadhaa haki zao nyingi hupotea kwa kuwa hakuna taasisi za kusemea haki zao.
Umoja huu ulianza kama wazo la wazee wachache na baadae kuungwa mkono na wazee wengine na hatimaye kuamua kufanya usajili ili kufanya kazi zao kwa uwazi na zenye nguvu za kisheria. Tangu Februari mwaka 2013 tulipata usajili rasmi kama chama cha kijaamii chenye makusudi ya kutetea na kuinua uchumi wa wazee katika vikundi vyao ya ujasiriamali.
Umoja huu wa wazee ulianza ukiwa na wanachama 58, ila kwa sasa tupo wa wazee 56 wa mkoa wa Dar es Salaam ambapo tunakusudia kuwafikia wazee wengine katika mikoa mingine ili tuunganishe nguvu kwa pamoja kwa kuwa na kauli mbiu moja yenye nguvu na tija kwa taifa.