Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

MWANAMBOGO UNITED YOUTH DEVELOPMENT created a Projects page.

$
0
0

MUYODE - TANGA: YAFANIKIWA KUIFIKIA JAMII KATIKA ELIMU YA MSINGI KWA SHULE YA MSINGI CHOGO NA KWAMDAMI.

Katika utaratibu wa kuhudumia jamii MUYODE imekuwa ikijituma kwa juhudi za pekee na hatimaye matunda yake yameanza kuonekana. Asasi ya MWANAMBOGO UNTED YOUTH DEVELOPMENT (MUYODE) iliingia katika maeneo ya Kabuku ndani na hasa katika vijiji vya CHOGO I, KWANJEDA, CHOGO II, na vijiji vingine vingi vidogo dogo ambavyo viko ndani karibu killometa kumi na zaidi kutoka barabara kuu. MUYODE iliingia kushirikiana na jamii ya hapa tangu mwaka 2010 nainatekeleza mradi wa kujitolea katika shule za msingi Chogo na Kwamdami tangu mwaka 2012 hadi sasa. Mradi huu unaojulikana kama“NIACHIE URITHI WA ELIMU BORA” ni mradi ambao kwa ujumla unatekelezwa kwa kutumia rasilimali zilizopo kwenye Asasi na Shule pamoja na Wadau na Walengwa.

Mnamo tarehe 05/06/2014 MUYODE TAWI LA HANDENI TANGA imetoa taarifa yake ya utekelezaji kwa awamu ya kwanzaili kutathmini kwa kiasi gani wameweza kuifikia jamii kupitia katika Elimu. Kwa kuanzia mradi huu ulianzia kwa shule mbili za msingi kutokana Walimu na kamati za shule hizi zilijitolea na kukubali kushirikianana Asasi pia ilikuwa ni hatua nzuri ilioleta msukumo katika utekelezaji na manufaa kuonekana.

Katika mafanikio ya utekelezaji wa mradi yamepatikana katika taaluma, utoro, michezo, lishe, sera na ushirikishwaji jamii. Shule hizi zimezungukwa na vijiji vingi na zina idadi ya wanafunzi kubwa kidogo kutokana mahitaji ya wananchi wa hapa. Katika Taaluma Shule ya msingi Chogo ilikuwa chini katika ufaulishaji kwa mwaka 2010 ambapo ilikuwa sawa na 56% na sasa mwaka 2014 imefikia 94% kwa mujibu wa matokeo ya darasa la saba ya mwaka 2013. Kwa Shule ya msingi Kwamdami pia ufaulu ulikuwa chini mwaka 2011 ilikuwa 49% na sasa mwaka 2014 ni aslimia 100% kwa mujibu wa matokeo ya darasa la saba ya mwaka 2013.

Pia kupungua idadi ya watoro shuleni kutoka mwaka hadi mwaka. Kwa mfano mwaka 2010 mahudhurio yalikuwa 67% na sasa mwaka 2014 ni 87% kwa shule ya msingi Chogo na mahudhurio ya Kwamdami mwaka 2010 ilikuwa 68% na sasa mwaka 2014 ni 85%. Takwimu hii ya mahudhurio na ufaulu ni kwa mujibu wa taarifa ya Shule za msingi CHOGO na KWAMDAMI.

Katika kufikia hapa haikuwa kazi rahisi bali ilikuwa ni juhudi za pamoja kati Asasi na Walimu wakuu na staafu zao katika kupanga na kubuni mbinu ambazo zimeweza kuleta mabadiliko ambayo ni furaha kwa kila mdau na walengwa wa mradi huu.

Miongoni mwa mambo yalioleta mabadiliko haya ni kupunguza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazozikumba shule hizi. vifaa vya michezo. Pamoja na kuchapa mitihani kwa gharama za Asasi. Pia Walimu kwa kushirikiana na Asasi tukaanzisha upatikanaji wa chakula shuleni hasa kwa darasa la kwanza na la pili kupatiwa uji kila wawapo shuleni na chakula cha mchana kwa shule nzima mara mbili kwa wiki. Hii ilipunguza utoro na afya ya wanafunzi ikaimarika.

MUYODE Imeweza kufanya yafuatayo katika mradi huu;

(a)  Kununua baadhi ya Vitabu vya Shule ambavyo vilionekana kupungua na kuhitajika,

(b)  Vifaa vingine vya Shule kwa lengo la kuimarisha elimu kama vile; Flipchart, Lesson plane, rimu, madaftari, kalamu, makapeni, n.k

(c)  Kushirikiana na shule katika kuchapa mitihani

(d)  Kununua komputa moja kwa shule hizi mbili ili utendaji wa shughuli za shule ziende vyema.

(e)  Kuanzisha program ya kutengeneza T-shirt za shule na kuimarisha mazingira bora ya shule

(f)   Kuanzisha mfumo wa upatikanaji wa chakula shuleni

Arika na taaluma ikapanda. Uchapishaji mitihani nayo pia ilikuwa ni sababu bia ya kufanya vizuri kwa shule hizi.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kwamdami Mr. KADALA na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi CHOGO Bi. SIFAEL MCHARO wanasema “maabadiliko ni makubwa ukilinganisha na kabla shule hizi hazijakuwa marafiki na MUYODE kwani sisi na MUYODE ni marafiki na leo hii tuna mabadiliko haya ingawaje hali bado sio nzuri sana. Juhudi za kuungwa mkono kwa shule zetu bado zinahitajika kwa kila mwenye kuguswa na hili. Na pia tunakabiliwa na matatizo kadhaa ambayo ni pamoja na upungufu kama

(a) Ukosefu wa jiko la kupikia chakula na chumba cha kulia chakula

(b) Upungufu wa matundu ya vyoo kulingana na mahitaji ya wanafunzi na     staafu ya shule.

(c) Upungufu wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia shuleni na

(d) Upatikanaji wa umeme kwa ajili ya kurahisisha utendaji shuleni.

(e) Ukosefu wa Madaftari, Kalamu na hata Sare za Shule kwa watoto yatima,    wanaoishi mazingira magumu na hatarishi

Tunaomba yeyote mwenye kuguswa na hili asaidie ili kuimarisha elimu hasa huku vijijini hali ni mbaya. Muige Asasi hii ya MUYODE kwa juhudi zake binafsi”.

Mwenye kiti wa MUYODE –TANGA ABDULAHI .H. MDEVE anasema “kwa kuwa lengo letu ni kuimarisha jamii katika elimu bora vijijini tukaona kila jambo tushirikiane na makao makuu MUYODE Dar-es- salaam ili kuongeza nguvu za pamoja ili utekelezaji wa mradi uendane na mahitaji yake.

Mwenyekiti ndugu MBERWA wa kijiji cha CHogoI na mtendaji wa kijiji hicho ndugu Habiba walithibitisha utekelezaji wa mradi wa kujitolea unaoendesha na MUYODE na kusema kuwa “ Asasi hii tunashirikiana nayo kwa kila jambo linaloigusa jamii/ wanachi hapa kwetu kijijini na hivi sasa tunatarajia kujenga jingo moja la chekechea hapa kijijini ili kutoa fursa watoto wadogo wasitembee umbali mrefu. Na pia kwa kushirikiana na MUYODE mambo sasa ni ushirikiano na kufanya kazi kama timu”.

Na pia mwenyekiti wa ChogoII Ndugu JABRIL SOMO anasema “mambo ya MUYODE tunayaona na ni furaha kuwa katika vijiji vyetu kwa ufupi imeleta mabadiliko mengi na idadi kubwa na watoto kijijini kwa waliomaliza darasa la saba mwaka 2013 wote wameanza kidato cha nne kwa hakika inatokana na utekelezaji wa mradi wa kujitolea wa MUYODE ujilikanao “NIACHIE URITHI WA ELIMU BORA” kwa shule za msingi kidogo tumepiga hatua lakini hali ni mbaya shule ya sekondari ya Chogo. Ningeomba MUYODE wakaitazama na shule ya sekondari hii”.

Lakini MUYODE imeandaa mpango mkakati amabao unatarajiwa kuzinduliwa na mheshimiwa DR. ABDALAH OMARI KIGODA (MB) na Waziri wa Viwanda na biashara. Uzinduzi wa mpango huu ni hatua ya kipekee itakayo ongeza upanuzi wa kutoa huduma katika kuwafikia wanajamii katika Wilaya ya Handeni ili Wilayah ii iwe na mwamko mkubwa zaidi kielimu. Ni mkakati wa mika mitatu na una kila hali ya kubadilisha mali ya elimu katika vijiji hivi na ni imani yangu kuwa mpango huu unaweza kuwa mwarobaini. Maandalizi yamefikia mwisho katika kufikia uzinduzi na ni imani yetu tutafanikiwa kuifikia jamii, anasema Abdulahi .H. Mdeve mwenyekiti.

Pia mwenyekiti huyo aliwashukuru wananchi ambao waliweza kuunga mkono juhudi zao na hata kufikia hatua ya kuamini kuwa MUYODE ndio mkombozi wa maswala ya kijamii hapa Kijijini.

Kwa mawasiliano zaidi katika kuunga mkono harakati hizi wasiliana

+255 784 286 594 mwenyekiti au kuchangia juhudi hizi akaunti namba ni (MWANAMBOGO UNITED YOUTH DEVELOPMENT A/C 41510003585 National Microfinance Bank- NMB –KOROGWE BRANCH)  


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles