Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Guluka Kwalala Youth Environment Group updated its Projects page.

$
0
0

MRADI WA KUKUZA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA NA KUIMARISHA UADILIFU, UWAJIBIKAJI NA UTAWALA BORA.

Guluka Kwalala Youth Environment Group tarehe 30th March, 2010 kwenye Hotel ya OASIS Mjini Morogoro tuliingia makubaliano na ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma (Idara ya Maadili).

Lengo la makubaliano hayo ni kujenga ushirikiano kati ya Guluka Kwalala Youth Environment Group na OR – MUU Hususani katika ukuzaji wa maadili ya mtumishi wa umma na kuimarisha Uadilifu, uwajibikaji na utawala bora ili wananchi wa Tanzania waweze kuipenda nchi yao wapate huduma zilizo bora.

UTEKELEZAJI WA MAKUBALIANO HAYO:-

MWAKA 2010

v  Tuliendesha Mafunzo katika Kata ya Vikumbulu Wilaya ya Kisarawe. Mafunzo yalilenga kukuza uelewa wa umma kuhusu maadili ya utumishi wa umma mafunzo haya yaliendishwa na mtaalamu kutoka ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma idara ya maadili Ndg. Nassoro Mlandila.

 

MWAKA 2011

Tulitekeleza makubaliano kwa kufanya kazi ya kutoa mafunzo eneo la Sera. Guluka Kwalala wakati tunatekeleza mradi wa kuimarisha utawala bora katika usimamizi wa rasilimali za maliasili, katika kata za Kisarawe, Mafizi, Kurui na Vihingo zilizopo Wilaya ya Kisarawe na Bupu, Shungubweni na Mkamba Wilaya ya Mkuranga. Tuliweza kutoa mafunzo ya kukuza uelewa wa umma kuhusu maadili ya utumishi wa umma. Ili jinsi iweze kupata huduma bora kutoka kwa mtumishi wa umma. Na ushiriki wa wananchi katika kuleta utawala wenye uwazi, unaowajibika na unaojali. Mafunzo haya yalitolewa kwenye kamati za rasilimali za maliasili kwenye hizo kata na jamii inayoizunguka hizo kata.

 Mada zilizojadiliwa

  •  Kukuza uelewa wa umm kuhusu maadili ya utumishi wa umma.
  •  Utekelezaji, usimamizi na kutathimini sera za maendeleo katika ngazi zote katika utaratibu mzuri.

 MWAKA 2012

Tuliendelea kutekeleza hii Program kwenye kata za Kisarawe, mafizi, Kurui, Vihingo, Mkamba, Bupu na Shungubweni.

Kwa kutumia mbinu zifuatazo:-

a)            Mikutano ya hadhara na mijadala.

b)            Warsha na semina

d)            Kugawa vitabu mbalimbali vya sera.

 

MWAKA 2013

Tuliendesha mafunzo juu ya kukuza uelewa wa umma kuhusu maadili ya mtumishi. Ili jamii iweze kupata huduma ilivyo bora na kwa wakati.

Tuliendesha mafunzo kwa viongozi na watendaji wa Wilaya ya Kisarawe. Juu ya kukuza uelewa wa umma kuhusu maadili ya mtumishi wa umma ili jamii iweze kupata huduma iliyo bora na kwa wakati.

Mafunzo haya yaliendeshwa na wataalam toa

i)             Ofisi ya Rais Utumishi

ii)            ofisi ya Rais Maadili ya Viongozi wa umma.

 

MWAKA 2014

Kwa kukuza uelewa wa umma kuhusu maadili ya utumishi wa umma na wananchi kupata huduma iliyo bora. Tulitoa mafunzo kwa wananchi wa Wilaya ya Ilala kutambua vipimo halisi na sahihi viavyopaswa kutumika wakati wa ununuzi na minzani ya kupimia. (Haya mafunzo na mkakati wa Asasi kutekeleza makubaliano ya Guluka Kwalala Youth Environment Group na OR –MUU.

 

 



Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles