Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

PLANET SOCIAL DEVELOPMENT(PSD) updated its Projects page.

$
0
0
PSD is now operating in Simiyu region with sports teachers and school children. The organization calls upon organizations and cbo's with similar goals to join hands in gearing social development in this young region

 

MAFUNZO YA MPIRA WA KIKAPU KWA VIJANA NA WATOTO YANAENDELEA JIJINI MWANZA

Mafunzo ya mpira wa kikapu kwa watoto na vijana yanafanyika katika uwanja wa kanisa katoliki Nyakahoja jijini Mwanza kwa siku za jumatatu na jumatano kuanzia saa 9:00 alasiri na siku ya jumamosi kuanzia saa 2 asubuhi. Mafunzo haya yanaandaliwa na kusimamiwa na Shirika la kijamii la Planet Social development (PSD) la jijini Mwanza pamoja na Chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Mwanza (MRBA) kupitia kamisheni ya watoto vijana na maendeleo na shule kwa kushirikiana na mlezi wa watoto na vijana (MRBA) ndg. Altaf Hirani Mansoor yanajumuisha watoto na vijana mbalimbali kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari za Jijini mwanza.

Planet Social Development (PSD) ni shirika la kijamii la hapa mkoani Mwanza linalojishugulisha na shughuli mbalimbali za kuendesha na kusimamia mafunzo mbalimbali ya michezo kwa watoto, vijana na walimu wa michezo.

Mafunzo haya yanaendeshwa na kusimamiwa na PSD na MRBA kupitia makocha na pia wachezaji wazoefu wa mchezo huu hapa mkoani Mwanza yana malengo yafuatayo hapa chini.

  1. Kuibua vipaji na jinsi ya kuviendeleza katika kusaidia maendeleo ya mchezo huu hapa mkoani Mwanza na Tanzania kwa ujumla ambao ni wito wa MRBA na Serikali kwa ujumla wa kutaka watoto na vijana wakishiriki katika michezo.
  2. Watoto na vijana hawa wanapata nafasi ya kujenga miili yao kiakili na kimwili (mentally & physically) wanaposhiriki katika mazoezi mbalimbali.
  3. Watoto na vijana hawa wanapata nafasi ya kukutana na wenzao kutoka shule mbalimbali na kujifunza mambo mbalimbali miongoni mwao.
  4. Kupitia michezo watoto na vijana wanaoshiriki wanapata elimu ya jinsi ya kupata nafasi ya kwenda kusoma katika shule na vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kutakiwa kusoma na kufaulu masomo yao vizuri na pia kufanya mazoezi kwa bidii ili waweze kuwa mchezaji wazuri (scholarship program).
  5. Kutoa nafasi kwa mashirika mengine ya kijamii ambayo hujishugulisha na utoaji wa elimu ya makuzi kwa watoto na vijana na kuwaelimisha katika kuzifahamu haki za mtoto katika kujifunza.
  6. Kutoa nafasi kwa walimu wa michezo kuwatambua wanafunzi wao ili waweze kuwatumia katika kuunda timu za shule katika mashindano ya shule katika ngazi za kata, wilaya, mkoa na taifa (umitashumta na umisseta).
  7. Kutoa nafasi kwa makocha wa mchezo huu hapa mwanza katika kujifunza namna ya kuendesha mafunzo kama haya kwa timu zao katika maeneo mbalimbali hapa mkoani.
  8. Kuendeleza mafunzo ya mpira wa kikapu tuliyoyaanzisha hapa jijini Mwanza October 2011 kwa kushirikiana na Mambo Basketball kutoka Dar es Salaam yaliyokuwa na lengo la kuwatayarisha vijana kwa ajili ya kambi ya mafunzo ya mpira wa kikapu itakayofanyika mwezi wa june 2012 kwa kushirikiana na kocha wa Basketball program ya Memorial Newfound University kutoka Canada .
  9. Kuendeleza na kutekeleza mafunzo tuliyojifunza wakati tulipohudhuria mafunzo ya ukocha wa mpira wa kikapu kwa watoto na vijana nchini Marekani mwaka 2009 kama US Sports program Alumni yaliyogharamiwa na Ubalozi wa Marekani – Tanzania kupitia US Sports program .

Pamoja na hayo hapo juu PSD na MRBA inaomba wadau mbalimbali wajitokeze kuweza kusaidia mpango huu endelevu wa kufundisha vijanakwa kusaidia vifaa mbalimbali vya kufundishia hasa mipira pia tunatoa rai kwa wazazi na walimu wawaruhusu na kuwelekeza watoto na vijana hawa kufika uwanjani kwa siku tajwa ili tuweze kuendeleza vipaji vya watoto hawa na kuinua kiwango cha mchezo huu hapa mkoani na Tanzania kwa ujumla.

Imetolewa.

 

Kizito Bahati

Mratibu wa mafunzo

kizitobahati@yahoo.com

http:// www.envaya.org/psd

                                        


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles