1.1. Historia ya Greenlbelt Schools Trust Fund
GSTF ni kikundi cha wakazi wa Morogoro wanaotoka katika jamii ya kawaida ambao wanakumbana na kero mbalimbali zinazo kwamisha maendeleo ya jamii. GSTF ni kifupi cha Green Belt Schools Trust Fund. Hii ni asasi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa Januari 2000 na kupata usajili tarehe 27/07/2000 chini ya sheria “Trustee Incorporation Ordinance Cap.375 na kupata cheti cha usajili Na. T. 1.8 kwa madhumuni yakuwasaidia watoto wa kipato cha chini kupata elimu kwa gharama nafuu zaidi, kuhamasisha jamii kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa, usimamizi wa rasilimali za umma, kufanya utafiti wa kupunguza umaskini wa kipato kwa jamii, ushawishi na utetezi wa sera za Taifa na kuelimisha jamii pamoja na viongozi wa serikali za mitaa kuhusu misingi ya utawala bora, demokrasia na haki za binadamu. Ofisi kuu ya GSTF ipo Morogoro mjini katika jengo la CCM Mkoa. Asasi hii pia inatawi la chuo cha Greenbelt Polytechnic College (GPC). Pamoja na kupanuka asasi hii, shughuli zake zimekuwa zinategemea sana ufadhili toka kwa wafadhili mbalimbali. GSTF ni asasi ya kujitolea, haina udini, si ya kisiasa na haina lengo la kugawana faida itokanayo na shughuli zake, ina ujuzi na uzoefu wa kutekeleza miradi mingi inayoombewa ufadhili.
DIRA (VISION) ya GSTF ni Kuimarisha Thamani Ya Mtu Katika Kupata Mabadiliko Ya Tabia Na Kupunguza Umasikini Na Dhuruma Ya Jamii Kama Msingi Wa Amani (To Strengthening Human Values In Achieving Behavioral Change And Reducing Poverty And Social Injustice As Foundation For Peace).
DHAMIRA (MISSION) ya GSTF ni Kutoa Elimu na Mahitaji Yake, Ushauri Na Usimamizi Wa Miradi, Ushauri Mtambuka Katika Jamii Hitaji Kwa Misingi Ya Kuimarisha Utawala Bora, Demokrasia, Umoja, Amani, Ubunifu Na Utunzaji Mazingira. (To Provide Education And Educational Needy Offers Consultancy Services Of