Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

TAWI LA CHAVITA MTWARA created a Home page.

$
0
0

MADHUMUNI YA CHAVITA MTWARA NI PAMOJA NA:-

1. Kufanya shughuli zote zinazohusu Viziwi,Kutoa huduma na kuandaa mikakati mbalimbali kwa manufaa ya Viziwi.

2.Kuwaunganisha na kuelimisha Viziwi ili wapate hali bora ya maisha,huduma muhimu kama vile Raia wengine wa Nchi

3. Kupigania haki na usawa,ushirikiano na jumuia zingine,vyombo vya Serikali na mashirika mbalimbali yenye lengo sawasawa na Chama chetu

4. Kushirikiana na Matawi mengine moja kwa moja au kupitia Chama cha Viziwi Tanzania

5. Kufanikisha malengo ya CHAVITA

6. Kulinda na kuheshimu Katiba ya CHAVITA

7. Kuhakikisha matumizi sahihi ya Lugha ya Alama yanapewa kipaumbele na kutumiwa ipasavyo kwa Viziwi wote na Wakalimani katika Matawi. Hivyo Matawi yatabuni mbinu mbalimbali za kuboresha na kukuza matumizi ya Lugha ya Alama. pia kushirikiana na CHAVITA Makao Makuu ili kuweka mikakati ya kupata Wakalimani bora wenye uwezo wa kuwaunganisha Viziwi na Watu wengine wanaosikia

8. Kukusanya takwimu sahihi za Viziwi waliopo kwenye Matawi(Mikoa/Wilaya) zao kwa kushirikiana na Ofisi za Vingozi wa Serikali za Mitaa.

 

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles