Quantcast
Channel: Envaya: Latest updates
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

UNITED AFRICANS updated its Projects page.

$
0
0

Shirika baada ya kupata nguvukazi (Wanachama Watendakazi) katika nchi na mikoa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Tanzania mikoa ya Rukwa, Tabora, Katavi na Kigoma, Wanachama Waliofuzu Mafunzo ya Kazi kwa nadharia na wengine Mafunzo ya kazi kwa vitendo ngazi ya mkoa, limekwishaanza kuwapeleka maeneo ya kazi na wengine maeneo ya Mafunzo ya Kazi kwa vitendo katika nchi na mikoa mbalimbali barani Afrika.

Nchini Tanzania mkoani Dar Es Salaam baada ya Shirika kushirikiana na mamlaka za Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa  mkoani humo kuanzia ngazi ya mkoa hadi mtaa, baada ya kupata Wakuu na Makatibu Watendaji wa Shirika ngazi ya wilaya, linatoa wito kwa wananchi wote kujiunga na kuunda Kamati za Uongozi ngazi za Mitaa katika wilaya za Ilala, Kinondoni, Temeke na Kigamboni. Idadi inayotakiwa ni Wajumbe 11 ili kufanya Kamati kuwa na jumla ya Wajumbe 12 akiwemo Katibu Mtendaji wa kuajiriwa.

Hivyo baada ya Wajumbe kupatikana, nafasi ya Katibu Mtendaji wa Mtaa hutangazwa kwa vijana na wastaafu wenye Elimu ya kidato cha nne na kuendelea wenye ujuzi wa kutumia kompyuta walioupata katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali.

Wajibu wa Kamati ni kusajili wanachama wa Shirika, Kusimamia wajibu na kutoa haki kwa Wanachama, kutunza na kusimamia Mali za Shirika; kubuni na kusimamia miradi, kupokea na kugawa misaada kwa walengwa; kuwapokea na kuwatunza wageni wa shirika,kuhamasisha na kuelimisha Wanajamii kujua sheria, wajibu na haki zao za msingi katika jamii; kutunga Sheria na Kanuni ndogo ndogo, kuunda vikundi vidogo vidogo, kuhakikisha na kutoa taarifa za usalama wa wananchi na mali zao katika maeneo yao kwa kuzipeleka kwenye vyombo vya usalama.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4212

Trending Articles